Biashara ya kusafirisha matunda Ulaya

Biashara ya kusafirisha matunda Ulaya

Kagalala

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2010
Posts
2,403
Reaction score
1,133
Wakuu naomba ushauri wenu.

Nimekuwa nitembelea maduka mbali mbali katika nchi za Ulaya hasa UK na kukuta bidhaa kazaa za kutoka Uganda na Kenya lakini sijawahi kuona bidhaa zozote kutoka Tanzania katika maduka ya UK. Nikiwa Tanzania naona kuna matunda mengi kama Machungwa, Mahembe, Nanasi, Mapalachichi, nk zimerundikwa tu barabarani na vinauzwa kwa bei ya chini sana kulinganisha na bei ya Ulaya.

Je kwa nini Watanzania hatuna akili ya kuweza kupeleka hivi vitu Ulaya na kupata soko zuri.

Mimi napenda sana ndizi Bukoba na huwa nazipata kwa urahisi sana katika Maduka ya UK zikiwa zina nembo ya (Product of Uganda). Hawa jamaa wananunua ndizi hata kutoka Bukoba na Karagwe. Sisi kwa nini tusifanye hivyo tena kutoka hata Mbeya? Waganda wanauza majimbi, viazi na hata nyanya chungu katika soko la Ulaya. Sisi tumelogwa?

Wakenya wametawala soko la maua, sisi kwa nini hatuwezi?
Naomba mawazo yenu
 
Mtafute balozi wa amani anaitwa risasi mwaulanga alisema atatoa elimu kuhusiana na hiyo kitu.
 
ww si uanza sasa.........maana hyo ndo opportunity yenyewe..........

Mimi nilishaanza lakini kwa bidhaa zingine ambazo nyingi naleta Tanzania, ila naona hili linanigusa kwa nini wenzetu wameweza sisi tunashindwa.
 
Kwasababu nchi yetu imejaa watu kama wewe wasio na dynamism and initiative.
 
Wengi wetu wanaogopa ushuru unaotozwa na complexities za uzalishaji wa bidhaa zenye viwango vinavyohitajika huko.
Yaan hata baada ya ile mipango ya AGOA na ... inayoturuhusu kuuza bidhaa njebila vikwazo vyovyote (hasa Marekani na Ulaya) kuanzishwa bado mwitikio ni mdogo ukilinganisha na wenzetu wa Kenya na Uganda.

Nadhani Mamlaka zinazohusika kama BET, TIC, MITM, ..bado hazijatoa elimu ya kutosha kwa wajasiriamali wetu. Hata BDSP (kama AMKA) nao wanahusika kwan sector hii bado ipo nyuma sana ukilinganisha na wenzetu wa Kenya na Uganda.

Cha msingi kwa sasa ni kuanza personally pale unapoona fursa
 
niliona mlolongo wa mpaka kuuza embe UK nikaona ni bora niangalie soko la ndani tu
Mkuu usiseme mlolongo ni taratibu waliojiwekea kuhakikisha bidhaa inayoingia soko lao imekidhi ubora.

Don't give up so easily Narubongo try harder this time,Am sure you will get there.
 
Mkuu kama wakenya na waganda wameweza na wewe unakutana nao join now wakupe mbinu zilete kwa Watz ili waweze kufika hapo tatizo kubwa la watz wengi walikosa exposure tofauti wa nchi jirani.Wewe umepata hicho kitu rudi saidia watz wenzako saidia nchi yako wote kwa pa1 tutasonga mbele.
 
Kaka observations zako ni nzuri tu sana, lakini inatia shaka kama wewe ni mfanyabiashara unayeingiza bidhaa kutoka UK kuja TZ una nafasi nzuri zaidi ya kuchukua bidhaa TZ na kupeleka UK, kwa nini usifanye uchunguzi wa kutosha na kutuletea hapa ripoti kamili ya bidhaa zinazohitajika, kiasi gani zinauzwa kkule, gharama ya nauli na ushuru mwingine, taratibu kamili na vitu kama hivyo. Sisi wengine ni wakulima tu kaka, maisha yetu yote mashambani, nyie mnaokwendakwenda huko duniani ndy mnatakiwa mtupe mwanga kidogo ili tutumie hizo fursa!
 
Wakuu naomba ushauri wenu.
Nimekuwa nitembelea maduka mbali mbali katika nchi za Ulaya hasa UK na kukuta bidhaa kazaa za kutoka Uganda na Kenya lakini sijawahi kuona bidhaa zozote kutoka Tanzania katika maduka ya UK. Nikiwa Tanzania naona kuna matunda mengi kama Machungwa, Mahembe, Nanasi, Mapalachichi, nk zimerundikwa tu barabarani na vinauzwa kwa bei ya chini sana kulinganisha na bei ya Ulaya. Je kwa nini Watanzania hatuna akili ya kuweza kupeleka hivi vitu Ulaya na kupata soko zuri.
Mimi napenda sana ndizi Bukoba na huwa nazipata kwa urahisi sana katika Maduka ya UK zikiwa zina nembo ya (Product of Uganda). Hawa jamaa wananunua ndizi hata kutoka Bukoba na Karagwe. Sisi kwa nini tusifanye hivyo tena kutoka hata Mbeya? Waganda wanauza majimbi, viazi na hata nyanya chungu katika soko la Ulaya. Sisi tumelogwa?
Wakenya wametawala soko la maua, sisi kwa nini hatuwezi?
Naomba mawazo yenu
Quality matters! unayoona mtaani unatakiwa na yale unayoyaaona UK! Matunda si kununua tu na kusafirsha lazima yatunzwe ili hata mnunuaji afurahi, sisi hapa hayo hatuangalii, ndo maana hata ya mtahani hayo kuyanunua pia hayatamaniki. Matunda yetu hayamwagiwi dawa hivyo utakuta mengi ya midoa kibao. sasa utachagua mpaka lini upate mazuri ya kusafirisha_
 
wakuu naomba ushauri wenu.
Nimekuwa nitembelea maduka mbali mbali katika nchi za ulaya hasa uk na kukuta bidhaa kazaa za kutoka uganda na kenya lakini sijawahi kuona bidhaa zozote kutoka tanzania katika maduka ya uk. Nikiwa tanzania naona kuna matunda mengi kama machungwa, mahembe, nanasi, mapalachichi, nk zimerundikwa tu barabarani na vinauzwa kwa bei ya chini sana kulinganisha na bei ya ulaya. Je kwa nini watanzania hatuna akili ya kuweza kupeleka hivi vitu ulaya na kupata soko zuri.
Mimi napenda sana ndizi bukoba na huwa nazipata kwa urahisi sana katika maduka ya uk zikiwa zina nembo ya (product of uganda). Hawa jamaa wananunua ndizi hata kutoka bukoba na karagwe. Sisi kwa nini tusifanye hivyo tena kutoka hata mbeya? Waganda wanauza majimbi, viazi na hata nyanya chungu katika soko la ulaya. Sisi tumelogwa?
Wakenya wametawala soko la maua, sisi kwa nini hatuwezi?
Naomba mawazo yenu

mkuu yale matunda unayo yaona mheza na pwani kule hayana viwango vya kuingia ulaya hata siku moja na huwezi pewa kibali cha kuingiza ulaya.

- wale wanacheza na standard si mchezo na kama hulimi kwa organic farming huwezi ingiza bidhaa ulaya,

- wale wanataka matunda na mboga zilizo zalishwa kwa organic only, yale mananasi yanayo puliziwa dawa za kufa mtu hayawezi kuingia kule,

- na hata kenya si kwamba wananunua matunda huku halafu wanasafirisha ulaya, no wanalima huko huko kwao, matunda ya mheza hata south africa huwezi ingiza mkuu
 
Nimeshawah kujaribu iyo biznes dah its complicated kufanya individual labda uwe na mtaji mkubwa sana ki2 ambacho wengi ha2na,wenzetu kenya na uganda wanaweza coz wanapata sapoti kubwa kutoka serikali zao ili uweze kuuza uk ni lzm uwe na certified packing house then tz hapa logistics ni tabu sana km unasafirisha kwa air freight 2na depend kwa kenya airways ambao wanawapendelea wakenya wenzao na emirates,british,klm ni expensive haitokulipa vzuri then ha2na exposure kwa kweli coz pale unapohtaj msaada wa government officials respond haiwi nzuri sana coz they dnt i understand what kind of biznes it this so dispointing kwa kweli
 
mkuu ni kweli iko complicated sana, ila tambua kwamba ni nchi husika ndo huwa wanatoa kibali baada ya kulizika na Ubora wa Matunda hayo, na hapo hakuna cha siasa wala rushwa mkuu na hakuna short cut kabisa njia imenyoka na ni moja tu,

- Na wanaozani serikali inaweza kuwasaidia kuingiza vitu kama matunda Ulaya wanajidanganya, wale wanaangalia Ubora na maswala ya Afya hawaangalii mambo ya Siasa kwamba Nchi fulani tuna Urafiki nayo, hawana short cut hata kidogio,

- Tembea wale TAHA wawape procedure za ku export matunda na mboga kwenda Ulaya hapo ndo utagundua kwamba inatakiwa juhudi zako ziwe 90%,

- Yale mananasi ya kule Pwani na machungwa ya muheza Tanga hayana viwango vya kuuzwa kwenye masoko ya Ulaya,

Wakuu naomba ushauri wenu.
Nimekuwa nitembelea maduka mbali mbali katika nchi za Ulaya hasa UK na kukuta bidhaa kazaa za kutoka Uganda na Kenya lakini sijawahi kuona bidhaa zozote kutoka Tanzania katika maduka ya UK. Nikiwa Tanzania naona kuna matunda mengi kama Machungwa, Mahembe, Nanasi, Mapalachichi, nk zimerundikwa tu barabarani na vinauzwa kwa bei ya chini sana kulinganisha na bei ya Ulaya. Je kwa nini Watanzania hatuna akili ya kuweza kupeleka hivi vitu Ulaya na kupata soko zuri.
Mimi napenda sana ndizi Bukoba na huwa nazipata kwa urahisi sana katika Maduka ya UK zikiwa zina nembo ya (Product of Uganda). Hawa jamaa wananunua ndizi hata kutoka Bukoba na Karagwe. Sisi kwa nini tusifanye hivyo tena kutoka hata Mbeya? Waganda wanauza majimbi, viazi na hata nyanya chungu katika soko la Ulaya. Sisi tumelogwa?
Wakenya wametawala soko la maua, sisi kwa nini hatuwezi?
Naomba mawazo yenu

Mkuu tafuta uwezekano wa wewe kuanza kuuza bidhaa au hayo matunda toka TZ. Ukweli ni kwamba hata kahawa ya TZ watu wanai-pack vizuri na kuandika kuwa ni product za kwao. Vile vile machungwa. machungwa ya Muheza wale wa kutoka jirani wanakuja wanayachuma kwa umakini ili yasipate mikwaruzo wanaya-pack na kuandika ni produce za kwao na kuuza. Sisi wa TZ tumekalia kulalamika. Na malalamiko hayaleti tija bali uchungu na akili kutokufanya kazi vizuri na kutokuona fursa zilizopo. Watu wachangamke!
 
Tatizo mfumo wa kusubiri serikali ifanye kila kitu ndiyo uliodumaza akili wa waTZ wengi. Serikali haiwezi fanya kila kitu na kuuza machungwa. Sisi wananchi ndiyo tuuze machungwa (export) na kuchangamkia fursa zilizopo. Merci!
 
Back
Top Bottom