Hongera mkuu
Ushauri wa kwanza, ukiitwa PM shtuka, usiende, kimbia kabisa
Pili Nakushauri wekeza kwenye miji/majiji ya kibiashara, Dar, Arusha, Mwanza, Mbeya, Kibaha, Morogoro ni pazuri.
Nakushauri usiweke mtaji wako wote kwenye mkoa mmoja.
Jenga katika miji ambayo bado haipo peak ila imechangamka
Jenga frames za biashara na nyumba za kupanga na nyumba hizo ziwe zile standard za wastani (hizi nyumba zina wateja wengi). Aina ya 3 ya majengo ya kuwekeza, jenga guest. Ukijenga nyumba complex sana, kwanza utatumia mtaji mkubwa sana na wateja wa hayo majengo hawapo wengi sana, na majengo makubwa ni vulnerable sana inapotokea economic crisis.
Nakushauri majengo yawe ya variation hizi, sio zote guest houses, au zote frames au nyumba za kupanga tu
Tenga kama 50 milioni kwa ajili ya kununua na kuuza viwanja. Yaani ukisikia sehemu ina kiwanja kizuri kwa bei nzuri unanunua leo, kesho akipatikana mteja kwa bei ya faida unamuuzia.
Kwenye hii biashara Jenga urafiki na Maafisa kwenye Ofisi za ardhi za wilaya, Maafisa Watendaji wa Mitaa au Kata ili kuwa na taarifa current za viwanja
Jenga majengo/nyumba karibu na shule, vyuo, hospitali, Ofisi za Halmashauri, center za biashara au taasisi yoyote inayovuta watu wengi
Hongera mkuu kwa kuwa na kibunda ulicho nacho. Pongezi zaidi ni kuwa na akili ya kuomba ushauri kabla ya kuanza kuzitumbua
Poleni na kazi wadau,
Mungu atusaidie kupata zaidi katika miangaiko yetu ya kila siku. Mungu ni mwema nyakati zote, nikiwa kama kijana Nipo mwaka wa pili udsm katika familia wanandugu tumeuza jengo flani la mzee na kufanikiwa kugawana kila mmoja million 386.
Plan yangu kubwa ni kuwekeza katika majengo ya kupangisha, kwa heshima kubwa ya wadau mbalimbali mlio humu nilikua naomba mawazo yenu ni jinsi gani naweza fanikisha lengo langu na niwekeze hasa katika majengo ya aina gani na yatayonilipa pesa nzuli (niwekeze Dar, Kilimanjaro, Arusha au Dodoma)
Sent from my iPhone using JamiiForums
Sent using
Jamii Forums mobile app