Biashara ya Kupasua Kokoto-Morogoro au Dodoma

Lambardi

Platinum Member
Joined
Feb 7, 2008
Posts
18,813
Reaction score
21,830
Wana JF heshima mbele,
Naomba kujua alie na upeo wa bishara ya kupasua kokoto kati ya Morogoro au dodoma..wapi pazuri na biashara yenyewe kwa ujumla na maeneo mazuri kwa kufunga mashine!

Nawasilisha
 
Nadhani Dodoma kuna projects za ujenzi nyingi zaidi kuliko Morogoro.
 
Nasikia Iringa na Songea wanakuja hadi Moro kupata kokoto!ni kweli Dodoma kuna ujenzi zaidi....
 
Wana JF heshima mbele,
Naomba kujua alie na upeo wa bishara ya kupasua kokoto kati ya Morogoro au dodoma..wapi pazuri na biashara yenyewe kwa ujumla na maeneo mazuri kwa kufunga mashine!

Nawasilisha

Kwanza kabisa hongera kwa kutaka kuwekeza kwenye sector hiyo ya ujenzi. Ila binafsi nilikua natafuta mashine za kusaga na kutengeneza kokoto na mashine ya kuyeyusha scraper na kutengeneza nondo kwa ajili ya ujenzi. Ninataka kujua upatikanaji wake, bei zake, gurantee, shipping charges etc. Kama una maujuzi yeyote tujuzane mkuu. Ntashukuru sana.

Barikiwa !!
 

Mkuu heshima Mbele,
Naona tuna interest sawa,bei iko juu kidogo hasa kwa sisi wajasiliamali wadogo google hawa ZENITH MININING & CONSTRUCTION MACHINERY LTD kwa bei ya machine za tani ndogo zaidi 40-60 Ton Per Hour inafika 200mil hadi hapa Tanzania...full set machines.

Kiwanda cha kuyeyusha nondo sijafanya utafiti ila ni gharama zaidi maana hata umeme wake ni balaaa sana!
 
Wana JF heshima mbele,
Naomba kujua alie na upeo wa bishara ya kupasua kokoto kati ya Morogoro au dodoma..wapi pazuri na biashara yenyewe kwa ujumla na maeneo mazuri kwa kufunga mashine!

Nawasilisha

mkuu hongera sana kwa wazo hili zuri, nami pia nimekua nikifikiri sana kuhusu buashara hii nadhani moro ni pazuri, vipi hauhitaji partners?
 

vipi kuhusu matumizi ya umeme kwa mashine za kokoto?
 

Kuna kampuni flan nimecheck nao hawa majamaa wako china nikawasiliana nao na waka share vitu vingi na mimi. Wacheck www.amecco.com

(walikuja kufanya maonyesho yao officially hapa Tanzania kwenye sabasaba event, wanatambulika hata serikalini, walinipatia catalogue ya makampuni yao mbali mbali yaliyoko china yanayo deal katika sector tofauti tofauti wakanambia pia yakua hata detail za makampuni yao yapo kwenye ubalozi wao hapa nchini so sio wababaishaji.

Swala la umeme ndio challenge moja wapo kubwa sana cz kuna watu on this industry wenye mitaji mikubwa na wanajielewa sana.
 
Jami kuna yeyote alifanikiwa kuanzisha hii biashara ya kupasua kokoto atujuze kama inalipa au la
 
Hongera kwa wazo Zuri!
Dodoma Ni sahihi zaidi, kiukweli tuna uelekeo unaofana.
nilikuwa India Julai kwa swala Hilo kuna Kiwanda nilitembelea wako vizuri Mno. Tulifanya mazungumzo niki import Jaw crusher mbili wanaweza kuanzinmsha Agency relationship.
Kuhusu Chuma Nimeanza na Foundry workshop iko Arusha Nikiwa na elekea kwenye Chuma. Ukiwa na Muda Ni PM.
Currently Niko Dar.
 
Wadau mmepotelea wapi? I'm have a very good Idea regarding construction industry any one who have similar interests let us talk business.
 
Nani nlivutiwa na hii business wiki iliyipita nimenunua eneo takribani ekari 6 lote limejaa mawe hivyo nkawaza vipi ntaanzisha kiwanda cha kuzalisha kokoto na juu ya upatikanaji wa machine ikiwemo bei na changamoto zlizomo kwenye hii project tunaomba mtujuze nyie ambao mmedhubutu nasi tujumuike katika kulijenga taifa letu kwa kukuza viwanda..
 
Jamani, tunaomba mrejesho wale walofanikiwa kuanzisha hii biashara
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…