Biashara ya kutengeneza bati

hussler

Member
Joined
Oct 7, 2017
Posts
78
Reaction score
33
Wakuu mwenye uelewa na biashara ya kutengenez bati, "roll forming " naomba tupeane uzoefu.
1. Roll forming machine bei gani
2. Inatengeneza aina ngapi za bati glazed etc
3.uagizaji wa coils na kodi zake.
4.coil moja ntapata mita 3 urefu na upana mita moja ngapi
5.soko la kilimanjaro liko vpi
6.je nikiwa na mtaji wa 70m naweza kuanza.
 
Safi sana mkuu! Mungu akusaidie ufanikishe then uje utujuze tuje kupiga kazi! Achana na mambo za kuwafanya watu waishi kishetani
 
Kuna jamaa humu alianzisha uzi kitambo sana alikuwa anauzwa mashine(complete production line)
 
Ngoja wenye uzoefu waje ila kwa hapa dsm ni biashara ngumu sana kwani kuna wachina wana viwanda vya kutosha na wao wana uwezo mkubwa wa kupa raw materials yani coil kule kwao kwa gharama nafuu sana kwani ni wazoefu wa kutosha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…