Biashara ya kusafirisha matunda Ulaya

Wakuu,tujuzeni soko la nje ya Tanzania kwa mazao ya matunda kutoka kanda ya kati yenye matunda mengi ya ubuyu na zabibu

Kwa zabibu wenyewe wanalima sana huko kwa hiyo kupata soko ulaya ni kazi labda within Africa na ubuyu kwa kweli sina uhakika ila huwa naona kwenye maduka ya wahindi
 
Kwa zabibu wenyewe wanalima sana huko kwa hiyo kupata soko ulaya ni kazi labda within Africa na ubuyu kwa kweli sina uhakika ila huwa naona kwenye maduka ya wahindi

Sisi tumeanza na kutafuta ubora wa bidhaa. Tumeanza na Ujenzi wa Greenhouses, mabwawa ya samaki, ufugaji ng'ombe na Kuku pamoja na ufugaji nyuki. Lengo ni kutosheleza kwanza soko la ndani viwandani na migodini. Baada ya hapo, tutataanza kuuza Nje. Tupo katika hatua za mwanzo. Hatua elfu huanza na moja. Tumethubutu na tutaweza.
Tusaidieni mliopo Nje. Tupeni masoko tutayamudu. Bofya: www.ujasirimali.blogspot.com
 
Nashangaa ndizi nyingi ( Matoke ) zinazouzwa Uingereza pia Marekani zinatoka Mbarara,Uganda.

Tanzania vip atulimi ndizi?
 
mfano halisi ni bakheresa
Naomba kusahihishwa kama mimi ndio sielewi... Hivi Bakheresa ana-export any genuine food product or processed product into the developed world? Ninachojua ni kwamba yeye amefocus on the bottom of the pyramid ie the cost driven market. Ndio maana anatununulia processed coconut cream Thai anatugawia kiduchu kiduchu ambavyo size amnazo wao hawafungi ili japo mia tano ipate kazi siku ziende. Haya juoce zake haziendi popote nje ya Africa.

Najua Arusha kuna company zina-export mbogamboga ulaya. Most wanalima wenyewe na pia wanaingia mikataba na wakulima wadogowadogo. Juzi nilipita sehemu nikakuta mzigo wa reject baby beans... Aisee zinavuto kidogo niombe nichambue japo sado moja nipeleke home... ukweli viwango viko juu na kwa ubabaishaji wetu wabongo hilo nalo lonaleta changamoto. Ningetamani sana niwe proven wrong... Inalipa sema nani anaweza kukomaa hadi akidhi masharti?
 
kuna ndizi nyingi uganda kuliko bukoba/tz kwasababu ugana is more equatorial than tz na kuna mvua nyingi sana. hivyo, ndizi chache za bukoba hizo hazijafikia nyingi za uganda.
 
Nenda Wizara ya Kilimo kitengo ch Afya ya mimea, plant Quarantine and Phytosanitary services watakupa taratibu zote za kufuata kuanza biashara hii
 
Kaka hiyo kitu inafanyika na baadhi ya watu. Kuna mzungu mmoja aliyefukuzwa na Mugabe yuko huko wilaya ya Rungwe. Nadhani ana kitu kinaitwa Rungwe Avocado Company. Hata uki google utapata taarifa zake. Huyo jamaa anasafirisha parachichi kwenda ng'ambo. Lakini shida si tunda tu. Kuna ugumu wa ganda ili liweze kustahimili rabsha za kusafirisha pasipo kuharibika.
 

Naomba tugawane majukumu.naomba utafute taarifa juu ya taratibu za kuingiza matunda uingereza zinazohusu ubora,kodi na masoko hapo uingereza mimi nitafuatilia taratibu za hapa tanzania kusafirisha haya mazao Tanzania mpaka kufika huko UK.
Muda ni wiki mbili toka sasa.Je,utaweza?Mimi naweza.
Huu ni wakati wa kuchukua hatua na sio kulalamika.
 

Samahani mkuu naomba utujuze taratibu za kufuata ili uuze bidhaa za matunda na kilimo nchini India.
Natanguliza shukrani.
 
mkuu mm nimetoa mfano tu ila kama wewe unao unawafahamu nambie usijali

 
mkuu itakuwa ni vyema mkkinishirikisha na mie
 
aksante ngoja nianze mchakato wa kutafuta hizo taarifa nizilete tuone tunafanyaje wakuu
Hamna tatizo unakaribishwa na wewe kutoa mchango wako wa kutafuta taarifa kuhusu hii fursa.
Baada ya wiki mbili utaleta ulichopata na mimi nitaleta za kwangu.
 
mkuu mm nimetoa mfano tu ila kama wewe unao unawafahamu nambie usijali

Wewe uko pande za wapi? Kama uko A-town kuna kampuni kama Serengeti veggies Ngaramtoni, nyingine iko Chekereni na Usa River wanaexport vitu tofauti including mboga na matunda. Pia zote zinalima kwa mikataba na wakulima wadogo ili kufit quotas perhaps na demand.

Mwisho wa hadithi pita TAHA (uzunguni jirani na Anglican church) watakupa requirements na ushauri juu ya mazao ya export, requirements na hata program zao za kuwezesha akina sie.
 
mkuu mm nimetoa mfano tu ila kama wewe unao unawafahamu nambie usijali

Labda niseme pia naamini njia nzuri ya kujifunza viwango ni kwa kulima na hayo makampuni ambayo tayari yana soko la export. Hapo watakufundisha ubora wanaoutaka na jinsi ya wewe kuproduce/kulima at that level. In my opinion hapo risk ni ndogo wakati unajifunza full speed.

Ukiwa tayari kutafuta mashamba ya kukodi au ku-buy pia nishtue nikudalale (-;
 

unaweza tutajia matunda wanayo export? ni kweli kuna soko nje ika ukweli ni kwamba ku export sio ishu ya kitoto hata siku moja. kenya wanafanikiwa kwa sababu ya usafiri wa anga ambapo ndege zao KQ zinaruka hadi Ulaya, kwa Bongo ukilima it means uwe na magari ya kubeba hadi Nairobi ndo upandishe kwenye ndege hapo ndo kuna changamoto na kwa wakulima wadogo kwa kweli ni ngumu sana tena mno.
Kuuza mboga hasa ulaya kutakuwa na maana endapo usafiri wa anga utaboreshwa sasa mfano Kia inatua KLM pekee na Ethiopoia na Uholanzi ndo kwao na matunda.
Na makampuni.mengi wanatumia uwanja wa Jomo Kenyata.
 
Na changamoto nyingine kwa sasa ni Baada ya RUSSIA kuweka vikwazo Ulaya kiasi kwamba Wakulima.wa mboga na matunda Ulaya hawana pa kuyapeleka nchi kama POLAND kiongozi wa kuzalisha Aple Duniani hana pa kupelekea Aple zake na namliloa USA anunue,

Kwa hiyo ndugu zangu kuna changamoto si ya kitoto kuweza kuuza mboga na matunda ulaya.
 
unaweza tutajia matunda wanayo .... wanatumia uwanja wa Jomo Kenyata.

Mkuu Chasha... Nilikutafuta kule kwenye thread yako ya maonyesho ya kilimo Kenya. Ulifanikiwa kwenda? Can you share anything toka huko...?

Back to topic: matunda kama strawberries, grapes, apples za kusini, na mboga kama capsicum (hoho), green beans, baby corn, etc ndio nimeshuhudia yakilimwa na extension farmers. Pia maua fulani fulani ya muda mfupi nayo wanalima kwa mikataba maalum ya wao kukuelekeza, kukupatia mbegu na pembejeo halafu unawauZia wao tu. Hizo bidhaa zinaelekwa UK etc kwenye maduka kama Tesco nk.

Again in this arrangement mtu anafunzwa at limited risk kwake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…