Mimi nilipokua nikienda Kariakoo kwa mishe zangu, ilikua lazima nile Combo ya Matunda, sikuwahi kuona yakiuzwa Posta ila nilikua naona yanauzwa Kariakoo tena na Wafanyabiashara wengi tofauti...!
Matunda yanapendeza yakiwa na ubaridi kidogo, matunda yanaanza kulika kuanzia asubuhi mpaka jioni....!
Huwezi kusema ni watu ama wafanyakazi wa kazi flani ndo walaji wa Matunda, yoyote anayeyaelewa anakula!
Kontena kwa 1,000 na nusu yake kwa 500 naona ni fair price!
Matunda yana walaji wake, labda katika sehemu yenye movement kwa wastani wa watu 500 wataopita jirani na Biashara yako kwa siku, labda wateja wa Matunda wakawa 50 tu...!