Biashara ya nafaka Dar ipoje?

Biashara ya nafaka Dar ipoje?

Fursa zipo kwenye kilimo ila uvumilivu ndio unahitajika.
Uko kwenye ufuta kukoje...uje Kuna mtu uku kanigusia ila kawa mchoyo wa taarifa kasema uko Hela inazaa Hela...alishakuwepo uko mwaka Jana akapata..nasasa hivi anataka auze kunia zake mia200 za mpunga awahi uko lindi mwezi wa5 anasema msimu ndo unaanza wamavuno kwaiyo anawahi kabla walanguzi matajiri Toka dar,mbeya,arusha hawajakuja kupandilia Bei
 
Njoo kilwa ununue ufuta kuanzia mwezi wa tano mkuu hautojuta tena anza na mtaji wowote ule kuanzia laki sita kama unajitafuta au mtaji upo anza hata na million mbili,tatu,tano,kumi yani ww tu na mtaji wako.
Mkuu nimeamini usemacho kuhusu ufuta..hapa Kuna mtu nafamiana nae kasema hivo hivo kama unavosema ila kawa mchoyo wa taarifa anadai anaenda lindi mwezi wa Tano ndo mwanzo mwa msimu Bei huwa chini kabla ya walanguzi hawajavamia
 
Kijana mdogo wa miaka 21 kawazidi mbali sana vijana wetu hawa wanakulia mashuleni mavyuoni huko wanahitimu na wanatoka bila kitu wanakaa nyumbani kusubiri ajira pambana Sana kijana
Ukute hata wewe huwa unaisikia kwenye matangazo ya biashara tu!!. Kusoma na kupata pesa ni vitu viwili tofauti.
 
Mahindi achana nayo, saizi Dar bei ni 550 mpk 500 kwa kilo. Hata uende viwandani au masokoni. Hamia kwenye Ufuta,mchele na maharage
 
Mimi sio dalali ila ninachokuambia ni ukweli kama kwasasa watu wanakopesha kula maua kwa bei ya 1000 kwa kilo labda wewe ndie unachanganya mambo,mkulima hawezi kukuuzia wewe ufuta ulio tayari kwa bei ya 1000 wakati tayari ameshajua bei ya mnada kuwa ni 3500
FUngua pm mkuu
 
Mkuu, wewe juzi juzi si ulikuwa unauliza ni wapi wanachukua walinzi ili na wewe upeleke form ya kuomba kazi ya ulinzi?

Hii biashara ya ufuta umeianza lini?, kama ina faida kwa nini utake kuomba kazi ya ulinzi?. Angalia usimuingize choo cha kike mdogo wetu.

Oya mdogo wangu, hapo juu kuna watu wamekupa ushauri mzuri sana. Hiyo hela yako kwa sasa tafuta sehemu uitunze kwanza, usiingize kwenye biashara yoyote ile. Tafuta mtu ambaye anafanya biashara ya nafaka, muombe awe mentor wako(Omba hata kujitolea kumsaidia kazi zake) mpaka pale ambapo utaielewa hiyo biashara vizuri. Siku ukitaka kuanza kufanya biashara rasmi, chukua robo ya hela yako (2M) anza kununua mzigo kidogo kidogo. Ukishaanza kupata wateja wa kutosha ongeza robo ya hela (Hapo utakuwa umeingiza nusu ya hela yako kwenye biashara). Nusu ya hela inayobaki itunze kama back-up capital.
Wazo zuri sana mkuu
 
Kama ndio unaanza kujitafuta ww njoo uanze hata na laki sita tu bei inaanza buku kwa kilo unapata gunia sita hapo na ikifika buku jero unapata gunia nne hapo na bei ghalani yani kwenye vyama vya ushirika inaanza 3000+ ila itahitaji upate mwenyewe tu ili uweze kupata mzigo kwa haraka au kama una mtaji wa kutosha anza na milioni mbili tu kwa kuwa ndio unaanza ili upate uzoefu na mwenyeji muaminifu hata ukija tena msimu mwingine unakuwa sio mgeni tena.
Mkuu upo kimya sana humu au ndio uko shamba. Naomba mawasiliano yako DM kuna vitu nataka nikuulize kwa kirefu. Nakuomba sana
 
Mkuu, wewe juzi juzi si ulikuwa unauliza ni wapi wanachukua walinzi ili na wewe upeleke form ya kuomba kazi ya ulinzi?

Hii biashara ya ufuta umeianza lini?, kama ina faida kwa nini utake kuomba kazi ya ulinzi?. Angalia usimuingize choo cha kike mdogo wetu.

Oya mdogo wangu, hapo juu kuna watu wamekupa ushauri mzuri sana. Hiyo hela yako kwa sasa tafuta sehemu uitunze kwanza, usiingize kwenye biashara yoyote ile. Tafuta mtu ambaye anafanya biashara ya nafaka, muombe awe mentor wako(Omba hata kujitolea kumsaidia kazi zake) mpaka pale ambapo utaielewa hiyo biashara vizuri. Siku ukitaka kuanza kufanya biashara rasmi, chukua robo ya hela yako (2M) anza kununua mzigo kidogo kidogo. Ukishaanza kupata wateja wa kutosha ongeza robo ya hela (Hapo utakuwa umeingiza nusu ya hela yako kwenye biashara). Nusu ya hela inayobaki itunze kama back-up capital.
Nakazia hpa zingatia huu ushauri
 
Back
Top Bottom