Wakuu, naomba ushauri kuhusu biashara ya kutuma fax. Nina stationery yangu Tabora, nafikiria kuweka huduma ya fax manake kuna mteja mmoja mmoja wanapitaga kuulizia hii huduma. Kwa vile sina uzoefu nayo naomba maoni yenu kuhusu:
1. mashine ya fax inayofaa
2. utaratibu wa kuunganishwa (nasikia sijui lazima uwe na simu ya landline halafu sijui ndo iweje....)
3. changamoto za biashara yenyewe
Natanguliza shukrani zangu za dhati kwa mawazo yenu!
Fax machines zipo nyingi tu usihufu kuhusu aina za machine zenyewe.
Ila naona kama vile siku hizi watuma fax sio wengi sana, watu wengi wamehamia kwenye email.
Ila ili uweze kuunganishwa na huduma ya fax, lazima uwe na landline (kama simu za kawaida za mezani za TTCL).
Ukishakuwa na landline, hapo jamaa wa TTCL watakuunganisha na huduma ya fax (baada ya kununua fax machine).
Changamoto ni uhaba wa wateja wa fax. Huku Dar fax kama vile hazitumiki kabisa... Sijui huku uliko !!
Nashukuru kwa kunipa mwongozo mkuu. Vipi hawa TTCL wanachaji kadri unavyotumia hiyo fax? au wana fixed charge per month bila kujali umefanya biashara/umehudumia wateja wangapi?