Biashara ya mama ntilie

Biashara ya mama ntilie

KIRIKIOU

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2014
Posts
241
Reaction score
57
Habarini za leo wadau!

Nimepata wazo la biashara, nataka nikodi frem nifungue mgahawa, nafikiria kumtafuta mama yeyote ili aniendeshee, yani namuanzishia kila kitu halafu yeye anaendelea.

Nataka nikubaliane nae awe ananipa kiasi fulani cha faida tu aidha kwa siku au kwa wiki. Basi wadau naomba wenye uzoefu na hii biashara au changamoto zozote tushirikishane!

Mtaji wangu ni laki saba. 700,000/=
 
Biashara ya chakula inahitaji usimamizi wa karibu sana ili iweze kuendelea, ukimuachia kila kitu afanye huyo mama hakikisha awe mwaminifu kwasababu yahitaji uaminifu sana kwenda kunua mchere wa Tshs 2500 wakati wa tshs1800 upo pia au yahitaji uaminifu sana kumwaga mafuta yaliyotumika kukaanga chips mara nyingi ilihali ukiendelea kuyatumia hakuna mteja atakayestukia wala mmiliki wa biashara.
 
Habarini za leo wadau!

Nimepata wazo la biashara, nataka nikodi flem nifungue mgahawa,,nafikiria kumtafuta mama yeyote ili aniendeshee, yani namuanzishia kila kitu halafu yeye anaendelea. Nataka nikubaliane nae awe ananipa kiasi fulani cha faida tu aidha kwa siku au kwa wiki.

Basi wadau naomba wenye uzoefu na hii biashara au changamoto zozote tushirikishane!
Mtaji wangu ni laki saba. 700,000/=

Je, umepata location sahihi? Je watu wa maeneo uliyochagua umewasoma vizuri? Maana mgahawa wa Temeke sio wa Mikocheni!!!!
 
je umepata location sahihi? Je watu wa maeneo uliyochagua umewasoma vizuri? Maana mgahawa wa temeke sio wa mikocheni!!!!

Nimefanya kautafiti kidogo,,location zipo barabara mbili zime cross, zipo karibu na flemu na zinahusisha waenda kwa miguu kwa wingi. Pia hakuna mgahawa hapo karibu.
 
Nimefanya kautafiti kidogo, location zipo barabara mbili zime cross, zipo karibu na flemu na zinahusisha waenda kwa miguu kwa wingi. Pia hakuna mgahawa hapo karibu.

Kama utategemea waenda kwa miguu na sio wakazi wa hapo, inabidi uwe na Mgahawa unaofanana na wateja wako
 
Habarini za leo wadau!

Nimepata wazo la biashara, nataka nikodi flem nifungue mgahawa,,nafikiria kumtafuta mama yeyote ili aniendeshee, yani namuanzishia kila kitu halafu yeye anaendelea. Nataka nikubaliane nae awe ananipa kiasi fulani cha faida tu aidha kwa siku au kwa wiki.

Basi wadau naomba wenye uzoefu na hii biashara au changamoto zozote tushirikishane!
Mtaji wangu ni laki saba. 700,000/=

Je, Unazani ni biashara sahihi ambayo itakutoa kimaishaaa....
 
Je Unazani ni biashara sahihi ambayo itakutoa kimaishaaa....

Ndo navyodhan,ila nafanya hvyo kulingana na huo mtaji. ila kama una bsness idea kwa huo mtaji waweza nipa pia.
 
Kivipi mkuu, embu nifafanulie.

Mgahawa wa wapita njia una vitu vinavyofanana nao, kwa mfano,juisi, chips, maziwa fresh, maji ya kunywa, bites, matunda, asali. Vitu vnavoharibika haraka usiweke. Nenda pale kkoo shule ya Uhuru kuna migahawa miwili ya jinsi hiyo, kaibe ujanja.
 
Ndugu yangu usithubutu kufanya jambo hili kwa kumtegemea mfanyakazi bila uwepo wako itakula kwako mazima?labda ungechukua likizo ya mwenzi mmoja ukae hapo ujue mapato na matumizi kwa cku ujue kg moja ya mchele inatoa sahan ngapi na faida yako ukishasoma mazingira ndan ya mwez hapo utakuwa na uwezo wa kumwachia huyo mpishi ukijua kwamba endapo atapika kg 10 ni sahani ngapi na faida ipoje nakuambia hivi coz hii ni kazi yangu ila mimi mgahawa wangu upo chuoni so ninauhakika wa wateja na asikuambie mtu biashara ya chakula inalipa sana.cha msingi jitahidi usafi na lugha nzuri kwa wateja.
 
ndugu yangu usithubutu kufanya jambo hili kwa kumtegemea mfanyakazi bila uwepo wako itakula kwako mazima?labda ungechukua likizo ya mwenzi mmoja ukae hapo ujue mapato na matumizi kwa cku ujue kg moja ya mchele inatoa sahan ngapi na faida yako ukishasoma mazingira ndan ya mwenz hapo utakuwa na uwezo wa kumwachia huyo mpishi ukijua kwamba endapo atapika kg 10 ni sahan ngap na faida ipoje nakuambia hivi coz hii ni kazi yangu ila mimi mgahawa wangu upo chuoni so ninauhakika wa wateja na asikuambie mtu biashara ya chakula inalipa sana.cha msingi jitahidi usafi na lugha nzuri kwa wateja

Sio tu achhukue likizo yeye anatakiwa kuwepo full time yeye ndo inititor wa Idea na yeye ndo anatakiwa kuipeleka idea yakwe kwa nex step.

Ushauri wangu kama hujajipanga acha kwanza kusanya mtaji na ukiona uko sawa Choma meli moto na ingia front line kupambana, Vingenevyo utajikuta mshahara ndo unaenda kulipa pango la huyo hoteli
 
Back
Top Bottom