Leo naanza mchakato wa kutafuta chumba...
nitaleta update
Heshima kwenu.
Naomba kama kuna mtu ana uzoefu na saloon za kunyoa anipe uzoefu, tena zile za 1000 kichwa maana kwa hesabu zangu nikilipa chumba 40,000/50,000 na nikiongea na kinyozi anipe 10,000 kila siku na nikaiboresha si nitapata?
au mnanishauri vip?
Mahitajio ya awali kwa saluni ya kawaida-
1.chumba elfu 50
2.vioo laki 1.5
3.mashine mbili laki 2
4.Viti vya kunyolea 2 laki 2
5.Makochi laki 3
6.TV+Radio laki 3
7.Vitambaa,vitaulo,sprit,poda,mafuta,picha za mitindo,sabuni. vyote kwa elfu 50.
Jumla ni tsh 1,250,000/-
Aina hii ya salun kama ukipata eneo zuri kibiashara inaweza kukulipa.
Sasa hili jukwaa kazi yake nini ?
Dah....!! Hii Budget mbona kama iko chini sana? ni kwa mkoa gani?
Mkuu mashine ya kunyolea ikiwa inauzwa chini ya laki kuwa makini kuikagua kama original ama na mara utajuta hyo mashine ni feki na kama ni feki baada mwezi 1ama 2 huanza kusumbua..mi naona kama ameandika bei ya juu maana mashine nataka kununua za 60,000@.
alafu TV,DEC,Kochi vyote ninavyo,na mashine moja tiyari ninayo.
mkuu kuna nyuzi nyingi humu zitakusaidia
ila nazani suala la mshahara ni maelewano tu ,kutokana na hadhi ya saloon!
Una mtaj kias gan mkuu?