Ugumu wa maisha unaoambatana na ukosekanaji wa ajira kwa mabinti, kukosa mawazo sanifu ya kibiashara pamoja na mitaji, na ugumu wa maisha unaoambatana na kupanda kwa bei za kimaisha ni miongoni mwa mambo yanayowapelekea wanawake wengi kujihusisha na biashara ya ngono ikidhaniwa kuwa ni moja ya njia rahisi ya kujipatia kipato kinachoweza kukidhi mahitaji yao.
Binafsi, nadhani kampeni zinazofanywa na viongozi jijini Dar kwa lengo la kukomesha biashara hizi kwa kuwakamata na kuharibu maeneo yao ya kazi, haiwezi kuwa tiba ya moja kwa moja. Bali ni kuhakikisha utafiti wa kudumu unafanyika juu ya namna gani wanawake hawa wanaweza kusaidiwa.
Kwanza ni kwa kuanza na tiba ya saikolojia itakayowajengea kujiamini kama wanajamii wengine na kuwatengenezea misingi ya fursa kwa kutoa mikopo itakayoambatana na masharti elekezi.