Biashara ya Mpunga Dodoma

Biashara ya Mpunga Dodoma

MONA WA KYEN

JF-Expert Member
Joined
Dec 23, 2016
Posts
340
Reaction score
271
Wakuu habari napenda kuuliza anaefahamu kuhusu biashara ya kukoboa na kuuza mpunga maeneo ya Dodoma mjini na hata pembezoni mwa jiji.

Ningependa kufahamu
1. Upatikanaji wa mpunga kwa bei rahisi na mzuri huwa hasa maeneo gani?
2. usafirishaji wake ukoje na garama yake ina range kiasi gani?
3. Gharama za kukoboa zikoje?
4. Eneo lenye biashara inayozunguka sana kwa mchele ni lipi? ndani ya jiji au nje ya jiji?

Mengineyo naomba aniongezee kama yapo, asaneni natanguliza shukrani.
 
Dodoma tunakula mchele unaotoka Bahi, Morogoro na Mbeya.
 
Biashara ni nzuri ukizingatia idadi kubwa ya watu mjini Dodoma.
Mpunga upo kwa wingi wilayani Bahi (50km toka Dom) na Kondoa.
Usafiri upo 24/7 (malori tupu toka mikoa/nchi jirani)
Gharama ya kukoboa ni ya kawaida kutegemea na gunia ulizonazo
 
Asante sana mkuu vipi mpunga gunia unakuwaga na kilo ngapi na huwa unatoa mchele kilo ngapi?
na gharama ya usafiri huwa sh ngapi?
 
asante sana mkuu vipi mpunga gunia unakuwaga na kilo ngapi na huwa unatoa mchele kilo ngapi?
na gharama ya usafiri huwa sh ngapi?
Gunia la mpunga linakuwa na kilo 90 hadi 100 kulingana mpimaji wakati wa kujaza na likikobolewa linatoa kilo 60+ za mchele.
Usafiri ni maelewano kati yako na dreva wa lori lakini kwa ujumla madreva wana njaa na wanataka pesa yoyote kuliko kurudisha gari tupu toka Kigali hadi Dar kwa mfano. Hivyo wakipata mzigo njiani huwa hawapotezi furusa na mnaweza kubaliana buku 2.5, 3.0 au 5 kwa gunia toka Bahi-Dodoma. Pia mnaweza kubaliana jumla tu mzigo unatembea na hii inafanya kazi kwa semi-trailers na unapokuwa na mzigo wa kilo 500+ za mchele.
 
Mkuu biashara ya kununua mpunga na kuukoboa ni biashara inayohitaji uzoefu sana.lazma ujue upate mtu anaejua mpunga wa kutoa mchele mzuri maana unaweza ukanunua mpunga kwa bei kubwa halafu ukatoa chenga za vitumbua ..Nkushauri kama hauna uzoefu wa hilo zao bas mtafute mtu awe anakunnulia kwa ...Bahi na morogoro ni kalibu
 
shukrani mkuu wa ushauri
 
Back
Top Bottom