Biashara ya kuuza vyombo vya kupikia kwa 400k as capital inawezekana?

Biashara ya kuuza vyombo vya kupikia kwa 400k as capital inawezekana?

DR HAYA LAND

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2017
Posts
23,928
Reaction score
63,499
I hope Wote wazima na walio wagonjwa Mungu awape Tumaini jipya wapate kupona na kurejea katika Majukumu yao AminašŸ™

Tuje katika wazo

Mimi Ni kijana 24Yrs naishi Dsm kwa sasa hivi nimepata wazo la kuanza kuuza Vyombo vya kupikia kwa capital ya 400k tu .

Nahitaji kujua starting point

Mimi niliwaza kuwa nauza katika Minada mbalimbali au kutembeza kwa Mguu sehemu tofauti tofauti.

Mwenye nyongeza asikose kutoa Maoni yake

Nb Mtu wa kujiita Smart AJ sihitaji comment yako hapa.
 
Huku kwetu kuna wanaokopesha kila siku wanachukua hela kuanzia 1000 ndani ya mwezi mmoja deni linakuwa limeisha hasa kwa bidhaa isiyozidi 30k.
Changamoto kubwa kupata wateja wasumbufu anakupiga sound hana hela
Kila ukifata hela unamkosa na Mdeni wako kuhama ghafla hivo unapata hasara.
Hapa inatakiwa uwe unajua kudai na uwe serious hasa ndio nadhani utaona faida Mana biashara ya kufanya na wanawake ukiwachekea chekea wanakufilisi.
 
Back
Top Bottom