Wakuu naomba ushauri wenu.
Nimekuwa nitembelea maduka mbali mbali katika nchi za Ulaya hasa UK na kukuta bidhaa kazaa za kutoka Uganda na Kenya lakini sijawahi kuona bidhaa zozote kutoka Tanzania katika maduka ya UK. Nikiwa Tanzania naona kuna matunda mengi kama Machungwa, Mahembe, Nanasi, Mapalachichi, nk zimerundikwa tu barabarani na vinauzwa kwa bei ya chini sana kulinganisha na bei ya Ulaya. Je kwa nini Watanzania hatuna akili ya kuweza kupeleka hivi vitu Ulaya na kupata soko zuri.
Mimi napenda sana ndizi Bukoba na huwa nazipata kwa urahisi sana katika Maduka ya UK zikiwa zina nembo ya (Product of Uganda). Hawa jamaa wananunua ndizi hata kutoka Bukoba na Karagwe. Sisi kwa nini tusifanye hivyo tena kutoka hata Mbeya? Waganda wanauza majimbi, viazi na hata nyanya chungu katika soko la Ulaya. Sisi tumelogwa?
Wakenya wametawala soko la maua, sisi kwa nini hatuwezi?
Naomba mawazo yenu