INAUZWA Biashara ya mchele kutoka Morogoro

INAUZWA Biashara ya mchele kutoka Morogoro

Hapo panatakiwa kumaanisha hivyo hivyo au panahitaji marekebisho?
Asante kwa kuliona hilo mkuu,nimekosea kuandika hapo,nitafanya marekebisho .ila ni 120,000Tshs,ambayo ni 1,200 kwa kilo moja
 
Anayeupa grade ni taasisi gani au ni wewe mwenyewe?
Boss huku kidogo kuna wabobezi (wengi ni mabwanashamba)kwahiyo huwa wanaangalia mbegu ya mpunga na namna unavyo chomoka baada ya kukobolewa ,kwahiyo wanatusaidia ku-sort kabla hujatoa mzigo mashineni.
Na ndio wanaotushauri mbegu ipi ya mpunga inauwezekano mkubwa wa kukupatia mchele super na ipi huwa ni ya kubahatisha.Kwa wanao-export pia kama wanahitaji professional sorting kuna watu wapo huku (mamlaka husika)wanaweza kusaidia zaidi .
Natumaini nimekujibu .
 
Niliwahi kutumiwa 'magunia' matatu ya mchele kwa reli ya Tazara. Treni imefika tangu saa 12 asubuhi niko natafuta mzigo siuoni. Mawazo yangu yalikuwa kuwa gunia la mchele la kg 100 litakuwa kubwa kama gunia la mahindi! Kumbe ni ka kiroba kadogo tu!
Nilifanikiwa kuyaona baada ya kuona jina langu kwenye kafurushi kadogo hivi. Nilishangaa sana.
Mmh kama ulilipima sawa mkuu,ila 100kg huwa si haba
 
Kilo 25 huuzi? Si kila mmoja wetu hapa atakuwa na uhitaji wa kilo mia kwa matumizi ya nyumbani
USHAURI:
Fungasha kilo 10, 10 utatuokota wengi sana
Kwahiyo nikufungie ngapi kaka mkubwa.?
 
Ninauza mchele super 1500Tshs kwa kilo. Nakusafirisha mzigo kuanzia kg100 kwa wateja wa Dar es Salaam utapokea mzigo wako Mbezi. Pia, kwa wanaohitaji kununua mchele/mpunga kwasasa kwaajili ya uwekezaji, nipe oda.
UPDATES
Jipatie mchele super unaochambuka vizuri kwa 1700Tshs@ 1kg.
Ndani ya Dar es salaam unaletewa mzigo wako mlangoni.

Karibuni

View attachment 1833869
Unanukia kama wa Kyela?
 
Nataka kuja kuuona , uko wapi? Pia naweza pata ule mchele wa magugu?
 
Back
Top Bottom