Biashara ya Kununua na Kuuza Mazao (nafaka): Jifunze Mbinu za Kuanzisha na Kusimamia

Ubarikiwe sana kwa mchango wako mzuri!
 
Biashara ya nafaka inalipa sana, endapo kama unausafiri wa kusafirisha hizo bidhaa. Mchele, nafaka kama maharage, mbaazi, kunde, choroko, Dengu nzima pamoja na njugu mawe. Zinalipa sana kwa utapata wateja wa mashuleni hasa hiz private school [emoji120]
 
kama vipi hii biashara bado inalipa hapa dar
 
Japo hii comment ni ya miaka miwili iliyopita, sio mbaya niikijibu kwakua member bado yupo active.

Mkuu ulizungumza kirahisi sana, kuuza tani 10 mara nne ndani ya mwezi mmoja inahitaji soko kubwa sana, vinginevyo utakaa na hizo tani zako mida mrefu kabla haijafata mzigo mwingine.
 

Mtaji ina range kiasi gani mkuu
 
HHay
Hiyo mikoa tajwa mahindi yake ni mazito!
 
Tupe mawasiliano Yako tafadhali
 
Habari za jioni ndugu , naomba mtu ambae ni mzoefu na hii biashara ya kununua na kuuza nafaka hasa mchele (kutoa mikoani) ambae anaifanya hapa Dar es salaam. nahitaji anipatie muongozo na utaratibu mzima wa kuanza lkn itapendeza zaidi tukawasilian 0673117224
 
Hii biashara ya nafaka asikudanganye mtu kuwa inalipa halafu ukaingia kichwakichwa sitosahau kilichokanikuta tandika, nilileta sampo ya choroko madalali wakaniambia choroko safi sana wewe zilete tu basi nikajichanganya nikakusanya tani 30 Kilwa vijijinii nikasafirisha kwa mbwembwe kupeleka Dar wale madalali nilipowapa taarifa kuwa niko njiani wakaniambia wewe zilete tu.

Tumeingia Dar asubuh ya Jumamos dalali ananiambia muhindi kasafiri ila Jumatatu anarudi na atazichukua zote hizi kwa 1200 kwa kilo na wakati huo mimi nilinunua kwa 600 nikajiona nishakuwa tajiri,nilikuwa na laki 3 nikaamua kuponda raha na watoto wazuri kwakuamini jumatatu naikunja hela yangu aiseee laiti ningejua.

Kiukweli Jumatatu ikafika nikamstua dalali twende basi kwa Muhindi akaniambia Muhindi hanunui tena kiukweli nilipagawa sana nikamuuliza nani sasa ananunua akaniambia hamna anayenunua kama vipi nichukue sampuli nipite natembeza kwenye masoko. Aisee nilitembeza masoko yote Dar kwa wiki mzima hata mmoja aliechukua nikaenda sehemu fulani nikakaa nikaanza kulia kilio cha chinichini na mfukoni nina kama elfu 20 tu ghafla napokea simu mwenye store anaitaka store yake kuna mzigo anataka kuuweka, baadae mtu fulani akanihurumia akaniunganisha na tajiri yupo dodoma yule jamaa alinunua zote kwa bei ya 1270.
 
Ukianza sasa hutaanzia chini bali utaanzia kwenye elimu na uzoefu ulipota kutokana na tukio hilo.

Hongera sana mkuu
 
Vipi mkuu samahani!,, ulifanikiwa kuanza hii biashara??
 
Ukajiona ushakuwa tajiri bonge la Businessman na ukaanza kutafuta watoto warembo,ogopa sana madalali[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]
 
Ukajiona ushakuwa tajiri bonge la Businessman na ukaanza kutafuta watoto warembo,ogopa sana madalali[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]
Yeye alikosea mzigo kama choroko hakuna haja ya dalali maana wateja wanafahamika ni wahindi,,angetakiwa kutembelea magodown wa wahindi kama kina Afrisian achukue namba anakua anapiga tu akihitaji kuleta mzigo,,,
 
Nimekuelewa sana ndg yangu wa choroko kisa kama hiki kilinikuta solo la mmbande dalali kaniambia nipeleke pilipili mwendo Kasi idadi yeyote ndoo kubwa sh 40,000 nikakopa mpaka nauli kufika na ndoo 10 dalali anasema hazijaiva vizuri hakuna biashara nikaanzq kuzunguka kila genge kuuza kidogokidogo kumbe wote wamoja,mwisho nikamwangukia dalali yuleyule akachukua kwa 10,000 kwa ndoo nikaapa kutorudia makosa madalali ni pasua bichwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…