Biashara ya kuuza maziwa fresh na mgando kwa Dar es Salaam

Biashara ya kuuza maziwa fresh na mgando kwa Dar es Salaam

#Nauliza jinsi ya kugandisha maziwa yawe matamu.

niliona Mzee mmoja yeye akishakamua labda amepata Lita Moja anayaweka kwenye kidumu kidogo ,
kesho yake pia akishakamua Tena anachanganya kwenye Yale maziwa ya Jana yake Ili dumu lijae la Lita 5 ndio asubiri yagande ,

baada ya siku nne au Tano anasema yapo tayari ,lakn ukiyanywa sio matamu ni kama unakunywa maji,ni mepesi sana na pia hayana ladha nzuri.
 
Hii biashara ya maziwa sio mbaya ni moja biashara kama zilivyo biashara nyingine.

Ila tatizo linakuja ktk ukweli wa maziwa yenyewe kwani wauza maziwa wengi wanatenda sana dhambi na siku utaingia ktk hii biashara itaiona dhambi yenyewe japokuwa ni biashara yenye faida lakini bado wauzaji kuanzia anayeuza jumla na rejareja ni wenye tamaa na wasio wakweli.

Na hawa wajumla kasumba yao kubwa ni jeuri hasa kipindi hiki ambacho maziwa ni adimu kutokana na kiangazi.
Mm ni muuzaji wa rejareja na jumla sijafikia kiwango cha kujisifia yakuwa nauza jumla kwani pale ambapo nitakapoanza kuandaa mwenyewe ndo nitakuwa tayari kumwelekeza mtu vizuri zaidi.

Mm kwa sasa ni mchuruzi bado karibu ktk hii biashara lile ambalo.na uwezo nalo nitawaelekeza kwani mm ndo miaka miwili kwenye hii kazi
Asante kwa kushare mkuu nimepata mawazo vzr kabsa
 
Nina jamaa yangu yeye anafanya biashara hiyo na inamuingizia vizuri tu faida,kwanza kabisa niende moja kwa moja kwa mfano wake.

Ipo hivi ndugu yangu mmoja yeye ana frem ndani ya jiji hili la Dar es salaam,yeye alikuwa anachukuwa mzigo kutoka njia ya kusini,huko kusini aliweka kama ofisi kubwa ya wafugaji kumuuzia maziwa kila siku usiku na mchana,yeye anajua au anatumia kifaa ya kugundua ya kuwa maziwa yamewekwa maji au laah,akishachukua maziwa kutoka kwa wafugaji basi anaya chemsha na akimaliza ana ya hifadhi kwa fridge(friza) kwa ajili ya kuto kuharibika,baada ya hapo ana yasafirisha kuja kuuza huku dar.

Nilicho jifunza toka kwake,tafuta sehemu ambapo utakuwa na uhakika wa kuuza hata little 100 kwa siku,tafuta boma nje ya dar ambapo utanunua mzigo kutoka kwa wafugaji na ku yaandaa pia hakikisha fridge (friza) lipo la uhakika na umeme pia,pia hakikisha mzigo unao nunua basi ni wenyewe yani hauja chakachuliwa,pia pata vijana waaminifu ambao watakusaidia kuandaa mzigo vizuri.

Kama ntakuwa sijakuelewesha vizuri basi karibu PM
Asante kwa mawazo
 
Hii biashara ya maziwa sio mbaya ni moja biashara kama zilivyo biashara nyingine.

Ila tatizo linakuja ktk ukweli wa maziwa yenyewe kwani wauza maziwa wengi wanatenda sana dhambi na siku utaingia ktk hii biashara itaiona dhambi yenyewe japokuwa ni biashara yenye faida lakini bado wauzaji kuanzia anayeuza jumla na rejareja ni wenye tamaa na wasio wakweli.

Na hawa wajumla kasumba yao kubwa ni jeuri hasa kipindi hiki ambacho maziwa ni adimu kutokana na kiangazi.
Mm ni muuzaji wa rejareja na jumla sijafikia kiwango cha kujisifia yakuwa nauza jumla kwani pale ambapo nitakapoanza kuandaa mwenyewe ndo nitakuwa tayari kumwelekeza mtu vizuri zaidi.

Mm kwa sasa ni mchuruzi bado karibu ktk hii biashara lile ambalo.na uwezo nalo nitawaelekeza kwani mm ndo miaka miwili kwenye hii kazi
Naomba kufahamu, umefikia wapi adi sasa kwenye hii biashara, naomba ni changamoto zipi unakumbana nazo kupitia biashara hii alkadhalika mafanikio uliyo yapata kupitia biashara ii
 
Back
Top Bottom