Biashara ya Michezo ya Video (Video Games): Jifunze Uendeshaji, Changamoto na Faida Zake

Mdogo wangu bado anachezesha kuanzia mwaka 2018 mpaka leo hii
 
Wakati naanza nilikua napata kuanzia 20K - 30K. Nikawa kama nimewashtua wadau so sasa hivi kuna sehemu nne zingine za play station. Now faida ni 10K mpaka 20K+ 30K imekua nadra.

Kulingana na ushindani na eneo ulilopo inawezekana ikawa bora uwe na 3 au 4. Mfano kuna eneo nilienda nilikuta wanachezesha PES 21 & FIFA 21 (PS 4) mechi moja 800 mechi tatu 2000. Wakati nilipo mechi moja kwenye 4 ni 500 na 3 ni 500. Ingawa naona ni bora ukawa na 3 na 4 kwa pamoja.

Biashara nilizofanya with hands on experience ni kuburn cd (muziki na seasons: library) na uboda boda. Katika hizi biashara tatu, kuburn CD kunaweza kukupa pesa kuliko PS kwakua kwa nilipo mimi PS inatakiwa ufungue saa 10 ili kuendana na muda wanafunzi wanakua wamerudi.

Ukijumlisha na competition iliyopo library inatoa pesa easily.
 
Kaka shukrani sana kwa kutoa taarifa bila kuyumbisha.....ofcouse mwaka huu natamani niwe na biashara nje ya kazi nione nilijaribu mtumba hela ikawa kubwa ila changamoto ya location ikanitoa.....

Nitanunua ps 3 moja na 4 nione uelekeo ea biashara kabla sijaongeza

Na hii biashara ukiwa mwenyewe katika eneo hilo utapata sana pesa. Maana haugawani wateja
 
Yea ukiwa mwenyewe ni sawa zaidi ama sivyo uweke kiwango ambacho unaona kitakufaa uwe unapewa na uliyemuacha.
 
Anza na ps2 moja, ps3 na ps4 moja.
 
Niliwahi kufikiria kuwekeza 2.6mil kwenye hii biashara wakuu... lakini sina uzoefu nayo wala taarifa sahihi inalipa vipi...ningependa siku moja nimpate mtu anayeifanya au aliyewahi kuifanya anipe muongozo... Asante
Njoo PM mkuu ikibidi nitakupeleka na field kabisa uone
 
PS 4 mbili na kodi na Tv na ps 3 hiyo hela haitoshi labda uanze na PS4 moja
 
Mkuu nakushauri chukua 4 MBILI ps 3 haina wapenzi kabisa kabisa sikuizi hata watoto hawaichezi
 
Nipo dar mkuu kama unahitaji ABC hadi location nzuri ninaweza kukusaidia mawazo
Shukrani kwa ushirikiano na mawazo Mkuu..
Tayari kuna project nilikuwa nimwanza kuzifanya , napia naendelea na michakto fulani.

Ila mishe zikitulia , nitakurudia tuzungumze zaidi , hata me nilifanya research kidogo
 
Wakuu habari za muda huu, katika tembea tembea zangu mitaani nimekuwa nikiona vijana wengi wakijikita kwenye biashara ya kuchezesha games. Hususani pad games either ps 3 or ps 4 au pc games.

Kama kichwa kilivoeleza hapo juu nilipenda nijue hii biashara ikoje changamoto zake faida zake.

Natanguliza shukrani sana.[emoji120]
 
Mkuu hiyo ni moja ya biashara nzuri sana ukipata location nzuri hasa iwe karibu na chuoni au location yeyote nzuri mtaji Tafuta almost 4 millions kama unataka kuanza na playstation 4 mbili na Tv flats 2 hapo utakuwa umeula sikushauri ununue ps 3 hazina soko mkuu zitakudodea.

Changamoto hapo pad kuharibika ili sio changamoto sana iyo mkuu, Faida ipo kutokana na location ps 4 mechi moja ya dakika 5 half kipindi ni 500 kwa lisaa lisaa limoja Elfu 3 ukipata location nzuri per day kwa ps 4 moja hukosi Maximam Elfu 15 japo inaweza kuzidi ila iyo ni Maximam.

Ni moja ya biashara ya games haichuji bei zake ps 4 moja used 650 unapata complete pad 2 na games ndani yake.
 
Asante mkuu na vipi changamoto zake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…