Biashara ya kusafirisha abiria

Hamisi Mhoja

Member
Joined
Nov 22, 2019
Posts
22
Reaction score
23
Jamani naomba ushauri kuhusu biashara ya kusafirisha abiria nilkuwa na mpango wa kununua hiace ambayo ni used nasikia Dar kuna yard zinauza hiace used.

Basi naomba ukweli kuhusu hili la hizi hiace kama zipo na bei zake, na kingine je hii biashara inalipa?

Nipo Bukoba Vijiijini, Nimeweka picha



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Da, nikiona hii kitu nakumbuka mjomba wangu masahibu aliyopitia na kuupata uzee wa ghafla sambamba na magonjwa tere. Sijui niseme bahati nayo huchangia au vipi.

ok anyway mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni biashara nzuri ila madereva pasua kichwa. Ukiwa nazo mbili utaifurahia hii biashara zaidi.
 
Hii biashara ni nzur endapo utapata sehemu sahihi ya kufanyia na ukapata watu sahihi wa kuwaajir na sehem ya mwisho mafund sahihi wa ku repear pind chombo kikiharibika.Pia jitahid sana kukijua chombo usiwe mtu wa kuelezewa tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna biashara ngumu kama hii, labda kama unasimamia mwenyewe kidogoooooo afadhali. Ila ni biashara ya kijinga sana. Maana trafikii, sumatra, sijui euwra mara ujinga mtupu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
biashara inalipa na inaweza kukukata kutokana na eneo utakspofanyia hiyo biashara,usimamizi na utunzaji wa chombo pamoja na dereva utakayempata maana yeye ndio atahusika na swala zima la utunzaji,lakini biashara ya usafirishaji abiria inalipa sana kama ukiwa makini nayo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…