Biashara ya mchanga mikoa ya pwani

Biashara ya mchanga mikoa ya pwani

Mtego wa Noti

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2010
Posts
2,591
Reaction score
1,616
Igweeeee!!!...Naamini wote humu ndani mko salama. Kuna hii biashara ya kuuza mchanga ambayo watu wameanza kuvutiwa nayo ambapo wananunua mashamba yenye mchanga na kuanza kuuza mchanga. Kwa ambao wameshaijaribisha hii biashara ina changamoto zipi? Nataka nianze kusaka maeneo ya kuwekeza kwenye biashara hii maana hali ni tete mifukoni.
Nimeona ikifanyika hasa kwenye maeneo ya Mkoa wa Pwani hasa maeneo ya Bagamoyo, Kibaha, Mlandizi na Mkuranga.
Je, ukifuata vibali vyote ukawa navyo, na ukaianza hii biashara kuna changamoto zingine tarajiwa? Naombeni msaada
 
Nasikia inalipa sana maana uhitaji wake ni mkubwa sana. Ukifanikiwa ukapata tenda ya kupeleka mchanga mahali ndio unatoboa kabisa. Komaa uanze halafu utatuletea mrejesho. Sijasikia changamoto zaidi ya watu wa mazingira kama hauna vibali vyao
 
Biashara ya kuchimba mchanga kwa juu juu inaonekana ina faida ila kiundani figisu nyingi sana.

Kuna jamaa yetu alifanya biashara hiyo mkuranga, kwa kifupi lazima ule uwe na koneksheni na maliasili, wadau wa mazingira, madiwani, halmashauri, wenyeviti wa mitaa/vijiji na wajumbe wa serikali za mitaa.

Uendelevu wa biashara ya mchanga kama mmiliki wa machimbo au mgodi unaweza ukaingia dosari kama moja wapo wa hao wadau tajwa hapo juu wasipo nufaika na mradi wako. Kwa hiyo ni biashara fulani ya kimchongo mchongo ingawa ukiwa umejipanga na unachanga karata zako vizuri ukiwa na soko au miradi mikubwa ya ujenzi itakulipa kwa wakati na sio kutegemea wateja binafsi.
 
Asante kwa ushauri huu. Kumbe inabidi kula na wengi. Ujaribu kuwashika ili mambo yakae vzr.
 
Nenda chanika mvuti uko utakuta kila kitu kipo swa au maeneo ya kitonga
 
Back
Top Bottom