Ushauri wangu chukua ps4 moja na ps3 moja. Na tv 2 za inch 32.Mkuu sitatumia ps 4, nitatumia ps 3 2 na tv inch 32, 2.....hiyo kwa bei ya laki 3 vyote ni mil 1 laki 2.....laki 150 padi za akiba laki 150 kodi miezi 3....
nitachezesha mechi 2 za dakika 10 kwa 500.....
kwa mwanzo wa hii hiashara ni heri ps3, ili ujifunze biashara inaendaje na changamoto za machine na pad na wateja wako unawasoma....maana PS4 padi zake zinafika hadi 100 sasa ukipata changamoto ya pad kama hujajipanga unaona hailipi
Ni mradi mzuri sana. Haumizi kichwa na ni operations cost yake ni ndogo sana. Cha umuhimu location na usimamizi mzuriKwa hii mitaa yetu huu mradi haupo ngoja niupe nguvu
Mungu akubarikiSikia.
*Ps4 chukua moja ni 650k. Chukua iliyochipiwa ndo inafaa kwa biashara.
*ps3 chukua 2 kwa 320k kwa kila moja.
*ps2 chukua 2 kwa 130k kwa kila moja.
* tv chukua 2 za inch 32 kwajili ya ps3 na moja ya inch 42 kwaajili ya ps4. Nenda kwa wapemba mbweni utapata inch 32 kwa 300k na inch 42 kwa 450k za mtumba. Za mtumba zitadumu muda mrefu sana. Nasisitiza usinunue za dukani ni hasara.
*chukua inch 22 kwaajili ya ps2. Vilevile za mtumba.
* nunua gaming pc used kwa 350k. Tafuta hawa jamaa wanaitwa camara huwa wanazo. Chukua na monitor ya inch 22 au tv yenye hdmi au vga port. Hii itakusaidia kuweka games zenye kuharibu pad mf. Mortal kombat x au xl au 11. Pad za pc ni ngumu na gharama yake ni 8k pad moja k.koo.
*ps4 na ps3 weka games za mpira na mission ambazo haziharibu pad. Pc tia game za ngumi na zenye kuharibu pad.
BEI
*Ps3 na ps4 mpira ni 500 kwa dakika 10
Ps2 mpira mechi 2 500 na ni dakika 10
*games zingn za mission ni dakika 15 kwa 500 kwa ps3 na ps4 na dakika 30 kwa ps2.
LOCATION*
tafuta sehemu yenye watu wengi hasa vijana na yenye usalama. Fremu ni kati ya 50k hadi 70k. Usiogope itakulipa tu.
* dumisha usafi na kama unamweka mtu basi mlipe kwa siku elf 5 mpaka elf 7 kwa siku kutegemea na mahesabu anayokuletea.
* fanya mwenyewe kama mwezi hivi ndo umpe kijana. Na uwe muda mwingi unapiga jicho maana wakizoea huwa wana tabia ya udokozi.
* biashara ikikubali weka cctv camera ni kama 450k kila kitu. Itasaidia usalama na pia kum monitor kijana.
*VIFAA VINGINE
*stabilizor ni muhimu sana kwaajili ya kulinda vifaa vyako.
*pads ni za kuchunga hasa za ps4 maana ndo kikwazo kikubwa cha biashara hii.
*kibali toka serikali za mtaa ni 20k tu na hakuna kenge atakaye kusumbua
●muda wa kufungua ni saa 3 asubuhi hadi saa 5 usiku. Ila siku za shule hakikisha madogo hawaingii chini ya saa 7 mchana.
● kwenye ps4 jaribu kuweka hata kijisofa itaongeza hadhi.
****** FAIDA ********
* ukifikia hayo juu jiandae kula kuanzia 20k hadi 30k kwa siku za kawaida na 40k kwa siku za weekend.
KUNA WATU WANAPENDA KUONGEA VITU WASIVYO VIJUA. KAMA HUJUI KITU NI BORA KUKAA KIMYA
Amina mkuuMungu akubariki
Ku update version ya game iliyo installed tayari au kufanya new installation ndio 10GB +?Wakumbushe pia, kutengeneza controller kwenye hitilafu ndogo kabisa ni kuanzia elfu5... Na inaenda hadi elfu 30.
Lerner hawajui kuwa analogue haihitaji nguvu, ikimeguka tu, kuibadili ni kipengele.
Ku-update game eg FIFA au GTA ni GB10 mpaka 20 inategemea na signal ya network.
Mwisho wa yote niwatakie mafanikio mema.
Hii ya game pc ndo naona iko vizuri ulivyoichanganua sijawahi itumia hii embu nielekeze unaunganisha vipi pc mpka unacheza kwenyeTv.Faida ya kuwa na gaming pc. Magame kibao unawekaView attachment 1756750
Shukrani sana kiongozi ubarikiwe.Kwa ps mcheki huyu jamaa. Yupo gerezani kariakoo. Anauza na kuchip ps. Anaingiza games.
Ps3 anauza 320k
Ps4 kuanzia 650k
Ps2 120k.
Hii ni pamoja na accessories zote.View attachment 1760548
Karibu mkuuShukrani sana kiongozi ubarikiwe.
KaribuDah! Uzi mzuri sana huu ngoja niweke kambi.
Simple tu. Tv inakuwa kama monitor. Either uunganishe kwa VGA au hdmi.Hii ya game pc ndo naona iko vizuri ulivyoichanganua sijawahi itumia hii embu nielekeze unaunganisha vipi pc mpka unacheza kwenyeTv.
Yah kabisaWakumbushe pia, kutengeneza controller kwenye hitilafu ndogo kabisa ni kuanzia elfu5... Na inaenda hadi elfu 30.
Lerner hawajui kuwa analogue haihitaji nguvu, ikimeguka tu, kuibadili ni kipengele.
Ku-update game eg FIFA au GTA ni GB10 mpaka 20 inategemea na signal ya network.
Mwisho wa yote niwatakie mafanikio mema.
Wakuu pes4 ni bei gan nataka kujaribu hii biashara
Mkuu ni wap ntapata bodaboda mbili kwa 2.5m zikiwa mpya ? Tuanzie hapoKUNA HII BIASHARA YA GAMES CENTRE kuna vijana wanapiga hela sana siku izi hasa izi PS4 iko hivi
Ps4 moja complete ni 550K mpk 650k Tv inch 40
Hapo una wastani wa kuingiza elfu 10 mpk elfu 20 kwa siku
Ukiwa nazo Ps4 mbili na Tv 2 una weza piga elfu 20 mpk 30 kwa siku
Je, ukiwa nazo Ps4 na Tv 4?
Hapo sawa sawa na mtaji wa kununua bodaboda 2 yaani m2.5 ambazo kwa siku ni elfu20
Lakini GAMES center mtaji wa m2.5 kwa siku ni elfu elfu 40
Unachotakiwa ni kujua tu eneo zuri la kuweka biashara yako wachezaji wengi na wanachuo vijana wa umri wa Kati
Generator muhimu kama sehemu ulipo kuna shida ya umeme
Kibali cha bodi ya game
Ukipata pata hivyo vitu unapiga hela tu kila siku elfu 40 kwa mtaji wa m2.5 na hakuna mkataba hapo hata miaka 20 unapiga tu hela
Mbona hujapigia bei ya furniture za ndani kama meza ,viti, hujapigia hesabu ya kodi, ....kwa 2.5m bado n haitoshiHiyo ni bei ya game tu ps4
Kutengeneza button moja tu ya pad za PS4 sio chini ya elfu 30.
CD ikisizingua tu, moja sio chini ya 120K OG, ku update mashine sio chini ya 30GBs za internet yenye speed kali.
Mkiongea haya mambo ongeeni kwenye uhalisia wake.
Nafanya hii biashara, usipokuwa makini, watu wavuta analogy joyride kama uoinde wa mshale, utajuta.... Zinameguka, spare elfu 60 [emoji23][emoji23][emoji23]