mkuu tuongee biashara ni PM
mkuu tuongee biashara ni PM
hivi hiyo yako au na unaiuza au?
N
Ni vyema kufungia vifuko vya karanga. Mfuko upo kwenye rola haina usumbufu katika kujaza. Unafunga kwa mashine zinauzwa 50,000 zinatumia umeme. Hizi ni za kuchomea tu
Ok
Hello friends,
Nitajibu comment zenu ila kwanza nianze na junsi ya kutengeneza ice cream za ubuyu.
Mahitaji
1. Ubuyu(tsh 2000 kisado)
2. Maji
3. Rangi(tsh100)
4. Ladha(tsh1000)
5. Sukari (tsh1300 nusu)
6. Vifungashio (tsh 500)
Kwa kipimo cha sado moja ya ubuyu utapata icecream nyingi zaidi ndio maana sukari itakua nusu. Sasa hapa ili upate bidhaa nzuri unafanya hivi chukua maji weka kwenye sufuria yenye ukubwa wa kutosha weka ubuyu wako kisha bandika jikoni (ubuyu ukibandikwa jikoni icecream yako itakua haibakizi kile kijiwe cha mwishoni ambacho hakina ladha ila inakua laini kabisa, japo unaweza kuloweka tu bila kuchemsha)
Funika sufuria yako utakua unafunua kukoroga ili ubuyu na mbegu viachane. Ikifikia hatua ubuyu unachemka tayari mbegu na ubuyu wa nje vitakua vimeachana epua subiri vipoe. Sasa chuja mbegu na uji uji wa ubuyu weka uji wako kwenye chombo kingine sasa ongeza maji taratibu huku ukikoroga ili kupata uzito wa uji ubaotaka usiweke maji mengi sana ikawa maji kabisa. Baada ya hapo malizia kuweka sukari, rangi na ladha unayotaka mie hutumia passion. Funga bidhaa yako gandisha, kazi imeisha unasubiri mkwanja tu.
Kwa mnaosema icecrean ni 100 tu, you are very wrong. Hata maandazi kuna jingine huwezi uza zaidi ya 100 lakini andazi hilo hilo duka la pili linauzwa 500. What matters ni ubunifu katika kazi yako; mimi huuza 200 na nikiitwa sehemu napeleka kwa 300.
Pia icecream sio spesho kwa watoto tu. Ukitengeneza vizuri hata watu wazima watanunua tu mbona (ukwaju wa Bakhresa unaliwa na kila rika?) Ile ni icecream tu kama hizi za kawaida sema kaboresha package na ubunifu. Mie siwauzii watoto tu, napata oda hadi za maeneo yenye mikutano japo I'm m still growing. Hivyo, kama unahisi upo kwenye nafasi ya kufanya hii kitu usiichukulie poa its a deal.
Kuhusu fridge, labda niseme hivi: ukiamua kweli kweli na ukiona unaweza kufanya hii kitu basi tafuta hata ki freezer used ufanyie kazi ama kama home kuna fridge basi ifanye iwe ni kama asset sio kuweka nyanya tu. Tuamke vijana wenzangu tusisubiri ajira tufanye yaliyopo kwenye uwezo wetu wakati tunasubiri hayo mambo mengine.