Kwanza kabla ya yote USIACHE KAZI,
Usiepuke kutembea masaa mawili kwa siku,
Ipende kazi yako,
Biashara ya Nafaka kwasasa sio nyepesi kama unavyoifikilia(sikukatishi tamaa nakupa ukweli) nafaka zipo nyingi sana mtaani kwa sababu ya mipaka kufungwa,
Bei yake sio nzuri sana, faida ni 100, 200 mpaka 300 kwa kilo.
Ukichukua fremu utakula hasara takatifu
Bei ya mzani mpya ni Tsh 150000 used laki mpaka laki na ishirini,
Kwa mtaji huo wa laki nne nakushauri ufanye yafuatayo
Tafuta kituo cha dala dala wanaposhukia watu wengi penye genge la mboga mboga (kwenye mikusanyiko ya watu wengi eneo liwe la mtaani).
Nunua kilo 50 za maharage ya njano kwa bei rahisi, kilo 50 za soya kilo 50 za mchele (ongezea pesa) kisha nenda katege hapo pembeni kwa wauza mboga kaa hapo uuze,
Mara nyingi wateja wanakujaga asubuhi na jioni mchana huwa ni wachache, uza kwa bei rahisi bandika viboksi vyenye bei ili wateja waone wanapopita maeneo hayo,
Mengine utajifunza ukishaanza biashara
NB usikodi fremu, nitaleta uzi kueleza jinsi hii biashara ilivyonipiga za uso kwa kukimbilia kupanga kwenye fremu.
Sent from my SM-A107F using
JamiiForums mobile app