Habarini za leo wadau!
Nimepata wazo la biashara, nataka nikodi flem nifungue mgahawa,,nafikiria kumtafuta mama yeyote ili aniendeshee, yani namuanzishia kila kitu halafu yeye anaendelea. Nataka nikubaliane nae awe ananipa kiasi fulani cha faida tu aidha kwa siku au kwa wiki.
Basi wadau naomba wenye uzoefu na hii biashara au changamoto zozote tushirikishane!
Mtaji wangu ni laki saba. 700,000/=
je umepata location sahihi? Je watu wa maeneo uliyochagua umewasoma vizuri? Maana mgahawa wa temeke sio wa mikocheni!!!!
Nimefanya kautafiti kidogo, location zipo barabara mbili zime cross, zipo karibu na flemu na zinahusisha waenda kwa miguu kwa wingi. Pia hakuna mgahawa hapo karibu.
Habarini za leo wadau!
Nimepata wazo la biashara, nataka nikodi flem nifungue mgahawa,,nafikiria kumtafuta mama yeyote ili aniendeshee, yani namuanzishia kila kitu halafu yeye anaendelea. Nataka nikubaliane nae awe ananipa kiasi fulani cha faida tu aidha kwa siku au kwa wiki.
Basi wadau naomba wenye uzoefu na hii biashara au changamoto zozote tushirikishane!
Mtaji wangu ni laki saba. 700,000/=
Je Unazani ni biashara sahihi ambayo itakutoa kimaishaaa....
Wewe una fanya nini mpaka biashara yako umwachie mtu?
Kama utategemea waenda kwa miguu na sio wakazi wa hapo, inabidi uwe na mgahawa unaofanana na wateja wako
Nafanya kazi mkuu, nimeajiriwa...hizo ni harakat tu za kuongeza kipato. Si unajua tena maisha magumu!!
Lazima utakua mwalimu wewe. Safi sana kamata fursa twende kazi
Kivipi mkuu, embu nifafanulie.
ndugu yangu usithubutu kufanya jambo hili kwa kumtegemea mfanyakazi bila uwepo wako itakula kwako mazima?labda ungechukua likizo ya mwenzi mmoja ukae hapo ujue mapato na matumizi kwa cku ujue kg moja ya mchele inatoa sahan ngapi na faida yako ukishasoma mazingira ndan ya mwenz hapo utakuwa na uwezo wa kumwachia huyo mpishi ukijua kwamba endapo atapika kg 10 ni sahan ngap na faida ipoje nakuambia hivi coz hii ni kazi yangu ila mimi mgahawa wangu upo chuoni so ninauhakika wa wateja na asikuambie mtu biashara ya chakula inalipa sana.cha msingi jitahidi usafi na lugha nzuri kwa wateja