Biashara ya mbao Vs Ufugaji wa kuku

Nimekuelewa mkuu sasa 1*8*12 za mlingoti mwekundu na mweupe usisahau, ulivyoandika hapo juu ndiyo nichokuwa nahitaji leta kama hivyo ulivyooredhesha sasa mkuu ww unapatikana wapi.
 
Nakumbuka ulishawahi leta mchanganuo flani wa kuku 1000 kwenye Uzi flani hivi sijui u nakumbuka? [emoji23] [emoji23] [emoji23]

Nikajua unafuga Kumbe ulikuwa umekopi tu mahali aiseee
 
nimekuelewa mkuu sasa 1*8*12 za mlingoti mwekundu na mweupe usisahau,ulivyoandika hapo juu ndiyo nichokuwa nahitaji leta kama hivyo ulivyooredhesha sasa mkuu ww unapatikana wapi
Mkuu, wewe unahitaji mbao za aina ipi na size ipi.? Naweza kukusaidia mawazo..
 
TEAM B-13,

Biashara ya mbao imejaaa dhuruma sana tena sana ukiwa mnyonge utalizwa sana coz hiyo biznez sio ya Cash nyingi ni mali kauli,ndo maana wanauana sana.
 
Mlingoti mweupe na mwekundu, mninga, na pines ziwe 1*8*12,2*4*12,2*2*12,1*4*12

Sent from my itel it1408 using JamiiForums mobile app
Leo nitakupa bei za Mlingoti mweupe kwanza.

1*8*12 Unaweza kupata kwa Tshs. 2000 - 3000.

2*4*12 = Tshs. 1000 - 1500

2*6*12 = Tshs. 2000 - 3000.

Pines.
1*4*12 = 2500 - 3000
2*4*12 = 2000 - 2500
2*6*12 = 2000- 2500

Ushauri: Ili ku-maxmize profit ni vema ukanunua miti na kuchana mwenyewe kuliko kununua mbao zilizochanwa tayari.

Kuhusu Mninga bei ni kwa mita za ujazo.
Mita moja ya ujazo unaweza kupata kwa Tshs. 260,000 . Hiyo ni gharama ya kulipia Serikalini pekee. Bado hujaweka gharama za uchanaji. Mita moja ya ujazo inaweza kutoa mbao kuanzia 20- 30 kwa kutegemea na size ya ubao husika.

Kwa mfano: Mbao 18 zenye size ya 1*8*12 ni sawa na mita moja ya ujazo.

NB: Hizo gharama za Milingoti na Mipaina ni kwa Mkoa wa Njombe.

Gharama za Miti ya Asili( Mninga) ni Constant mahala popote.
 
Nashkuru mkuu ubarikiwe mlingoti mwekundu usisahau kunipa bei zake.
 
Mkuu, hazitofaiti sana na mbao nyeupe za mlingoti. Utofauti wake mdogo ni ktk hizo bei za mbao nyeupe uongeze kuanzia tshs. 1000-2500 .
mkuu hivi hizi mbao naweza kupata njombe sehemu gani
 
mkuu hivi hizi mbao naweza kupata njombe sehemu gani
Unaweza kuzipata Mkoa mzima wa Njombe. Wilaya zake zote isipokuwa Wilaya ya Wanging'ombe, Kilimo cha Miti ni maarufu. Mkoa wa Njombe una Wilaya za Njombe, Makete, Ludewa na Wanging'ombe. Kwà hiyo ni chaguo lako, either uende Ludewa, au Makete au Njombe yenyewe. Kadri unavyozama Maeneo yà Ndani zaidi ndo bei inakua nafuu zaidi, japo pia gharama za usafirishaji Ndo zinakua zinaongezeka kidogo.
 
Nashkuru mkuu.
 
Hongera mkuu kwa mchanganuo mzuri hizo bei ni soko lipi mkuu?
 
Ngoja niongeze nyama kidogo juu ya hili la mbao

Biashara ya mbao hususani nyeupe ipo ktk makundi almost matatu

1. Huyu ni yule mfanya biashara anae vuna miti na kuichana kisha kuziuza mbao zake huko huko shamba kimsingi kundi hili yeye kajikita ktk kuvuna tu katika kundi hili kuna aina mbili kuna wale wavunaji wadogo yani wale wenye mitaji midogo ambao huvuna sanasana miti ya watu binafsi hii kwasababu ya uhaba wa mitaji yao na kundi la pili ni wavunaji wakubwa hawa mostly wanapatikana mafinga hawa wanamitaji mikubwa then wanavuna miti ya serikali ambayo inazalisha mbao bora na hata ktk soko la ushindani popote mbao yake haishindwi ingawa hapo ni lazima uwe na mtaji kweli mkubwa

2. Kundi la pili ni yule mfanya biashara wa mbao ambae yeye anatoa mbao shamba kuja kuziuza mjini kwa maana anatoa sehem ya uvunaji na kuleta mzigo mjini kama vile mafinga mjini, Njombe Mjini, na hata makambako atleast kundi hili halitumiii mitaji mikubwa sana

3. Kundi la tatu ni wale wafanya biashara wanaotoa mbao mafinga, Njombe na nk kupeleka masoko makubwa kama Moro, Dar, Mwanza, Arusha, Nairobi nk

Sasa ntaelezea kidogo kundi la 3

Hilo kundi la tatu linahitaji msingi mkubwa kidogo kwa mfano unataka kupakia mbao fupi yaani za futi 12 gari moja ni lazima uwe na at least mtaji wa Ml 17 hiyo ni kwa gari utakayo pakia njombe kwasababu wastani gar ikipakia njombe hubeba wastani wa pics 2700-3200 hutegemea na mchanganyiko wa size ya mbao.

Changamoto kubwa kwa masoko ya mbao haulipwi cash masoko mengi ukishusha gari yako utapewa nusu ya thamani ya mzigo then hela nyingine utamaliziwa kulingana na maelewano ni ndio huwanya watu wengi kushindwa kufanya biashara hii

Lakini ukiwa na mtaji hata wa gari mbili au tatu at least utafanya kwa raha.
 
nashkuru mkuu
 
Hongera mkuu kwa mchanganuo mzuri hizo bei ni soko lipi mkuu?
Wakuu samahanini kwa kuwa mbali na uzi kwa muda. Michongo ya porini sometimes ndio inatuweka mbali na net. Hizo bei ni ktk soko la Makete mjini namaanisha ndani ya mji mdogo wa Iwawa ambako ndio makao makuu ya wilaya ya Makete. Yaani namaanisha mitaa ya Ndulamo, Ludihani, Ivalalila, Mwongolo, Mpangala, Dombwela na Maleutsi. Pamoja na vijiji vya pembeni kidogo ya mji kama Kisinga, Mago, Ugabwa, Ivilikinge, Isapulano na Ujuni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…