Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Waziri mkuu wa JMT leo ametembelea biashara ya UDART katika eneo la Gerezani amekuta mfumo wa kutoa tiketi na kuhakiki wa kielektroniki hautumiki badala yake tiketi zinaprintiwa, zinawekwa pembeni, abiria akigaiwa tiketi hakuna uthibitisho kama ni ya serikali kweli au za wajanja nje ya Serikali.
Amekuta gari iliyokuwa na ubovu wa gia boksi tu ikiwa imeng'olewa viti na vitu vingine ambavyo inaonekana vimeenda kutumika kama vipuri kwingine! Waendeshaji waliona ni bora zaidi kufanya hivyo kuliko kuagiza spea nyingine!
Waziri mkuu amechukuziwa sana na hali ya kujifia mradi kama alivyoikuta aliyoukuta gerezani. Tangu 2019 mpaka leo bado wako wanajenga mfumo wao wa kielektroniki, miaka 2.
Serikali ya JK ilifanya jambo zuri sana kuja na mradi wa UDART. Ilikuwa sahihi sana kujenga miondombinu yote ya mradi kwa kiwango cha juu. Serikali ilikosea sana kuendelea hadi kushiriki biashara yenyewe ya usafirishaji, kununua mabasi na kuwa mwendeshaji.
Mabasi ya mwendokasi ni kama daladala tu. Tofauti yake ni kuwa na upendeleo wa kuwa na barabara zake maalum. Zipo kampuni na watu binafsi wengi wanaoweza kuendesha biashara ya daladala kwa ufanisi na tija kubwa kuliko UDART ya sasa inavyoendeshwa.
Serikali ifanye utaratibu haraka wa kuipeleka hii biashara kwenye sekta binafsi na yenyewe ibaki na majuku yake ya msingi ya udhibiti na ukusanyaji mapato kama inavyofanya kwenye mabasi, magari ya mzigo na daladala.