Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu, soma vizuri maana ya fetish halafu relate na biashara inayozungumzwa hapa.Kawa wewe ni mwanaume unapenda kuuza /kuona vitu kama sidiria au chupi za kina dada ina weza kuwa ni kaugonjwa fulani [ FETISH]
Ngariba asante sana kwa hii post nilichukua nondo zako zote ndo zinaniongoza hadi mda huu, japo nmeanza na mtaji kidogo ila mambo si haba aliye juu anajalia japo kidogo napata aiceee.. Mzigo nmechukulia mwanzaPamoja mkuu.
Safi mkuu , umetema nondo zoteNgoja nieleze kwa uzoefu wangu mdogo kuhusu hii biashara.
Aina za chupi
Chupi zipo za ubora tofauti kulingana na material. Kuanzia za dzn Tsh 8,000 hadi Tsh 45,000 na kuendelea.
Kundi la dzn 8,000 hadi 14,000 tunaliita lonya, ni zile nyepesi (za watu wa kipato cha chini), 15,000 hadi 32,000 ni ubora wa kati (za wa kipato cha kati) na 34,000 na kuendelea ni high quality (hizi za wa kipato cha juu).
Jua aina ya wateja wako ujue kundi gani la ubora ulangue zaidi. Si mbaya kuchanganya ila isiwe nusu lonya na nusu high quality. Kama wateja uliowalenga ni wa kipato cha chini basi jaza lonya na quality chache, na kinyume chake ni kweli (vice versa is true).
View attachment 1320903
Mtaji kiasi gani?
Inategemea na quality ya chupi uliyoamua kuuza. Mil 2 hadi 3 inaweza kukupa dzn 150 hadi dzn 200 za lonya, huku fedha hiyo hiyo ikakupa dzn 50 hadi 60 ya zile quality. Mtaji unaamuliwa na aina ya mzigo kulingana na wateja wako.
Size na aina ya wateja.
Kulingana na mahali unapoenda kuuza ila kumbuka wanunua chupi zaidi ni wadada wa rika la kati, umri miaka 20 hadi 35. Wengi hawana majukumu mengi ya kimaisha, wanajipenda na wako kwenye mahusiano ya mapenzi motomoto. So, size za kundi hili ndizo ziwe nyingi.
Wapi utapata mzigo wa jumla?
1. Dsm, Kariakoo mtaa wa Msimbazi na muhonda zipo lonya nyingi sana.
2. Dsm, Kariakoo mtaa wa mchikichini na Manyema (kama sijakosea majina) jirani na ukumbi wa ddc. Hapo kuna quality nyingi. Pia yapo maduka machache kule Congo, mtaa wa Mchikichi na Nyamwezi, n.k
View attachment 1316585
3. Mwanza pembeni ya njia panda ya barabara ya Pamba na Miti mirefu. Upande wa stand ya zamani ya Tanganyika. Maduka yako bondeni kidogo (yamejificha).
4. Kampala, Uganda kuanzia makutano ya William street na Ben Kiwanuka Rd, na ukiteremka na hiyo Ben Kiwanuka hadi unakaribia njia panda ya stend ya zamani ya daladala (Kampala Old Tax park). Kabla ya hiyo njia panda kuna maduka yako ndani ndani.
Kumbuka; maduka mengi ya barabarani hapo William street na Kikuubo Rd (tamka Chikuubo) yenye wauzaji wengi ni ya rejareja, maduka ya jumla yako ndani. Kampala duka 1 wanaweza changia watu hata 6, kila mtu anauza upande wake. So, ukiona duka la nje limejaa na lina wauzaji wengi basi kuwa makini, wakijua ni mgeni nao wanajifanya wanauza jumla, then unapunguziwa kidogo kwenye bei yao ya rejareja so unakuwa umepigwa.
Zingatia;
- Dsm unapata mzigo wa aina zote kwa bei nzuri
- Mwanza mzigo mwingi ni ile quality ya kati na unatoka Kampala na Nairobi. Nairobi zinatoka Skin tight na brazia nzuri na baadhi hazipo Dar. Bei za Mwanza ni juu kidogo kuliko Dar japo baadhi ya tight na brazia Mwanza ni nafuu na nzuri kuliko za Dar.
- Kampala chupi nyingi ni quality ya kati (si lonya wala high quality) na nafuu. Tatizo hawana brazia nzuri na tight nzuri.
Muuzaji
Kwa uzoefu wangu, wateja wengi hasa wadada (ambao ndio kundi kubwa) wanapenda wauzaji wa kiume hasa akiwa mchangamfu na mwenye kauli nzuri. Muuzaji asipitilize na kuleta utani na mitongozo.- Mabinti wadogo wana aibu, wanapenda wauzaji wa kike, uzuri wao si wanunuzi sana. Bado wanafunzi.
- Wamama watu wazima sana hawapendelei wauzaji wa kiume ila endapo muuzaji akimpokea na kumsemesha kwa heshima, ananunua.
- Wanaume wanapenda wauzaji jinsi zote tu. Akimkuta muuzaji wa kike atatamani ajue yeye anapenda ipi, akikuta wa kiume anatamani ampe uzoefu wanawake wengi wanachagua zipi. Hili nalo ni kundi dogo.
Ni chupi tu?
Hapana, lazima uuze na skin tight, brazia, lesso, sox, night dress,vest, boxer n.k
Changamoto
- Mzigo kupitwa na fashion. Usirudie mzigo mara nyingi hata kama ulipendwa. Mara zote uwe na vitu vipya.
- Wauzaji wa kiume kuingia kwenye mapenzi na wateja.
- Biashara kuwa kijiwe cha story hadi kuziba wateja. Wadada wanaongea sana hasa ukiwachangamkia na wakikuzoea.
- Mteja kutaka kurudisha / kubadirisha nguo ya ndani baada ya kufika nayo nyumbani. Usikubali. Bora anune umpoteze coz hata ukimkubalia utampoteza pia coz atajua ndio mchezo wako.
Kumbuka kutoa zawadi kwa wale wateja wa siku zote na kwa wale wanaonunua mzigo mkubwa. Mf. Kanunua chupi 8 @ Tsh 3000 - Tsh 4000. Mpe hata lesso ya 500. Haitokufilisi ila atafurahi sana.
Sawa kaka ntaludi tena aice maana nimesaga sana sori kutafta ajira almost miaka mi 5 nashukuru niliukumbuka huu mchango wako humu nikabidi niusake nikaufanyia kazi kwa mda huu nipo huku visiwani nakomaaKaribu mkuu. Nafurahi kusikia kuwa ulichukua hatua ukaanza na sasa unasonga na umerudi kutoa mrejesho.
Ukiwa na jambo karibu tushauriane.
Watu kama hawa ndoo wanatakiwa kuwepo dunianiSafi mkuu , umetema nondo zote
Hongera sanaNgariba asante sana kwa hii post nilichukua nondo zako zote ndo zinaniongoza hadi mda huu, japo nmeanza na mtaji kidogo ila mambo si haba aliye juu anajalia japo kidogo napata aiceee.. Mzigo nmechukulia mwanza
Upo vizuriNgoja nieleze kwa uzoefu wangu mdogo kuhusu hii biashara.
Aina za chupi
Chupi zipo za ubora tofauti kulingana na material. Kuanzia za dzn Tsh 8,000 hadi Tsh 45,000 na kuendelea.
1. Kundi la kila dzn Tsh. 8,000 hadi 14,000 tunaliita lonya, ni zile nyepesi (za watu wa kipato cha chini).
2. Kundi la kila dzn Tsh 15,000 hadi 32,000 ni ubora wa kati (za wa kipato cha kati).
3. Kundi la kila dzn Tsh 34,000 na kuendelea ni high quality (hizi za wa kipato cha juu).
Jua aina ya wateja wako ujue kundi gani la ubora ulangue zaidi. Si mbaya kuchanganya ila isiwe nusu lonya na nusu high quality. Kama wateja uliowalenga ni wa kipato cha chini basi jaza lonya na quality chache, na kinyume chake ni kweli (vice versa is true).
View attachment 1320903
Mtaji kiasi gani?
Inategemea na quality ya chupi uliyoamua kuuza. Mil 2 hadi 3 inaweza kukupa dzn 150 hadi dzn 200 za lonya, huku fedha hiyo hiyo ikakupa dzn 50 hadi 60 ya zile quality. Mtaji unaamuliwa na aina ya mzigo kulingana na wateja wako uliowalenga.
Size na aina ya wateja.
Kulingana na mahali unapoenda kuuza ila kumbuka wanunua chupi zaidi ni wadada wa rika la kati, umri miaka 20 hadi 35. Wengi hawana majukumu mengi ya kimaisha, wanajipenda na wako kwenye mahusiano ya mapenzi motomoto (wanatamani chupi nzuri na nyingi ili kuwavutia wenza wao). So, size za kundi hili ndizo ziwe nyingi.
Wapi utapata mzigo wa jumla?
1. Dsm, Kariakoo mtaa wa Msimbazi na muhonda zipo lonya nyingi sana.
2. Dsm, Kariakoo mtaa wa mchikichini na Manyema (kama sijakosea majina) jirani na ukumbi wa DDC. Hapo kuna quality nyingi. Pia yapo maduka machache kule mtaa wa Congo, mtaa wa Mchikichi na Nyamwezi, n.k
View attachment 1316585
3. Mwanza pembeni ya njia panda ya barabara ya Pamba na Miti mirefu. Upande wa stand ya zamani ya Tanganyika. Maduka yako bondeni kidogo (yamejificha).
4. Kampala, Uganda kuanzia makutano ya William street na Ben Kiwanuka Rd, na ukiteremka na hiyo Ben Kiwanuka hadi unakaribia njia panda ya stend ya zamani ya daladala (Kampala Old Tax park). Kabla ya hiyo njia panda kuna maduka yako ndani ndani.
Kumbuka; maduka mengi ya barabarani hapo William street na Kikuubo Rd (tamka Chikuubo) yenye wauzaji wengi ni ya rejareja, maduka ya jumla yako ndani. Kampala duka 1 wanaweza changia watu hata 6, kila mtu anauza upande wake. So, ukiona duka la nje limejaa na lina wauzaji wengi basi kuwa makini, wakijua ni mgeni nao wanajifanya wanauza jumla, then unapunguziwa kidogo kwenye bei yao ya rejareja so unakuwa umepigwa.
Zingatia;
- Dsm unapata mzigo wa aina zote kwa bei nzuri
- Mwanza mzigo mwingi ni ile quality ya kati na unatoka Kampala na Nairobi. Nairobi zinatoka Skin tight na brazia nzuri na baadhi hazipo Dar. Bei za Mwanza ni juu kidogo kuliko Dar japo baadhi ya tight na brazia Mwanza ni nafuu na nzuri kuliko za Dar.
- Kampala chupi nyingi ni quality ya kati (si lonya wala high quality) na nafuu. Tatizo hawana brazia nzuri na tight nzuri.
Muuzaji
Kwa uzoefu wangu, wateja wengi hasa wadada (ambao ndio kundi kubwa) wanapenda wauzaji wa kiume hasa akiwa mchangamfu na mwenye kauli nzuri. Muuzaji asipitilize na kuleta utani na mitongozo.- Mabinti wadogo wana aibu, wanapenda wauzaji wa kike, uzuri wao si wanunuzi sana. Bado wanafunzi wasio na kipato.
- Wamama watu wazima sana wanapenda wauzaji wa kike, hawapendelei wauzaji wa kiume ila endapo akimpokea na kumsemesha kwa heshima, ananunua.
- Wanaume wanapenda wauzaji jinsi zote tu. Akimkuta muuzaji wa kike atatamani ajue yeye anapenda ipi, aikiamini atakachopenda muuzaji basi na mwenza wake atakipenda pia. Akikuta wa kiume anatamani ampe uzoefu wateja wengi wa kike wengi wanachagua zipi. Hili nalo ni kundi dogo.
Ni chupi tu?
Hapana, lazima uuze na skin tight, brazia, lesso, sox, night dress,vest, boxer n.k wateja wapenda duka lenye bidhaa tofauti (one stop centre) ili amalize shida zake hapo.
Changamoto
- Mzigo kupitwa na fashion. Usirudie mzigo mara nyingi hata kama ulipendwa. Mara zote uwe na vitu vipya.
- Wauzaji wa kiume kuingia kwenye mapenzi na wateja.
- Biashara kuwa kijiwe cha story hadi kuziba wateja. Wadada wanaongea sana hasa ukiwachangamkia na wakikuzoea.
- Mteja kutaka kurudisha / kubadirisha nguo ya ndani baada ya kufika nayo nyumbani. Usikubali. Bora anune umpoteze coz hata ukimkubalia utampoteza pia coz atajua ndio mchezo wako.
Kumbuka kutoa zawadi kwa wale wateja wa siku zote na kwa wale wanaonunua mzigo mkubwa. Mf. Kanunua chupi 8 @ Tsh 3000 - Tsh 4000, mpe hata lesso ya 500. Haitokufilisi ila atafurahi sana na utamteka.
Habari bro,vipi bado unapambana na biashara ya chupi? Mwanza mzigo ulichukua sehemu gani?Sawa kaka ntaludi tena aice maana nimesaga sana sori kutafta ajira almost miaka mi 5 nashukuru niliukumbuka huu mchango wako humu nikabidi niusake nikaufanyia kazi kwa mda huu nipo huku visiwani nakomaa
Asante mkuuUpo vizuri
Asante mkuuSafi mkuu , umetema nondo zote
Mkuu.. mi naomba mwongozo wa biashara ya sidiria tuu.. za mtumba zile..Asante mkuu
Be blassed ni wachache sana wanaweza kufunguka kiasi hiki wengi wabifsi sanaNgoja nieleze kwa uzoefu wangu mdogo kuhusu hii biashara.
Aina za chupi
Chupi zipo za ubora tofauti kulingana na material. Kuanzia za dozen (dzn) Tsh 8,000 hadi Tsh 45,000 na kuendelea.
Makundi ya chupi
Ninayatenga makundi kulingana na bei na ubora (quality) ya chupi.
1. Kundi la kila dzn Tsh. 8,000 hadi 14,000. Hili tunaliita lonya. Ni zile nyepesi (za wateja wa kipato cha chini).
2. Kundi la kila dzn Tsh 15,000 hadi 32,000. Hili ni la ubora wa kati (za wateja wa kipato cha kati).
3. Kundi la kila dzn Tsh 34,000 na kuendelea ni high quality (hizi za wa kipato cha juu).
Juwa aina ya wateja wako ujue kundi gani la ubora ulangue zaidi. Si mbaya kuchanganya ila isiwe nusu lonya na nusu high quality. Chagua kundi utakalojikita nalo. Mfano, kama wateja uliowalenga ni wa kipato cha chini basi jaza lonya na quality chache, na kinyume chake ni kweli (vice versa is true).
View attachment 1320903
Mtaji kiasi gani?
Inategemea na quality ya chupi uliyoamua kuuza. Mil 2 hadi 3 inaweza kukupa dzn 150 hadi dzn 200 za lonya, huku fedha hiyo hiyo ikakupa dzn 50 hadi 60 ya zile quality. Mtaji unaamuliwa na aina ya mzigo kulingana na kundi la wateja uliowalenga.
Size na aina ya wateja.
Wakati wa kulangua mzigo zingatia uchaguzi wa size kulingana na mahali unakokwenda kuuza. Kumbuka wanunua chupi zaidi ni wadada wa rika la kati, umri miaka 20 hadi 35. Sababu ni kuwa wengi hawana majukumu mengi ya kimaisha, wanajipenda na wako kwenye mahusiano ya mapenzi motomoto (wanatamani chupi nzuri na nyingi ili kuwavutia wenza wao). So, size za kundi hili ndizo ziwe nyingi.
Wapi utapata mzigo wa jumla?
1. Dsm, Kariakoo mtaa wa Msimbazi na muhonda zipo lonya nyingi sana.
2. Dsm, Kariakoo mtaa wa mchikichini na Manyema (kama sijakosea majina) jirani na ukumbi wa DDC. Hapo kuna quality nyingi. Pia yapo maduka machache kule mtaa wa Congo, mtaa wa Mchikichi na Nyamwezi, n.k
View attachment 1316585
3. Mwanza pembeni ya njia panda ya barabara ya Pamba na Miti mirefu. Upande wa stand ya zamani ya Tanganyika. Maduka yako bondeni kidogo (yamejificha).
4. Kampala, Uganda kuanzia makutano ya William street na Ben Kiwanuka Rd, na ukiteremka na hiyo Ben Kiwanuka hadi unakaribia njia panda ya stend ya zamani ya daladala (Kampala Old Tax park). Kabla ya hiyo njia panda kuna maduka yako ndani ndani.
Kumbuka; maduka mengi ya barabarani hapo William street na Kikuubo Rd (tamka Chikuubo) yenye wauzaji wengi ni ya rejareja, maduka ya jumla yako ndani. Kampala duka 1 wanaweza changia watu hata 6, kila mtu anauza upande wake. So, ukiona duka la nje limejaa na lina wauzaji wengi basi kuwa makini, wakijua ni mgeni nao wanajifanya wanauza jumla, then unapunguziwa kidogo kwenye bei yao ya rejareja so unakuwa umepigwa.
Zingatia;
- Dsm unapata mzigo wa aina zote kwa bei nzuri
- Mwanza mzigo mwingi ni ile quality ya kati na unatoka Kampala na Nairobi. Nairobi zinatoka Skin tight na brazia nzuri na baadhi hazipo Dar. Bei za Mwanza ni juu kidogo kuliko Dar japo baadhi ya tight na brazia Mwanza ni nafuu na nzuri kuliko za Dar.
- Kampala chupi nyingi ni quality ya kati (si lonya wala high quality) na nafuu. Tatizo hawana brazia nzuri na tight nzuri.
Muuzaji
Kwa uzoefu wangu, wateja wengi hasa wadada (ambao ndio kundi kubwa) wanapenda wauzaji wa kiume hasa akiwa mchangamfu na mwenye kauli nzuri. Muuzaji asipitilize na kuleta utani na mitongozo.- Mabinti wadogo wana aibu, wanapenda wauzaji wa kike, uzuri wao si wanunuzi sana maana bado wanafunzi wasio na kipato. Hili ni kundi dogo.
- Wamama watu wazima sana wanapenda wauzaji wa kike, hawapendelei wauzaji wa kiume ila endapo akimpokea na kumsemesha kwa heshima, ananunua. Hili nalo ni kundi dogo.
- Wanaume wanapenda wauzaji wa jinsi zote tu. Akimkuta muuzaji wa kike atatamani ajue yeye anapenda ipi, akiamini atakachopenda muuzaji basi na mwenza wake atakipenda pia. Akikuta muuzaji wa kiume anatamani ampe uzoefu wateja wengi wa kike wanachagua zipi. Hili nalo ni kundi dogo.
Ni chupi tu?
Hapana, lazima uuze na skin tight, brazia, lesso, sox, night dress,vest, boxer n.k wateja wapenda duka lenye bidhaa tofauti (one stop centre) ili amalize shida zake hapo.
Changamoto
- Mzigo kupitwa na fashion. Usirudie mzigo mara nyingi hata kama ulipendwa. Mara zote uwe na vitu vipya. Design ukishaileta mara 3 au 4 iache hata kama bado wateja wachache wanaiulizia.
- Wauzaji wa kiume kuingia kwenye mapenzi na wateja.
- Biashara kuwa kijiwe cha story hadi kuziba wateja. Wadada wanaongea sana hasa ukiwachangamkia na wakikuzoea. Epuka hili.
- Mteja kutaka kurudisha / kubadirisha nguo ya ndani baada ya kufika nayo nyumbani. Usikubali. Bora anune umpoteze coz hata ukimkubalia utampoteza pia coz atajua ndio mchezo wako.
- Wateja wa kike kupenda mikopo mikopo. Usikubali.
Kumbuka kutoa zawadi kwa wale wateja wa siku zote na kwa wale wanaonunua mzigo mkubwa. Mf. Kanunua chupi 8 @ Tsh 3000 - Tsh 4000, mpe hata lesso ya 500. Haitokufilisi ila atafurahi sana na utamteka.
Karibuni kwa maswali.
Amina mkuu. AsanteBe blassed ni wachache sana wanaweza kufunguka kiasi hiki wengi wabifsi sana
Sina uzoefu na biashara ya mtumba. Wataalam watakuja kukupa nondoMkuu.. mi naomba mwongozo wa biashara ya sidiria tuu.. za mtumba zile..
Bei ya belo, changamoto, namna ya kupata belo zuri n.k