Biashara ya mahindi mabichi

Biashara ya mahindi mabichi

Mashima Elias

Member
Joined
Dec 22, 2010
Posts
18
Reaction score
52
KILIMO CHA MAHINDI YA KUCHOMA.

Dhana ya kulima mahindi na kuyauza mabichi kwenye soko kabla hayajafikia hatua ya unga mgumu inajulikana kama kilimo cha mahindi ya kuchoma au uzalishaji wa mahindi mabichi, Kwa kawaida zao la mahidi hudumu kwa takribani siku 90 hadi 120 shambani inategemeana na aina ya mbengu lakini kwa mahindi ya kuchoma ni takribani siku 60 hadi 75 tu yanatoka shambani, Kilimo hiki kinamruhusu mkulima kuwa na angalau misimu miwili kabla ya msimu wa mvua kama analima kwa umwagiliaji.

Ni dhahiri kuwa kilimo cha mahindi mabichi ni mradi wa faida ukizingatiwa na kutiliwa maanani, kwenye ekari moja kuna wastani wa miche 17, 700 hapo utakua umepanda mbegu mbili kwenye kila shimo kwa umbali wa Sentimita 75 kwa 60, sasa baada ya kuwekeza pesa yako kwa vile unalima kibiashara ni matumaini utafuata hatua zote za kilimo bora cha mahindi, sasa ni muda wa kuingia sokoni, Tunakadiria kuwa ulivuna mahindi 15,000 tu, yaani kila mche upate hindi moja tu bora, achilia mbali habari ya mahindi kubeba mawili mawili kila mche na bado tumepunguza idadi miche kutoka 17 elfu hadi miche 15 elfu sasa unajua una kiasi gani hapo?

Ni hesabu ndogo sana, chukua Tsh.150 zidisha kwa 15,000. Mia hamsini ni bei ya kuuzia shambani hapo utapata milioni mbili laki mbili na elfu hamsini Tsh. 2,250,000/= basi toa milioni moja kama gharama, hapo unapata faida ghafi ya milioni moja na laki mbili na hamsini.

TOA MAONI YAKO [emoji3516].


images%20(6).jpg
 
Write your reply...kama nina robo eka lazma niwe na machine ya kumwagilia(pump) au naeza komaa kw mkono tu
 
Hapo kama ni hekari moja igawe panda nusu heka baada ya wiki mbili panda nusu heka. Vuna weka vijana wachome. Weka sufuria chemsha. Tafuta ka center. Kusanya maokoto.
Hii imekaa vizuri zaidi [emoji120]
 
Kama wewe ndio mkulima kwenye hii biashara ni HASARA

Mimi nimeyalima sana, anayefaidika ni dalali na yule muuzaji wa mwisho anayeuza kwa kuhesabiana
 
Ukiwa nyanda za juu kusini mahindi hayo yalime kuanzia mwezi wa tatu na uvune kuanzia wa Saba au mwezi wa nane utapiga hela sana
 
Back
Top Bottom