Biashara ya Kusafirisha Mazao Nje ya Nchi: Jifunze Utaratibu wa Kufuata, Changamoto, Faida na Uzoefu wa Wengine

emmanuel1976

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2011
Posts
301
Reaction score
80


Wadau, naomba kujua nini cha kufanya kabla sijaanza kusafirisha biashara nje ya bara la Africa. Nataka ku export chai na kahawa nahitaji nini kwanza. Kama ni leseni ni aina gani ya leseni, ama vibali na zinapatikana wapi.

Asanteni

WADAU WENGINE WANAOHITAJI KUFAHAMU BIASHARA HII

MICHANGO NA UZOEFU WA WADAU
 
Exportation ni jambo zuri kwani linainua uchumi wa nchi. Nchi yetu itaweza pata pesa za kigeni ktk hilo wazo lako zuri. Lakini kwanza tafuta masoko nje ya nchi ili ujue ni wapi unataka peleka bidhaa zako.

Na pia haujaweka wazi kama unataka safirisha bidhaa gafi yaani chai na kahawa ambavyo havija sindikwa au una export processed goods. Nasema hivi maana taratibu na mamlaka zinatofautiana kutegemea na nini unaexport.

Pia uzingatie kwamba baadhi ya nchi ukipeleka ungraded goods ni kosa la jinai ambalo yeyote atakayeshirikiana nawe akiwa nchi hizo aweza fungwa. Nchi hizo ni kama USA na Canada. Ukiingiza chakula ambacho ni substandard utafungwa.
 
Do you have ready market or customers?
 
Wadau, naomba kujua nini cha kufanya kabla sijaanza kusafirisha biashara nje ya bara la Africa. Nataka ku export chai na kahawa nahitaji nini kwanza. Kama ni leseni ni aina gani ya leseni ama vibali na zinapatikana wapi. Asanteni

Mambo kama haya ndo yananifanya mimi mrdash1 niamini kuwa watanzania tumeumbwa na nusu akili. yaani wewe ufikirie biashara nje ya nchi kabla ya biashara ya ndani? Mtoto ambaye bado hajajua kutembea atawezaje kukimbia?

Mimi nakuhakikishia kwa hapa bongo Da slam ndo jiji namba moja lakini mvua ikinyesha mitaa inafurika maji watu wanabebana migongoni, uchafu na takataka kila pahala, watu wachovu, majumba yamechakaa na magari yamechoka, mitaa imejaa watu wamevaa yeboyebo wamebeba biashara za mikononi hivi eti ndo mtu wa jamii kama hii ndo afanye biashara ya kimataifa? Ha ha ha ah mimi mrdash1 acha nijichekee!

Ushauri wangu wa bure anzisha biashara ndani kwa ndani, imarisha viwango na uzalishaji. Makampuni yote duniani yalianza kama local companies nchini mwao baadae yakapanuka hadi nje ya mipaka. Mbongo anataka aanzie nje ya mipaka. Kudadadeki!
 
Wadau, naomba kujua nini cha kufanya kabla sijaanza kusafirisha biashara nje ya bara la Africa. Nataka ku export chai na kahawa nahitaji nini kwanza. Kama ni leseni ni aina gani ya leseni ama vibali na zinapatikana wapi. Asanteni
Kama uko serious, nakushauri utafute firm or individual consultant, ambaye amebobea kwenye international business, uwe tayari kulipa consultation fee, then atakushauri vizuri.

Tatizo tulionalo sisi wafanyabiashara waTZ we dont use experts, tunafanya mambo kienyeji mno.
 

Kaka, naomba na mimi unisaidie kama unaweza kuniunganisha na Consultant wa Biashra hasa hizi za kijasiriamali ili anisaidie na mimi nitamlipa alimradi anipe CV yake kabla sijawasiliana naye.

Nitashukuru kwa msaada wako maana nami natapenda nijingize kwenye biashara za kijasiriamali na baadae za nje.
 
Pamoja na mambo mengine utahitajika kuwa na import permit toka nchi unayotaka kupeleka, export permit toka Tanzania, na inspection certificate ya hiyo kitu unayotaka kusafirisha.
 
Kwa kweli hujamtendea haki kabisa aliyeuliza swali. Wewe umefikiria tu kuwa mwulizaji wa swali hafanyi biashara yeyote Tanzania.

Kwamba Tanzania kuna maisha duni haimaanishi kuwa nchi haiuzi vitu nje ya nchi. Nakuomba ufanye utafiti wa biashara ambazo Tanzania inauza nje na inapata kiasi cha pesa nchi inapata kwa mwaka.
 
Kwanza fanya business name Registration Brela.
 
Pili nenda wizara husika kwa ajili ya leseni ya biashara hiyo.
 
Halafu nenda Board ya Chai na Bodi ya Kahawa kwa vibali vyao.
 
Kwa kukusaidia kutakiwa na Mkutano na wafanyabiashara toka UAE May 8 pale Kempinski Jaribu kuwasiliana na TIC ujisajili.
 

Hakuna umeme, hakuna maji, hakuna usafirishaji na usafiri wa uhakika, hakuna technology, watu hawawezi kuongea kiingereza ambacho ndo lugha ya biashara ya kimataifa, huduma za benki dhaifu, mfumo wa uchumi wa kijima ambamo pesa nyingi zipo kwenye informal sector etc etc etc, bidhaa gani hizo za nje ya nchi?

Kuuza ngozi za ng'ombe na mbuzi? Hata hizo huwezi maana huna vifaa vya kupimia magonjwa hatari ya wanyama kwa mfano anthrax. Tumeikenulia sana meno CCM kwa muda mrefu hadi dunia yote imetuacha, hakuna matumaini siyo leo wala kesho.
 
Kwa kukusaidia kutakiwa na Mkutano na wafanyabiashara toka UAE May 8 pale Kempinski Jaribu kuwasiliana na TIC ujisajili
Naomba details ya hio mkutano ya wafanyabiashara wa UAE.
 
NAMNA YA KUUZA BIDHAA NJE YA NCHI (EXPORT) UKIWA TANZANIA

Kwa sheria ya forodha ya Tanzania haikutozi kodi ya aina yoyote wewe unayeuza bidhaa nje ya nchi isipokuwa kwa aina mbili (2) tu za bidhaa nazo ni ngozi ghafi pamoja na korosho ghafi. Endapo utakuwa unauza/safirisha ngozi ghafi toka Tanzania utatozwa ushuru usiozidi 60% ya bei ya FOB au TSH. 600 kwa kilo.

Na kwa upande wa korosho utatozwa ushuru usiozidi 10% ya FOB au Dola za kimarekani 160 kwa kila tani moja ya mraba (metric ton).

Hatua za kupitia unapouza/safirisha bidhaa nje ya nchi

1. Muuzaji/msafirishaji unatakiwa kutafuta wakala wa shughuli za upokeaji na usafirishaji (Clearing and Forwarding Agent (CFA)) atakayeshughulika na maswala ya hati zinazohusika kwa njia ya intaneti.

2. Wakala atashughulika na hati na/au vibali vyote kwa njia ya mtandao maalumu uliounganishwa kutoka kwake na mfumo wa TRA kabla ya ukaguzi wa mwisho na kutolewa kibali cha kusafirisha. Hizo ndio hatua za awali kabisa za kuzipitia unapoanza kuuza/kusafirisha nje ya nchi.

Hati zinazotakiwa

1. Risiti ya mauzo

2. Mpangilio wa ufungashaji (park list)

3. Cheti chako cha mlipa kodi (TIN)

4. Cheti cha ridhaa kutoka wizara husika kwa aina ya bidhaa inayosafirishwa. Mfano wizara ya kilimo kwa mazao, au wizara ya madini kama ni madini yanasafirishwa au mamlaka ya chakula na dawa kama bidhaa ni chakula au madawa.

5. Barua ya kumruhusu au kumpa kazi huyo wakala wa upokeaji na usafirishaji (CFA).

Wakala atashughulikia kila mipango mwanzo hadi mwisho.

Wewe kwa upande wako utakuwa na jukumu la kuwa karibu naye kwa kila hatua anayopitia ili pia uweze kutoa taarifa kwa upande wa mteja wako wa nchi ya nje mfano utatakiwa kumtumia hati ya kusafirishia toka shirika la meli (kama ni meli) au namba ya ufuatiliaji (tracking number) kama ni kwa ndege.
 
Asante sana kwa huo ufafanuzi.

Sisi tumevumbua hapahapa Tanzania, Natural remedy ya kutatua matatizo mengi ya ngozi na urembo wa ngozi, hii si uvumbuzi mpya bali ilikuwa haijulikani kama hii bidhaa Tanzania ipo ya aslili tena ni nzuri zaidi ya hiyo ya nje. Kwa kuwa ipo hapa Tanzania, bei yake ni nafuu sana na ni nzuri sana ukilinganisha na bidhaa kama hii zinavyouzwwa nje.

Tunatafuta mshirika/washirika watakao weza kuifanyia packing, branding, marketing na mengineyo. Bidhaa tunayo tayari na wengi wameijaribu ni nzuri sana.

Tunataka wawekezaji wa ndani, hatuoni umuhimu wa kuweka wawekezaji wa nje kwa kuwa tuna uhakika sisi wenyewe tunaweza.

Kwa anaefikri anaweza hayo apitie hapa: Aunt Zainab's Natural Super Clay

Wawasiliane nami kwa PM maelezo zaidi.
 
Habari ndugu zangu, haja Yang kubwa hapa ni kujua ni kwa namna gain naweza nikaexport Nafaka nje nchi kama mchele, maharage, Mahindi n.k ikiwa kuna mtu anaexport Nafaka kibiashara naomba tupeane ujuzi hapa JF kwa faida ya wengi, ili tupate kujua ni utaratibu gani ufatwe na vibali vinavyoitajika.
 
Lazima uwe na mteja nje ya nchi. Hakikisha pesa imeingia katika akaunti yako ndio utoe shehena, sina uhakika kama mahindi bado ni marufuku kuuza nje, mengine huhitaji kibali. Onana na clearing ajent atakusaidia kutengeneza nyaraka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…