Biashara ya kusambaza vitu na huduma kwenye makampuni makubwa

Biashara ya kusambaza vitu na huduma kwenye makampuni makubwa

AfricaUnited

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2010
Posts
2,367
Reaction score
1,293
Ndugu wanajamvi,

Kwa muda baada ya kuona watu baadhi ya makampuni yakisema yametumia mabilioni ya fedha kwa suppliers wazawa haswa makampuni makubwa.

Mfamo migodi, UN, viwanda vya cement, mahoteli kimataifa, Total, Songas, Oryx, Puma energy ni hasa ya kigeni.

Nimevutiwa kujua haya.

Naomba kujua ABC ya hizi biashara za kuuza vitu kwenye makampuni makubwa ya kigeni /viwanda.

1. Tender za kusupply Gpysum kwenye viwanda vya cement kama Twiga,simba au tembo cement

2. Ku-supply spare parts za machine, magari na mitambo kwenye makampuni makubwa.

3. Ku-supply mafuta au lubricants.

Ninahitaji kufanya zote au moja kati ya hizi.

Sijafanikiwa kukutana na yoyote mwenye uzoefu wa hizi nijue :-

*Mtaji una-range kiasi gani
*Ugumu wa kupata tenda
*Malipo. Wanalipa kwa wakati?

NB: Kampuni ninayo

Asante
 
Viwili hivyo naweza,ila cha Corruption mmm.
Lakini nikijua ABC bila underground hizo ,nitapambana ,nimefanya kwenye taasisi za umma ,na nilipata tenda bila kutoa hata senti ,na sasa Taneps itapunguza mianya hiyo
Tatizo taasisi za umma nyingi malipo changamoto, yanachukua muda.
 
Dili ya ku Supply Gypsum kwa hao jamaa labda uwe dereva wa kukodiwa kupeleka mzigo tu. Ila kuwa Agent its about millions of money!

Unaambiwa weka Advance Payment kiwandani about 200G! Utaweza?
 
Dili ya ku Supply Gypsum kwa hao jamaa labda uwe dereva wa kukodiwa kupeleka mzigo tu. Ila kuwa Agent its about millions of money!

Unaambiwa weka Advance Payment kiwandani about 200G! Utaweza?

Asante Kwa mchango ,kama wanalipa let's say 30 days within ....naweza weka mil 100 advance payment!!!! Je pia so wanakuwa na suppliers wengi?kukwepa kumpa mmoja akazidiwa?

Vipi kuhusu advance payment guarantee nikipewa na banki nipeleke kiwandani wanipe advance?

Hio 200g ni mil 200?
 
Ndugu wanajamvi,

Kwa muda baada ya kuona watu baadhi ya makampuni yakisema yametumia mabilioni ya fedha kwa suppliers wazawa haswa makampuni makubwa.

Mfamo migodi, UN, viwanda vya cement, mahoteli kimataifa, Total, Songas, Oryx, Puma energy ni hasa ya kigeni.

Nimevutiwa kujua haya.

Naomba kujua ABC ya hizi biashara za kuuza vitu kwenye makampuni makubwa ya kigeni /viwanda.

1. Tender za kusupply Gpysum kwenye viwanda vya cement kama Twiga,simba au tembo cement

2. Ku-supply spare parts za machine, magari na mitambo kwenye makampuni makubwa.

3. Ku-supply mafuta au lubricants.

Ninahitaji kufanya zote au moja kati ya hizi.

Sijafanikiwa kukutana na yoyote mwenye uzoefu wa hizi nijue :-

*Mtaji una-range kiasi gani
*Ugumu wa kupata tenda
*Malipo. Wanalipa kwa wakati?

NB: Kampuni ninayo

Asante
Mkuu,
hakuna mtu atakuambia hilo.
Kampuni unayo, gari unalo? Unatakiwa uzunguke sana na uwe na watu potential na ubaya wa hali halisi watu sasa hivi wanajiogopa pia isitoshe wazo ulilonalo wewe wenzio waliishajikita huko siku nyingi hawaachii!
Kuna changa moto kubwa Fanya juhudi kubwa kutimiza lengo hilo.
 
Asante Kwa mchango ,kama wanalipa let's say 30 days within ....naweza weka mil 100 advance payment!!!! Je pia so wanakuwa na suppliers wengi?kukwepa kumpa mmoja akazidiwa?

vipi kuhusu advance payment guarantee nikipewa na banki nipeleke kiwandani wanipe advance?

Hio 200g ni mil 200?
Yeah bro, unaweza ambiwa weka ata 100M ukapewa zone zako! Kulingana na scales ndo jinsi utapewa advance payment.

Kwakuwa ni biashara ya ghali competitors sio wengi kama kwenye biashara za vitumbua.
 
Dili ya ku Supply Gypsum kwa hao jamaa labda uwe dereva wa kukodiwa kupeleka mzigo tu. Ila kuwa Agent its about millions of money!

Unaambiwa weka Advance Payment kiwandani about 200G! Utaweza?
Kaka ongea kitu ambacho unakijua usiwakatishe tamaa, Gypsum unaomba tender ukipewa wanakuletea mpaka magari wao viwanda vya cement kuja kuchukua mawe, labda changamoto ni kupata hiyo Tender

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kaka ongea kitu ambacho unakijua usiwa katishe tamaa Gypsum unaomba tender ukipewa wanakuletea mpaka magari wao viwanda vya cement kuja kuchukua mawe, labda changamoto nikupata hiyo Tender

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwenye kuipata hio tender ndio hapo kwenye mkasa wa hizo namba hapo. Kusambaza hata mimi nawewe tunaweza ila Credibility ndio mzizi.
 
naelewa kaka lakini hamna rahisi kila kitu nikupambana but vitu vinafanyika
Sio Tz...nchi ni corrupted balaa..! Kuna majitu yamejisimika huko ..siongei blah blah nami Kuna ishu nafatilia mweee🤧! Nabak kutoa tu business card 🤧
 
Tz ukisikia neno Tender, basi Corruption ndio kitu kitakachofuata.. Bila hivo mzee utasugua sana vile already kuna watu tayari wanafanya hizo kazi miaka nenda rudi, wameota mapembe, mizizi na mabawa kabisa so kuwachomoa inahitaji nguvu ya ziada na usikate tamaa.

KIla jambo linawezekana ila Unatakiwa uwe tayari kulipa gharama zake.
 
Back
Top Bottom