Frankly speaking, nimeifanya tangu 2019 hadi sasa sina jibu nitaendelea au ndio basi tena.
Kikubwa kilichonipa short break ni ughali wa mafuta. Tangu kindoo cha lita 9 kiuazwe 50,000, viazi 1,000 @kg na tray ya mayai 9,000 nilikaa chini nikafanta review nikajikuta kila tray inanilipa chini ya 1,000 nikajidharau kupotez muda.
Nikajipa pumziko kwanza bei ya mafuta ishuke. Sasa hivi ilipanda hadi 63,000 ile kubwa ikigonga 115,000 na kiazi 1,200 na mayai 10,000.
Wateja wanataka bei ile ile. Hata nikicheza na vipimo sina pa kuokoa.
Utafiti na time to time business review no muhimu sana. Vinginevyo unaweza kumlaumu mfanyakazi bure.