Ndugu zangu! nafikiria kuanza biashara ya kuuza ngozi ya mamba nchi za nje! Mimi ni mwenyeji wa kutoka wilaya ya Ludewa ziwa nyasa. Mwezi wa kumi na mbilli nilikwenda likizo ziwani na kushuhudia vifo vya watu zaidi ya watatu wakiliwa na mamba hapo kwetu.
Nilifanya utafiti mdogo na kuona kuwa idadi ya mamba imeongezeka sana kiasi cha kuwaona kama samaki maana ni wengi mno, wala sio wa kutafuta. Likaniijia wazo hili la kufanya biashara ya ngozi ya mamba, je kuna mwenye kujua kuhusu soko huko nje na bei zake ili niweze kuchangia kuwapunguza hawa jamaa (mamba)
Nakaribisha maoni