Biashara ya printing inalipa?

Cash Generating Unit

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2019
Posts
13,286
Reaction score
39,418
Wakuu wajasiliamali mambo ni vipi? Tukiendelea na hustles za kila siku leo nmekuja na hii.,,

Nimebahatika kupata printer mpya kabisaa buree brand ni EPSON L850 ina uwezo wa kuprint coloured, photo, kuscan na kutoa copy.

Sasa nikakumbuka na dogo langu ana goli karibu na chuo huko mkoani nataka ipeleka ikapige kazi kuliko niuze bora nizalishie.

Kwa wataalam wa hii biashara naombeni msaada na maelezo juu ya hii plan yangu. Bei elekezi na vifaa vyake kama wino nk.

Pia inatumia network (internet)
 
Inalipa, yanihapo kama huyo dogo ni mtaalam wa graphics anaweza tengeneza posters, stickers za kubandika kwenye bidhaa za wajasiliamali hiyo printer inaweza kuprint hivyo vitu. Nunua zile karatasi za sticker weka pale fanya kazi.
 
Inalipa, yanihapo kama huyo dogo ni mtaalam wa graphics anaweza tengeneza posters, stickers za kubandika kwenye bidhaa za wajasiliamali hiyo printer inaweza kuprint hivyo vitu. Nunua zile karatasi za sticker weka pale fanya kazi.

Shukran sana[emoji120]
 
Nasikia printer za Epson zimewaweka watu mjini wanasema hazitumii wino mwingi ndio maana hapa mwanza wanaprint kwa shilingi 50
ninayo epson l382 kwa matumizi ya ofisi, hii ibauzwa 380K hadi 420K.

Unapoinunua utaweza kuprint page hadi elf 4 za black and white na za rangi kama elf 1

inasafisha pia picha na passport size kwa zile karatasi za picha, hapa unaweza kusafisha nyingi tu na kuna faida kubwa,

hizo copy elf 4 ningechaji shilingi 100 kwa page, mapato ni laki 4, gharama ya wino hapa ni vichupa viwili tu vya elf 4 jumla elf 8

wino wa rangi nao unatoa page za kutosha za rim na unaweza kutumika kusafisha picha za za albun na passport, kuprint rangi kwa rim 300, kusafisha picha ya album 500, passport size 2000. pesa ipo ya kutosha tu unaingiza milioni kwa gharama ya vichupa vya elf 20


Ni biashara nzuri pia kwa wanafunzi wa vyuoni, unaweka printer chumbani kwako, hata umeme ukirudi usiku bado unaendelea na kazi.

Hapo komaa utumie kitambulisho cha wafanya biashara wadogo cha elf 20 kwa mwaka ,
 
Kama vile kilimo cha kwenye karatasi, kwa mtaji wa laki 5 kilimo cha matikit unavuna million 10

Naomba nitoe somo upande upande wa changamoto
Machine kula karatasi, wino kumwagika, machine kuzingua
Frame ya biashara, usafi, TRA, ulinzi,

Na kwasabubu kijijini kumbuka raia sio wengi, na pia hautakua peke yako uki run hiyo mishe

Na kwasababu maeneo ya chuo kuna kipindi cha likizo za chuo ni kipindi cha ukata sana. Ujipange sana

Ndio maana kuna wajinga pale bungen wanakuambia watu wajiajiri lakini wao hawataki kuachia viti

Business is faith,
 
Nilikuwa nayo wakati niko chuo, hakika nilikuwa sikosi 80k-100k kwa mwezi as minimum.
 

Maelezo yako yamejitosheleza sana mkuu shukrani
 

Mkuu si picha zote za simu na camera pia
 
Printing inalipa ila usitegemee hizo printing za kawaida target printing ya stickers, posters, flyers, business cards, kadi za mialiko hizo zina pesa Sana, ila kitu kikubwa jifunze graphics, yani graphics ukijua hapo utapiga Sana pesa, Nina uzoefu maana Nina L805 na pia Nina utaalamu wa graphics, Niku mfano was kazi ya kadi za mialiko, Kuna mteja alikua anataka kadi Mia mbili, hizi kadi Kila Moja namuuzia mia tano ni kadi ambazo kwenye karatas Moja zinatoka nne,

Kumbuka hapa tunatumia karatas za gloss paper ngum zinang'aa pande zote ambazo bundle Moja kwa huku nilipo Ni elfu kumi na katika bando Moja Kuna pc 50, kwahiyo kwa kadi Mia mbili natumia bando Moja ambalo nimenunua elfu kumi 10, na kazi ya kadi 200 mteja atalipia laki Moja, nikitoa elfu kumi inabaki 90, kumbuka wino wake hua hizi Epson za L805 zina tank sita na nikichukua wino zote sita kwa being ya jumla napewa kwa elf 24, na nikichukua hizi wino sita kwa pamoja ntapiga kazi nyingi Sana sana, so tuchukue 10k kwa ajili ya karatas na 24k kwa ajili ya wino inakua 34k ukitoa laki inabk 66k. Huo wino utapiga kazi mwezi mzima.

Hii business ya printing ina faida Sana Sana, kikubwa jifunze graphics tuu uwe mtaalamu utapiga sana pesa, Kuna kazi inakuja kwa siku unalaza laki mbili faida tuu ukitoa expenses zote.
 
Samahani kama nitakuwa nakukwaza.
Epson L382

Black colour _ 13000 pages
Coloured _ 65000 pages

Wino ni 4 colour (Black, Yellow, Magenta na Cyan)

Inashauriwa cartridges zote ziwe na wino hata kama hauutumii, hii itafanya head isichoke haraka kwakuwa kavu.
 
Asante kwa ushauri, Dah hii mashine najiulizaga kila siku wino mbona hauishi tu

kwa kopi hizo 6,500 za rangi na 13,000 black and white wacha watu wale maisha.

Wino sio changamoto asante kwa bei rafiki ya buku 3 hadi 5 kwa kachupa ka wino, Ni gharama karibu na sifuri kuihudumia hii mashine ukilinganisha na faida utayopata endapo utaitumia kwenye biashara,
 
Asante kwa ushauri, Dah hii mashine najiulizaga kila siku wino mbona hauishi tu 😂😂

kwa kopi hizo 6,500 za rangi na 13,000 black and white wacha watu wale maisha.

Wino sio changamoto asante kwa bei rafiki ya buku 3 hadi 5 kwa kachupa ka wino, Ni gharama karibu na sifuri kuihudumia hii mashine ukilinganisha na faida utayopata endapo utaitumia kwenye biashara,

Pia kwa wenye bajeti finyu kuna huyu mjuba nae yupo fresh tu. nmechukua picha kutoka duka la "discount kubwa" lipo kariakoo

 
Hawa discount kubwa naomba contacts zao mkuu
 

Mkuu unapatikana wap
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…