jokotinda_Jr
JF-Expert Member
- Apr 9, 2022
- 882
- 1,536
Hii mbinu kuna mwamba alinifundisha mwaka 2018 kule mbingu morogoroNgoja tupeane uzoefu kidogo.
2015 - 2017 niliwahi kujihusisha na kilimo cha Mpunga huko Mkoani Morogoro, Wilaya ya Mlimba, Kijiji cha Ngalimila na kupata kuishuhudia biashara hii pasipo kusikia.
Mahitaji
1. Viroba
2. Ndoo za kupimia mpunga
3. Mahali pa kuhifadhia mpunga (godown)
4. Vibarua wa kukununulia mpunga wenye utaalam wa kutosha kuweza kung’amua mpunga mzuri.
5. Mahali pa kuhifadhia mpunga (sehemu unayokusanyia mpunga)
6. Usafiri kusafirisha mpunga kupeleka godown
7. Vituo vya kukusanyia mpunga. Lazima uwe na kituo zaidi ya kimoja kuongeza nafasi ya kukusanya mzigo kwa wakati na kupunguza ushindani kwa wenzako wanaofanya biashara hiyo.
8. Fedha za kuwalipa wanunuzi kwa kila kituo ulichoweka.
Changamoto
1. Kupata mtu muaminifu wa kusimamia upatikanaji wa vijana wa kufanya kazi hiyo kwa idadi ya vituo utakavyoweka kukusanya mpunga.
2. Uaminifu wa wanaokununulia mpunga kukataa mpunga usio mzuri (Mind u that utawalipa kwa idadi ya gunia wanazokusanya so mwingine anaweza asiwe muaminifu ili apate malipo mazuri)
Ushauri
Vema kwenda mashine kusubiri wakulima wanaokuja kukoboa mpunga wao na kupatana nao bei na kukuuzia mchele, still bei yao ipo chini na gharama zitatofautiana kidogo sana na za wewe kwenda huko vijijini kukusanya mpunga.
Huko vijijini unaweza kusumbuka zaidi na mchakato mzima na mwisho wa siku ukapigwa na kitu kizito kichwani ukajikuta umenunua mpunga halafu ukikoboa unakutana na chenga kumbe mpunga ulikauka sana shambani.