Biashara ya nafaka Dar ipoje?

Kwanza umeipataje hiyo pesa , kama Kuna biashara unafanya ndio iliyokuingizia hiyo pesa nakusihi endelea na hiyo hiyo biashara Kwa kuongeza WiGo zaidi wa biashara Yako.
Maana biashara mpya Huwa Sana na itakuchukua muda kidogo kuzimaster .
Shida biashara niliyokuwa nafanya ipo kijijin Sana hainipi changamoto na mzunguko mdogo pia ndo maana nataka kuja dar
 
Nilitaka kuongea ila nikaona wacha niendelee kusoma na kweli bana nikakuta koment yako aiseeee!! Nimecheka mpk kichwa kinauma 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Arooo 🤣🤣
 
Bro mi nipo mtwara
Sasa kaka upo mtwara kwani hamulimi ufuta huko?mtwara na lindi ndio mikoa yenye fursa nyingi sana za biashara kwani ndio mikoa inayokuwa na misimu mitatu ya mazao ya biashara,kuna msimu wa ufuta ambao unaanza mwezi wa tano,kuna msimu wa korosho ambao unaanza mwezi wa tisa na kuna msimu wa mbaazi hayo yote ni mazao ya biashara na watu tumetoboa kupitia mazao hayo nakushauri kama upo mtara au lindi usitoke kuja dar kwa kipindi hiki utarudi nyuma komaa kwanza hukohuko angalau uwe na kuanzaia million 15 au 20 ndio uje kupambana na biashara Dar hapo utakuwa umesimama tayari.Asante
 
Biashara za mazao nazan huzifaaham kk ivi wew unaijua korosh vizur Yan bei kununua unajipangia wee afu anaekuja kununua hujui anakuja kununua bei gan hili zao linawafaa wakulima tu sio wafanyabiashra na Kama mfanyabiashara ukinununua inabid uvumilie miez na miez ili uje kuuza kwa bei ya faida ufuta hiyo bei ya 3000 mpk 4000 sio kila mwakaa unawza ingia ukajichangany hela yako haiwez Rudi Tena wakulima wamekalili tiar bei huwez wew asaiv kumuamuru mkulima akuuzie wew ufuta kilo buku au buku jero hizi biashara za mazao acha tu. Mwaka Jana nimenunua karanga za million tatu mpka Leo zipo tu ndani toka mwaka Jana mwez wa nne. Wateja hakuna kwaiyo bro hizo biashara ulizotaja nazijua. Vizur
 
umeongea point sana sasa kama mtu anataka kuja uko mkoa gani wewe ili tuje
 
Shukrani Sana but nilikuwa naomba muongozo wa biashara ya NAFAKA hio
Tafuta frame karibu na soko, then nenda kwa wauzaji waambie wakuuzie mzigo kwa bei ya juml.

Mi kuna mzee pale tabata shule alikuwa anauza 2800 p/kg. Lakini kwa jumla alikubali kuniuzia kwa 2650 p/kg.

Nafaka zina faida nzuri sana na haziharibiki hovyo. Ukifanikiwa kuuza 100kg kwa faida ya 150 una 15,000 tayari. Kwa product moja. Bado maharage nk
 
Gunia moja unaweza kuuza kwa muda gani na bei za frame sehem hiyo ya soko ilyochangamka inaweza kuwa bei gan kwa mwez
 
Gunia moja unaweza kuuza kwa muda gani na bei za frame sehem hiyo ya soko ilyochangamka inaweza kuwa bei gan kwa mwez
Inategemea upo mkoa gani. Kwa dar, sehemu za masokoni frame zimechangamka kwa sababu biashara inakuwa ya uhakika.

Masoko kama ya tandika,mbezi,kawe na tegeta, inatakiwa uwe unatoa mzigo mkoa mwenyewe. Coz kuna giants huko mzigo wanatoa mkoani kwa bei imenyooka kdg.

So inabidi utege kwenye soko ndogondogo kama segerea, vingunguti ndanindani, kimara nk.

Biashara ikiwa nzuri, kwa kulangua unaweza uza zaidi ya gunia kwa siku, coz itabia uwe na mchele wa aina zaidi ya 3 na ukauza kila aina zaidi ya 30+ kg.

Kama unatoa mikoani mwenyewe, inategemea kama utauza kwa jumla au rejareja, jumla utauza hata wote ulionao kwa siku moja. Rejareja utauza ata gunia 5 coz utacompete na giants kwenye mzunguko mkubwa kibiashara
 
Acha kumdanganya kijana wa watu.
Mueleze changamoto zake pia.
 
Wewe acha kumpoteza huyo kijana hiyo biashara unayomuambia ni kweli Ina faida ila inatakiwa awe na mwenyeji huko wa kumsaidia. Tofauti na hilo atapoteza pesa zote maana asili ya hiyo biashara lazima atafute vijana wakwenda kutafuta mzigo madhambani huko na hapo ndio shida inapoanzia maana uaminifu ni mdogo.

Vijana wa kusini unawajua kitendo Cha kuweka heshima bar Kwa pesa za watu wengine ni sekunde tu.

Cha pili msimu wa ufuta Bado na hakuna anaejua kama bei itakuwa hiyo uliyoisema.
 
Bro nimekuchek pm usisite kunitafutia I need more explanation
 
Hivi nafak zipi no Bora kuanza nazo kwa huo mtaji nichanganye Aina zote kwa udogoudogo? Au kuchagua nafaka moja au mbili za kuanza nazo Kama ni mchele na maharage Basi nguvu yako yote unaelekeza huko
 
Hiyo hela usiichome yote kwenye biashara, anza na nusu kwanza upime upepo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…