Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Huijui biashara ya mpira na wachezaji.Timu ya Simba ilitamba kwenye soka la bongo kwa takribani Miaka minne mfululizo, ikijengwa na wachezaji wenye uwezo Mkubwa na wenye historia ya soka la Afrika.
Baada ya Mo, kuanza kuisaidia Simba msimu wa 2017 - 2018. Simba ilifanya usajili mkubwa wa kuchukua wachezaji wa Azam na baadhi ya nyota wenye ubora kutoka nchi mbalimbali za Afrika, wakiwemo Paschal Wawa, Kagere na wakazidi kuongeza nyota kadri miaka ilivyozidi kwenda. Hii yote ilikuwa ni Kampeni ya Mo kujenga uaminifu wa kuaminika na Simba ili apewe timu.
Msimu wa 2021 kwenda 2022, ni dhahiri sasa Mo amekabidhiwa timu na katiba ya Simba iliyopo inamlinda. Kwa mwelekeo sasa ameigeuza Simba kuwa ''academy " ya kulelea wachezaji ili baadae awauze. Ukiangalia usajili wa Simba msimu huu umejikita kwa vijana kuanzia miaka 20 mpaka 25, ambao wengi wao hawafahamiki kwenye Soka la Afrika zaidi ya kupambwa na Magazeti ya Kibongo na Media tofauti.
Nimeiangalia Simba kwa game mbili za Tp Mazembe na Yanga ni dhahiri sasa, uwezo wa timu ni Mdogo na Ubunifu wa viungo haupo tena. Wachezaji waliopo ambao inaaminika kwenye timu wameshakaa muda mrefu wengi wao umri ushawatupa Mkono na hata ile kasi ya timu haipo tena. Ila kwa sababu ni Biashara ikaonekana waendelee tu kupunguza gharama za usajili wa Nyota wapya.
Simba iliwauza wachezaji wawili tegemeo ambao waliibeba Simba kwenye Ligi tofauti na ikasajili average player wengi wenye umri mdogo ambao hawana uzoefu wa Mechi za Kimataifa. Kilichofanyika ni "kamari "tu.
Sitegemei kuiona Simba ikifika mbali kwenye Michuano tofauti ya Msimu huu na ni ukweli haiwezi kutamba mbele ya Azam au Yanga ambao wameboresha vikosi vyao na wamedhamiria kutwaa Ubingwa. Muda ni mwalimu mzuri na ukweli huu utajulikana baada ya kuisha Msimu.
Bado wana nafasi ya kuweka sawa Kikosi ila kama ndiyo sera ya klabu kwa sasa. Simba haitatoboa kokote. Ukweli lazima uwekwe wazi.
kwani biashara ni nini, si ni kununua na kuuza? tambua kuna maisha baada ya SimbaMimi sina shida sana na kuuzwa kwa Miqueson....
Ila kumuuza CHAMA ilikuwa ni kosa kubwa ....
Jamaa alikuwa anaituliza timu...unaona kabisa anachotumia ndani ya 18 wakati stickers wengine wanajipanga haraka...