Biashara ya mtaji wa milioni 2

Wakuu samahani nimekwama hapa, nawaza ni biashara gani naweza fanya ya mtaji wa milioni 2 nikapata faida pamoja na rejesho la kila wiki shilingi elfu 90, kwa mwenye wazo anisaidie tafadhali
Njoo Kariakoo tafuta meza. Meza zinatofautiana bei kutokana na mitaa, zinaanzia moja mfano mitaa ya aggrey na sikukuu, 150k, 200k mpaka 300k kwa mwezi mitaa ya Congo.

Kuhusu kulipa inategemea na muhusika na swaga zako na miezi, unaweza anza lipa miezi3, minne mpaka 6.

Tukija kwenye biashara kuna vijora😂😂hii kitu watu wanadharau ila ni hatari, sababu nashinda huku naona.

Kuna vitu vya urembo kama hereni, cheni n.k
Kuna kuuza visendo vya watoto wa kike.
Kuna kuuza mitumba.

Kwangu hizo ni biashara nzuri na unaweza rudisha pesa

NB(Biashara inahitaji akili na uchangamfu in tx Dullah voice)

Karibu mkuu tupambane
 
Hivi mtu unaweza kuagiza vitu china ukawa unauza kwenye meza mfano madodoki ya kuogea au ni lazima biashara ziwe zinafanana na chinga wengine
 
Hivi mtu unaweza kuagiza vitu china ukawa unauza kwenye meza mfano madodoki ya kuogea au ni lazima biashara ziwe zinafanana na chinga wengine
First thing first.
Fanya tathmini nzima ya kuona cost zote za kuagiza mpaka mzigo ufike.
Kariakoo wapo big fish(supplier) kama unaweza kuona cost zinafanana its better ukachukulia hapo hapo.

Si lazima biashara zifanane ila in nature Kariakoo palivyo biashara zipo sehemu zinazofanana ili iwe rahisi kwa watu kufika, kuna mitaa ya maduka ya simu, mapazia na mashuka, vyombo na vitu vya umeme, nguo n.k

Ni unaangalia tu biashara uliyopoint ipo wapi kwa ukubwa sababu wateja watafika hapo kwa wingi wakifahamu mitaa fulani kuna bidhaa fulani.
 

Kuna vitu ma big fish hawaleti mpaka waone mtu umeleta kime trend ndo wanaleta. Natamani sana kufanya biashara Kariakoo, hivi chinga nao wanalogana?
 
kuna vitu ma big fish hawaleti mpaka waone mtu umeleta kime trend ndo wanaleta. natamani sana kufanya biashara kariakoo ,hivi chinga nao wanalogana ?

Mkuu mimi siamini kuhusu hivyo vitu, kipindi naanza niliambiwa hivyo vitu, napiga kazi.

Unauza kwa sababu kuna ni sehemu yenye movement kubwa
Kariakoo hakuna kitu ambacho hakuna japo inategemea na ukubwa wa bidhaa hiyo kama ina demand au laaah.

Njoo upige kazi mkuu hizo kulogana ni stori za vijiweni.

Hujaona Kariakoo mtu akikosa bidhaa anamwambia cheki duka linalofata au wanauziana?
 
Asante, ngoja nikuze mtaji nitakutafuta kama utakuwa bado ni active member.
 
Mpe mchongo sasa mwenzako, kutuelezea unavyo tengeneza hizo pesa sio suluhisho.
Inawezekana Kupata Zaid ya Hiyo Elfu 90 kwa Wiki , Mim nimewekeza Milion 4 Napata Mpaka Laki tatu kwa Wiki , Na Kila Siku sikosi 50 mpaka 70[emoji849]
 

Umetisha
 
Wakuu nimeona baadhi ya watu wamenitext PM nashindwa kureply PM yangu inaandika connecting na shida hii watu wengi wamelalamika lakini naona viongozi wapo kimya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…