Inategemea upo mkoa gani. Kwa dar, sehemu za masokoni frame zimechangamka kwa sababu biashara inakuwa ya uhakika.
Masoko kama ya tandika,mbezi,kawe na tegeta, inatakiwa uwe unatoa mzigo mkoa mwenyewe. Coz kuna giants huko mzigo wanatoa mkoani kwa bei imenyooka kdg.
So inabidi utege kwenye soko ndogondogo kama segerea, vingunguti ndanindani, kimara nk.
Biashara ikiwa nzuri, kwa kulangua unaweza uza zaidi ya gunia kwa siku, coz itabia uwe na mchele wa aina zaidi ya 3 na ukauza kila aina zaidi ya 30+ kg.
Kama unatoa mikoani mwenyewe, inategemea kama utauza kwa jumla au rejareja, jumla utauza hata wote ulionao kwa siku moja. Rejareja utauza ata gunia 5 coz utacompete na giants kwenye mzunguko mkubwa kibiashara