Biashara ya Matunda na Mbogamboga.

Biashara ya Matunda na Mbogamboga.

Joined
Jun 11, 2019
Posts
2
Reaction score
0
Wanajamvi wasalaam,

Mimi ni kijana, mkulima mdogo wa matunda na mbogamboga, ninapambana na hali yangu yenye changamoto lukuki. Moja ya changamoto kubwa inayonielemea ni kuhusiana na soko la hizi bidhaa ninazozizalisha, mara zote nimefika karibu na kukata tamaa kwani sijapata bado yale mafanikio ninayoyaota na jambo kubwa linalonitupa ni kuwauzia wafanyabiashara (wachuuzi) wanaokuja moja kwa moja shambani lakini sasa nimepiga moyo konde nataka nikauze mwenyewe kwenye masoko yaliyopo mjini Dar es salaam (vetenari/Sterio) kwa sasa nategemea kuvuna tani mbili za tikiti maji.

Naomba wenzangu waungwana, wenye uzoefu na uelewa mnisaidie ushauri kuhusiana na haya yafuatayo, natanguliza shukrani.
i. Tozo/ushuru ambao utanikabili katika mageti ya maliasili wakati nimejitwika kamzigo kangu kuelekea sokoni.
ii. Gharama za ushuru wa soko na madalali endapo nitafikisha mzigo wangu salama sokoni (Vetenari/Sterio).

Naomba kuwasilisha, Ahsanteni..
 
Matunda ya aina gani na mboga za aina gani?

Kwenye biashara lazima ujue unawalenga watu gani na kwa nini?

Unalima lets say Tikitiki maji unajua fika wazalishaji ni wengi sana sokoni na unakuta hata Market share inapungua.
 
Hata ukijitishwa ukapelaka bado unaweza kuta hajatatia changamoto na huenda ukaongeza Changamoto zaidi.
 
Navyoona wengi wetu hapa tunalimia mtaandaoni tu syo mashambani hivyo nachokushauri nenda pale vetenari kamtafute mkuu wa soko umuulize taratibu za kufatwa pale, tokea hapo utaendelea kupata uzoefu
 
hii ndo shida yetu watu weusi. unaanzisha biashara kisha ndi unatafuta soko. ni kama vile kufungua banda la kitu moto pemba hivi unategemea kuuza kg ngapi??? kitu cha kwanza ni kujiuliza ni nani atakaye nunua bidhaa yako. na je anaweza kukulipa bei unayotaka???
 
Back
Top Bottom