Biashara ya Michezo ya Video (Video Games): Jifunze Uendeshaji, Changamoto na Faida Zake

thinka

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
334
Reaction score
153

Nataka nianzishe biashara ya kuchezeshaa game aina ya playstastion ila kabla sijaanza inanibd nifanye utafiti kuhusu biashara. naomba kwaa aliye na uzoefu na hilo aniambie faida na hasara zake.


WADAU WANAOHITAJI MUONGOZO KUHUSU BIASHARA HII

MAJIBU NA MICHANGO YA WADAU
 
Mkuu kama wewe ni great thinker usifanye hii biashara, naichukia sana, inafanya watoto wawe wajinga sana, Huu utandawazi unawaathiri sana watoto, make wanatoroka shule na kwenda kucheza hizo game, usiangalie tu pesa, au uweke sheria kwamba masaa ya shule hakuna mtoto kusogea hapo.
 
Biashara hiyo sio mbaya lkn eneo ni muhimu,pili vifaa kama unachezesha PS2 nunu vidude au mikono ya psone ni migumu kweli, kwenye upande wa tv nunua inchi 28.

CD weka mpira, magari, ngumi.

Jaribu kuweka kitu kama membershp ya duka lako mfano wewe unachaji 1000 kwa saa au miatano, jaribu kuweka kuwa mtu anasajili kwa 5000 badala ya kupata masaa matano anapata saba unusu. Lakini lazima uwe na game nyingi.

Ps3 sio wapenzi sana lkn usiweke zaidi ya moja lkn PS2 imezoeleka na haina hasara kwenye vifaa vyake vikipata kuharibika.
 

Hapo sasa inabidi awe anafungua kwanzia sita unusu hadi jioni kwa siku za shule, weekend kwanzia asubuhi.
 
Habarini wadau.

Huku mtaani kwetu kuna ka biashara kanashamiri sana siku hizi kila kona ya mtaa utaona kakibanda ka michezo ya watoto yaani Play Station. Inaonekana kama inalipalipa hivi kwani kila uchao vyaongezeka.

Ombi. Kuna mdau yoyote mwenye kujua juu ya hili ili atushawishi kama ni kabiashara kazuri hasa kina sisi kapuku tujiweze kujihifadhi na maisha haya magumu kila leo?

Asanteni wadau.
 
Na wewe unataka ujiunge katika biashara ya kuharibu akili za watoto?
 
Na wewe unataka ujiunge katika biashara ya kuharibu akili za watoto?

Sidhani kama inaharibu akili. Zama hizi sio kama zenu zile Big Papa enzi zenu za utoto. Viwanja vingi, Michezo kibao ya kitoto. Enzi hizi hakuna playground za watoto, afu wanazaliwa kwa fujo so i think is a kind of enjoyment to them. Mi naona kama ndo wanakua na akili aktive vile kwani hiyo michezo yenyewe inawafanya wawe very active esp in decission making etc.
Embu niambie inalipa?
 
Inalipa, tafuta sehemu yenye watu wengi haswa uswahilini weka kama 6 ivi hela yako itarudi na faida tele.
 
Ukitaka ufanikiwe kibiashara uwe na passion nayo na uijue vizuri.

Mara nyingi ukiiga biashara kutoka ni ngumu sana. Good luck!

Usisahau ukitaka playstation 3 nitafute nikuuzie na cd zake maana umri umenitupa mikono, mishe za maisha nyingi sana nakosa muda wa kuicheza.
 
Ukiifanya kisasa ukaweka flat tv utaingia katika ushindani mzuri.
 
Hizi biashara uwa zinawafanya watoto wawe wezi hivyo kama unania njema fanya ruhusa kwa watoto walio juu ya miaka 18.
 
Kuna PS 2 inauzwa hapa 200000 bei maelewano inaweza pungua unapata na cd na 2 pads
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…