Biashara ya Mpira inavyoanza kuigharimu Simba

Biashara ya Mpira inavyoanza kuigharimu Simba

kidaru

Member
Joined
Mar 30, 2017
Posts
22
Reaction score
51
Timu ya Simba ilitamba kwenye soka la bongo kwa takribani Miaka minne mfululizo, ikijengwa na wachezaji wenye uwezo Mkubwa na wenye historia ya soka la Afrika.

Baada ya Mo, kuanza kuisaidia Simba msimu wa 2017 - 2018. Simba ilifanya usajili mkubwa wa kuchukua wachezaji wa Azam na baadhi ya nyota wenye ubora kutoka nchi mbalimbali za Afrika, wakiwemo Paschal Wawa, Kagere na wakazidi kuongeza nyota kadri miaka ilivyozidi kwenda. Hii yote ilikuwa ni Kampeni ya Mo kujenga uaminifu wa kuaminika na Simba ili apewe timu.

Msimu wa 2021 kwenda 2022, ni dhahiri sasa Mo amekabidhiwa timu na katiba ya Simba iliyopo inamlinda. Kwa mwelekeo sasa ameigeuza Simba kuwa ''academy " ya kulelea wachezaji ili baadae awauze. Ukiangalia usajili wa Simba msimu huu umejikita kwa vijana kuanzia miaka 20 mpaka 25, ambao wengi wao hawafahamiki kwenye Soka la Afrika zaidi ya kupambwa na Magazeti ya Kibongo na Media tofauti.

Nimeiangalia Simba kwa game mbili za Tp Mazembe na Yanga ni dhahiri sasa, uwezo wa timu ni Mdogo na Ubunifu wa viungo haupo tena. Wachezaji waliopo ambao inaaminika kwenye timu wameshakaa muda mrefu wengi wao umri ushawatupa Mkono na hata ile kasi ya timu haipo tena. Ila kwa sababu ni Biashara ikaonekana waendelee tu kupunguza gharama za usajili wa Nyota wapya.

Simba iliwauza wachezaji wawili tegemeo ambao waliibeba Simba kwenye Ligi tofauti na ikasajili average player wengi wenye umri mdogo ambao hawana uzoefu wa Mechi za Kimataifa. Kilichofanyika ni "kamari "tu.

Sitegemei kuiona Simba ikifika mbali kwenye Michuano tofauti ya Msimu huu na ni ukweli haiwezi kutamba mbele ya Azam au Yanga ambao wameboresha vikosi vyao na wamedhamiria kutwaa Ubingwa. Muda ni mwalimu mzuri na ukweli huu utajulikana baada ya kuisha Msimu.

Bado wana nafasi ya kuweka sawa Kikosi ila kama ndiyo sera ya klabu kwa sasa. Simba haitatoboa kokote. Ukweli lazima uwekwe wazi.
 
Simba Ina wavulana ambao ili watambe wanatakiwa wapewe muda kitu ambacho hakuna shabiki anataka kusikia.

Wenzao Yanga wanaitaji kurudisha ubabe wao katika soka ndio maana wameingia gharama kuleta wachezaji wazoefu.
 
Mchezaji kama kaafiki dili la kuuzwa mwache auzwe, ya nini kumng'ang'ania ili hali kaamua kutafuta changamoto mpya.
Kuuza wachezaji hakukataliwi , Ila uza chuma nunua chuma. Kama ni biashara ya 2b basi nunua wa 1.5 B sio unanunua wachezaji wa thamani za milioni 60 na 70 ukategemea utatoboa, hiyo ni ngumu sana. Ukitaka Makombe wekeza kwenye wachezaji wenye ubora. Sio wavulana wadogo.
 
Jamaa ameshaiharibu timu kwa njaa zake za kuwauza akina Chama
 
Yanga walitufunga kwenye mechi ya pili ya ligi iliyoisha.

Chama alikuwepo na Miquessone alikuwepo.

Tatizo la Simba hatuna mshambuliji mzuri wa kariba ya Prince Dube au Okwi au Kipre Cheche.

Nashanga Simba kila kukicha wanasajiri wakabaji wa katikati tu wakati hawana mfungaji.

Hao akina Peter Banda, na Dunkan Nyoni sioni maana ya usajiri wao wakati hawana msaada wowote wa kuwazidi wenyeji akina Kibu Dennis na Mhilu.
 
Tatizo sio kufungwa, hakuna timu duniani isiyofungwa. Ila tunachoangalia ubora wa wachezaji wa Simba kwa sasa, ukilinganisha na vilabu vingine, unaona kabisa kwa Msimu huu, kuna kazi kubwa ya Kufanya.
Hatuna mshambuliaji wa kariba ya
Prince Dube
Okwi
Kipre Cheche.
Akina Dunkani, Banda, Sakho, Kannute
Sio washabuliaji.
Kwanini hatusajiri washambuliaji makini japo mmoja tu ?
 
Mchezaji kama kaafiki dili la kuuzwa mwache auzwe, ya nini kumng'ang'ania ili hali kaamua kutafuta changamoto mpya.
Tatizo sio kuuza tatizo ni unapouza unayemsajili ni mchezaji wa aina gani, Ana kiwango gani Kama cha yule uliyemuuza, unafanya replacement ya aina gani apo ndo kuna tatizo, duniani kote wachezaji uuzwa akuna anaebisha lakini unaangalia replacement ya maana ambayo aitakuchukua mda mrefu kuupata ubora uleule ya yule aliyeondoka au kuukaribia sio kusajili kuziba tu nafasi iyo sio sawa ndo kitakachowatesa simba msimu huu
 
Timu ya Simba ilitamba kwenye soka la bongo kwa takribani Miaka minne mfululizo, ikijengwa na wachezaji wenye uwezo Mkubwa na wenye historia ya soka la Afrika.

Baada ya Mo, kuanza kuisaidia Simba msimu wa 2017 - 2018. Simba ilifanya usajili mkubwa wa kuchukua wachezaji wa Azam na baadhi ya nyota wenye ubora kutoka nchi mbalimbali za Afrika, wakiwemo Paschal Wawa, Kagere na wakazidi kuongeza nyota kadri miaka ilivyozidi kwenda. Hii yote ilikuwa ni Kampeni ya Mo kujenga uaminifu wa kuaminika na Simba ili apewe timu.

Msimu wa 2021 kwenda 2022, ni dhahiri sasa Mo amekabidhiwa timu na katiba ya Simba iliyopo inamlinda. Kwa mwelekeo sasa ameigeuza Simba kuwa ''academy " ya kulelea wachezaji ili baadae awauze. Ukiangalia usajili wa Simba msimu huu umejikita kwa vijana kuanzia miaka 20 mpaka 25, ambao wengi wao hawafahamiki kwenye Soka la Afrika zaidi ya kupambwa na Magazeti ya Kibongo na Media tofauti.

Nimeiangalia Simba kwa game mbili za Tp Mazembe na Yanga ni dhahiri sasa, uwezo wa timu ni Mdogo na Ubunifu wa viungo haupo tena. Wachezaji waliopo ambao inaaminika kwenye timu wameshakaa muda mrefu wengi wao umri ushawatupa Mkono na hata ile kasi ya timu haipo tena. Ila kwa sababu ni Biashara ikaonekana waendelee tu kupunguza gharama za usajili wa Nyota wapya.

Simba iliwauza wachezaji wawili tegemeo ambao waliibeba Simba kwenye Ligi tofauti na ikasajili average player wengi wenye umri mdogo ambao hawana uzoefu wa Mechi za Kimataifa. Kilichofanyika ni "kamari "tu.

Sitegemei kuiona Simba ikifika mbali kwenye Michuano tofauti ya Msimu huu na ni ukweli haiwezi kutamba mbele ya Azam au Yanga ambao wameboresha vikosi vyao na wamedhamiria kutwaa Ubingwa. Muda ni mwalimu mzuri na ukweli huu utajulikana baada ya kuisha Msimu.

Bado wana nafasi ya kuweka sawa Kikosi ila kama ndiyo sera ya klabu kwa sasa. Simba haitatoboa kokote. Ukweli lazima uwekwe wazi.
Muda wa Muddy sasa kufanya biznes baada ya kupewa timu,maana anasemaga amejitolea sana hela zake...
 
Timu ya Simba ilijengwa na djuma makocha wote wanaokuja walikuwa wanajenga Kwa huyu mwamba

Mkumbukeni aje aijenge tena

Simba walikuwa wakiswichi Sana wakitumia wachezaji mamluki ili kuwafanya wapinza washindwe kuisoma mbinu.

Kingine ni janja janja nje ya uwanja
 
Hakuna namna- mzunguko wa maisha ya mpira ndivyo ulivyo- huwezi kuwa juu siku zote- Kuna kupanda na kushuka- Simba imekuwa juu- kwa misimu minne- asilimia kubwa ikitumia wachezaji wale wale- wanachoka na umri unaenda- Yanga pia Kuna Kipindi walikuwa juu- baadae wakashuka- sasa wanajenga timu ili wapande tena- Kipindi Yanga wako juu- Simba tulikuwa tunajenga timu- tukahamisha kikosi kutoka Azam- kikosi hicho kwa kiasi kikubwa ndio kinatumika mpaka leo-wengi wamechoka- Yanga wamefanya hivyo hivyo wamehamisha sehemu ya kikosi Cha Ac vita- inavyoelekea kitawasaidia- kwa sababu kuwaunganisha ni rahisi- kuliko kuchukua sehemu tofauti tofauti- sio kwenye soka letu tu- hata ulaya- timu zinapanda na kushuka- wote tunaikumbuka Ile Barcelona OG- kwa kifupi Simba msimu huu utakuwa mgumu kidogo kwetu- ukiangalia beki line haiko vizuri- inapitika sehemu zote- katikati unapita - pembeni unapita- Wawa kachoka- Kapombe kachoka- Lwanga mzee wa rafu nyingi- pongezi kwa Manula- la sivyo vilio vingekuwa vikali zaidi-viungo wa juu bado muunganiko- wasambuliaji ndio hao kina Mugalu- tumesajili wachezaji wa wapya- lakini wengi wanakaa benchi - wanaendelea kutumika wale wale wa zamani- kazi iendelee.
 
Back
Top Bottom