Ngoja niongeze nyama kidogo juu ya hili la mbao
Biashara ya mbao hususani nyeupe ipo ktk makundi almost matatu
1. Huyu ni yule mfanya biashara anae vuna miti na kuichana kisha kuziuza mbao zake huko huko shamba kimsingi kundi hili yeye kajikita ktk kuvuna tu ktk kundi hili kuna aina mbili kuna wale wavunaji wadogo yani wale wenye mitaji midogo ambao huvuna sanasana miti ya watu binafsi hii kwasababu ya uhaba wa mitaji yao Na kundi la pili ni wavunaji wakubwa hawa mostly wanapatikana mafinga hawa wanamitaji mikubwa then wanavuna miti ya serikali ambayo inazalisha mbao bora na hata ktk soko la ushindani popote mbao yake haishindwi ingawa hapo ni lazima uwe na mtaji kweli mkubwa
2 kundi la pili ni yule mfanya biashara wa mbao ambae yeye anatoa mbao shamba kuja kuziuza mjini kwa maana anatoa sehem ya uvunaji na kuleta mzigo mjini kama vile mafinga mjini, Njombe mjini, na hata makambako atleast kundi hili halitumiii mitaji mikubwa sana
3 Kundi la tatu ni wale wafanya biashara wanaotoa mbao mafinga, Njombe na nk kupeleka masoko makubwa kama Moro, Dar, Mwanza arusha Nairobi nk.
Sasa ntaelezea kidogo kundi la 3
Hilo kundi la tatu linahitaji msingi mkubwa kidogo kwa mfano unataka kupakia mbao fupi yaani za futi 12 gari moja ni lazima uwe na at least mtaji wa Ml 17 hiyo ni kwa gar utakayo pakia njombe kwasababu wastani gar ikipakia njombe hubeba wastani wa pics 2700-3200 hutegemea na mchanganyiko wa size ya mbao
Changamoto kubwa kwa masoko ya mbao haulipwi cash masoko mengi ukishusha gari yako utapewa nusu ya thamani ya mzigo then hela nyingine utamaliziwa kulingana na maelewano ni ndio huwanya watu wengi kushindwa kufanya biashara hii
Lkn ukiwa na mtaji hata wa gari mbili au tatu at least utafanya kwa raha.