Biashara ya nguo za kike au kiume kariakoo

shibi

Member
Joined
Dec 8, 2016
Posts
10
Reaction score
2
Habari zenu wakuu, kama title ilivyo hapo juu nimejichanga ili nifungue duka/goli la nguo kariakoo. Mtaji wangu ni 15m (huenda kwa kkoo ni ndogo lakini nimeona niende hukohuko angalau kwa siku watapita wateja wawili watatu kuliko kuanzia huku mtaani ambako naona biashara ni ngumu sana) changamoto nimeshindwa kuamua nijikite nguo za kiume au za kike?

Naomba wenye uzoefu na mitaa hiyo mnishauri kutokana na soko ni zipi zinatoka zaidi maana hali ni tete nisingependa kupoteza hata hiki kidogo nilichonacho.

Pia kuna mdau amenishauri kuliko nguo ni bora nifungue hardware ya vifaa vya umeme....kwa ufupi ndugu zangu sielewi nichague kipi kati ya hivi. Ushauri wenu muhimu sana ndugu zangu.
Nawasilisha.
 
Hardware nipesa ndogo sana..labda hiyo ukanunue mchele kyela au ufungua biashara ya chupi zakike boxer blazia taiti za kike singlendi i
 
Mkuu ukianzisha goli la nguo mikoani hasa Dodoma na vikiwemo na hivyo vyupi kwa mtaji wako baad ya mwaka mmoja uko kwingine kabisaaaa.
 
Kariakoo wenzako naona wanapakimbia kutokana na kuwepo kwa rundo la wamachinga ambao hawachagui pa kusimama au pakukaa..
 
Mkuu ukianzisha goli la nguo mikoani hasa Dodoma na vikiwemo na hivyo vyupi kwa mtaji wako baad ya mwaka mmoja uko kwingine kabisaaaa.
Asante kwa ushauri, tatizo makazi ni Dar na biashara kama hiyo siwezi kutumana
 
Kariakoo kwa sasa kuna changamoto ya TRA wanakaba mpaka penati na wamachinga nao ndio pasua kichwa Dera /Kijora unachouza ww dukani 10-15k yeye anauza 7-8k kwa akina dada wengi wananunua vitu kwa Machinga

Ushauri wangu nenda kafanye Research ya kutosha pale Kkoo nadhani uta gain kitu usijiridhishe na maoni ya hapa JF peke yake

Kila la heri mkuu
 
Mpendwa kwanini usinunue tu belo lako la mitumba
Kama belo la jeans kali za kike bei ni 600,000 hvi ndani unakuta nguo mpka 250
 
Ushauri wangu...kkoo saa hivi utachemsha
(Kkoo kwa sasa sikushauri kabisa)...

Kama unatapenda nisikiza, ni hivi nunua passo used 5m - 6m ifanye uber endesha we mwenyewe.....(piga kazi kuwa na discipline na hela. Save hela kwa nidhamu sana kama ni bata kula kwa mahesabu makali sana)

Hyo hela nyingine iweke sikilizia upepo kwanza, uje hapa tena kabla ya kukurupuka....

Hyo gari hata baadae useme unaiuza hukosi mteja (na huku hela za uber ushaokota sanaa). Zingatia matunzo.

Kuna mambo mengi sana unaweza fanya ukiwa na gari (unaweza ukawa dalali real estate etc na hyo gari inakusaidia mobility na mteja ambae lazima alipie service ya kuzunguka nae)

Baada ya hapo mdogo mdogo fikiri kuwekeza kwenye Car Wash Business.


Utanikumbuka. Narudia tena “ Utanikumbuka “
 
Mpendwa kwanini usinunue tu belo lako la mitumba
Kama belo la jeans kali za kike bei ni 600,000 hvi ndani unakuta nguo mpka 250
Mdoa mada anataka kufanya biashara ya nguo sasa wewe unamshauri afanya betting, eti nunua balo la mtumba!
 
mku biashara ya nguo inalipa Sana hasa za kike ndo wahitaji wakubwa Sana,pambana,Ila jitahid uchukue nguo Bora Zaid ,namin utakuja na ushuhuda jf
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…