Nikifa MkeWangu Asiolewe
JF-Expert Member
- Feb 26, 2024
- 12,463
- 27,556
Wakuu habari za uzima wenu nyonte.
Si Kwa ubaya Kwa wale wote hasa wafanyabiashara ya nafaka (maharage) mchongo upo morogoro wilaya ya Gairo Kijiji cha Rubeho umbali kama wa dk20 kutoka Gairo mjini.
Nilifika mwenyewe kule katika harakati za hapa na pale nikakutana na mnada hivyo nikaanza kuuliza wenyeji
Bei ya maharage kule hawapimi Kwa kg wanapima Kwa Lita Kuna makopo Fulani Hivi yenye ujazo wa lita1
Maharage ya njano debe la Lita 20 wanauza 37,000-40,000/=
Kopo la Lita1 maharage ya njano wanauza 2000/=
Maharage mengine bei ni 1500/
Kwa kopo la Lita Moja.
Huku kahama niliko Mimi maharage bei ni 3000-3400/= Kwa kg1 yale ya njano.
Hayo mengine huku hayana soko sana kama ya njano bei ni 2500/= Kwa kg1
Hii ni bei ya jmos 29/09/2025 lakini walidai yamepanda hivyo bei inaweza kufika Hadi 45k Kwa debe lita20!
Wakasema Kuna muda huuzwa Hadi 25,000/= debe 1 la maharage ya njano!
Bei hupungua kulingana na mzigo unachukua niliwaambia nikihitaji Tani 5 naweza kupata Kwa kg1 hata Tani hawajui wengi wanao uza ni wakina mama ndhani karibia 99.99%
Nikiwa na maana ya kwamba sikuonana na mwanaume hata mmoja anauza maharage pale.
Mzigo upo wa kutosha sana hata fuso Lina jaa ukiyakusanya yote.
Nilipiga picha za hivyohivyo maana. Simu nimeharibu sijatengeneza bado.
Hivyo wewe mpambanaji unaweza kufika hapo nauli Kwa boda ni Tsh 10,000/= kwenda na kurudi kama anakusubiri Hadi umalize mambo Yako mtaelewana kulingana na muda mtakao subiriana huko.
Kwa walio seriously tu nina namba za mwenyeji ambaye ni boda boda anajua Kila kitu kuhusu mnada huo hivyo anaweza kukupokea muda wowote na kukupeleka mnadani!
Kwa upande wa mifugo kama mbuzi bei si rafiki sana asee.
Upande wa mahindi debe ni sh12,000/=
Vitu vingine sikuuliza maana sio hobby yangu.
Ni hayo tu