Biashara ya Kuuza Mkaa: Uzoefu, Vibali vya kuchoma, Changamoto na Ushauri

inawezekana kwa kibali maalum, jaribu kuuliza kwa hao wafanyabiashara, mkaa unafaida sana nilisikia ukipata eneo lililochangamka kwa makazi ya watu.
 
mkuu ..mkaa cyo lazima ukate miti... saiv unaweza kutengeneza mkaa wa kisasa ambao hauchafui mazingira ....
hivi bado wanaruhusu hiyo biashara?
nilisikia imepigwa marufuku sababu ya ukataji wa miti hovyo
 
Habari wakuu.

Twende kwenye mada. Naombeni ushauri kwa mwenye uzoefu na kuifahamu hii biashara ya mkaa kwani nina mtaji wa 1.5 million ila sina uzoefu wowote ule katika biashara na ningependa kupewa muongozo pia ushauri faida na changamoto zitokanazo na biashara hii.

Nawasilisha.

Biashara ya mkaa ni nzuri sana sana kama ukiamua kuwa serious na unachokifanya lakini pamoja na hayo biashara hii ina usumbufu mkubwa sana hasa watu wa maliasili hao ni kama TRA wakiona mkaa mahali maskio yana wasimama.

Unapofanya hii biashara ifanye kwa malengo na ujue si biashara ya kudumu maana miaka inaenda na teknolojia inakua so unapofanya hii biashara jiwekee moyoni mwako mimi ntaifanya hii biashara kwa miaka mi 5 tu kisha ntaachana nayo.

ukishajiwekea malengo hayo basi anza kazi sasa ambapo kwa mtaji huo ulionao ni hakika utafanya biashara sana ambapo nakushauri kwa mtaji huo ugawe mara 3 nikimaanisha ufungue ofisi 3 na kila ofisi iwe na mtaji wa laki 3 jumla kwa ofisi tatu utakua umetumia 900,000 then kwenye hiyo 1.5m utabaki na laki 6 imetulia,hiyo laki 6 tumia kwa akili kununua mahitaji/vifaa ya ofisi zote tatu nikimaanish ndoo za kupimia,visado,mifuko mbadala,nk

kisha weka vijana kwenye kila ofisi na hakikisha ofisi zimesambaaa usiweke ofisi mtaa mmoja,kama unafanya hakikisha biashara yako unaifanyia uswazi uswazi kwenye makazi ya watu au kama ni huku town hakikisha unatafuta center flani (sio barabarani) yenye bar na sehemu kuna kina mama ntilie wakutosha weka kambi hapo.

Mkaa gunia ni 50,000 kwa bei ya shamba ambapo wanapokea oda kuanzia gunia 3 kama wewe ni mkazi wa mjini nadhani utakua umeshakutana au pishana na piki piki za namna hii

View attachment 1266529

jamaa akiwa kakalia tank juuu lina magunia ya mkaa ma tatu so trip 1 akija kukuletea mkaa unampa 150,000 na haleti chini ya gunia 3.

kwa mtaji wa laki 3 atakuja trip mbili atakuletea mkaa konki jiwe jiwe magunia 6 ambapo kila goli atapeleka gunia 6 kisha wewe utajua mwenyewe unarudishaje hiyo hela ya mkaa uliyonunulia maana mkaa kila sehemu kuna vipimo tofauti zunguka sehemu unazotaka weka goli angalia wakazi wa eneo husika wanapendelea nunua mkaa kwa vipimo gani kisha ndio uweke.

Kwenye mkaaa kila kitu kinauzwa mkuu,vumbi la mkaa,chenga, na mkaa wenyewe hapo ni wewe sasa angalia bei unayotaka BEI PANGA MWENYEWE sikufundishi bei maana kila mtu ana malengo yake ila kwa ushauri kwenye bei zako hakikisha unakua na bei za chini na jitahidi upate mkaa kwa wauzaji wanaojielewa mkaa uwake bila moshi na sio uletewe mkaa kukolea unakolea ndani ya lisaaa,kuisha ndani ya dk 5 (utakimbiza wateja) hakikisha unapata wauzaji mkaa wenye uzoefu na kazi yao.

maana ukinunua gunia za mkaa 6 halafu ukute zote umepigwa mkaa mbovu itakubd uingie cost ya kuagiza mkaa mwingine mzuri ili uje uchanganye na huu uweze kuuza na ndio mana kwenye ile 1.5M sikushauri uimalize tumia 900k then nyingine weka akiba.

NOTE:

Hii biashara ina pesa tena ina pesa kweli ila tu usiwe na mkono wa birika panapohitaji pesa TOA usitake longo longo sanaaaaa na usiwe mbahili ila kwa ufupi upo ini ze raiti trakiiii.

Kapepo utakua umeambulia machache.
 
Kuna Uzi mmoja humu umeelezea na umefafanua vizuri kuhusu biashara iyo.
Jaribu kuu tafuta utapata maelezo ya kutosha.
 
Biashara ya mkaa ni nzuri sana sana kama ukiamua kuwa serious na unachokifanya lakini pamoja na hayo biashara hii ina usumbufu mkubwa sana hasa watu wa maliasili hao ni kama TRA wakiona mkaa mahali maskio yana wasimama.

Unapofanya hii biashara ifanye kwa malengo na ujue si biashara ya kudumu maana miaka inaenda na teknolojia inakua so unapofanya hii biashara jiwekee moyoni mwako mimi ntaifanya hii biashara kwa miaka mi 5 tu kisha ntaachana nayo.

ukishajiwekea malengo hayo basi anza kazi sasa ambapo kwa mtaji huo ulionao ni hakika utafanya biashara sana ambapo nakushauri kwa mtaji huo ugawe mara 3 nikimaanisha ufungue ofisi 3 na kila ofisi iwe na mtaji wa laki 3 jumla kwa ofisi tatu utakua umetumia 900,000 then kwenye hiyo 1.5m utabaki na laki 6 imetulia,hiyo laki 6 tumia kwa akili kununua mahitaji/vifaa ya ofisi zote tatu nikimaanish ndoo za kupimia,visado,mifuko mbadala,nk

kisha weka vijana kwenye kila ofisi na hakikisha ofisi zimesambaaa usiweke ofisi mtaa mmoja,kama unafanya hakikisha biashara yako unaifanyia uswazi uswazi kwenye makazi ya watu au kama ni huku town hakikisha unatafuta center flani (sio barabarani) yenye bar na sehemu kuna kina mama ntilie wakutosha weka kambi hapo.

Mkaa gunia ni 50,000 kwa bei ya shamba ambapo wanapokea oda kuanzia gunia 3 kama wewe ni mkazi wa mjini nadhani utakua umeshakutana au pishana na piki piki za namna hii

_DSC6790.JPG

jamaa akiwa kakalia tank juuu lina magunia ya mkaa ma tatu so trip 1 akija kukuletea mkaa unampa 150,000 na haleti chini ya gunia 3.

kwa mtaji wa laki 3 atakuja trip mbili atakuletea mkaa konki jiwe jiwe magunia 6 ambapo kila goli atapeleka gunia 6 kisha wewe utajua mwenyewe unarudishaje hiyo hela ya mkaa uliyonunulia maana mkaa kila sehemu kuna vipimo tofauti zunguka sehemu unazotaka weka goli angalia wakazi wa eneo husika wanapendelea nunua mkaa kwa vipimo gani kisha ndio uweke.

Kwenye mkaaa kila kitu kinauzwa mkuu,vumbi la mkaa,chenga, na mkaa wenyewe hapo ni wewe sasa angalia bei unayotaka BEI PANGA MWENYEWE sikufundishi bei maana kila mtu ana malengo yake ila kwa ushauri kwenye bei zako hakikisha unakua na bei za chini na jitahidi upate mkaa kwa wauzaji wanaojielewa mkaa uwake bila moshi na sio uletewe mkaa kukolea unakolea ndani ya lisaaa,kuisha ndani ya dk 5 (utakimbiza wateja) hakikisha unapata wauzaji mkaa wenye uzoefu na kazi yao.

maana ukinunua gunia za mkaa 6 halafu ukute zote umepigwa mkaa mbovu itakubd uingie cost ya kuagiza mkaa mwingine mzuri ili uje uchanganye na huu uweze kuuza na ndio mana kwenye ile 1.5M sikushauri uimalize tumia 900k then nyingine weka akiba.

NOTE:

Hii biashara ina pesa tena ina pesa kweli ila tu usiwe na mkono wa birika panapohitaji pesa TOA usitake longo longo sanaaaaa na usiwe mbahili ila kwa ufupi upo ini ze raiti trakiiii.

Kapepo utakua umeambulia machache.
 
ukinogewa kwenye hiyo biashara inabd uchague kama wewe ni KE upate mume maliasili kama wewe ni ME hakikisha unapata ka mke Maliasili na kama wewe ni PADRI hutaki hizo mambo hakikisha kila siku kwenye faida tenga 3000 (hii iwe kila siku unaitenga mahali) ili kikinuka tu wewe unaenda kwenye zile 3000 zako unahesabu unachukua unatoa.KWISHA.

usifunge ndoa na biashara moja chagua kuwa Mfanya biashara na sio Muuza mkaa
 
Assante sa
CONTROLA,
Assante sana mkuu ntaufanyia kazibushauri wako na je vipi kuhusu management ya stoo zote tatu imekaajenhili?
 
Back
Top Bottom