Biashara ya salon za kiume na kike

Biashara ya salon za kiume na kike

Salon ya kiume Andaa 2.5M
Naanzaa na hair cutting @ 1 120000
Salon chair vya kawaida kabisa @1 350000
Viooo vya Ukutani andaaa jumlaa ya tsh laki 500000
Kama utaweka mlango wa kioo mlangoni ni 450000
Madawa Pamoja na vifaa vitambaa sijui chana n.k ni 200000
Kama unataka Ac ni 500000 jeshini
Kama utaweka feni ni @1 45000-100000 inategemea na Aina
Makabati ya salon kama utaweka andaaa 250000
Kama unataka tengeneza kochi ni 200000
Yaaani kwa ufupi sana ndio vitu kama hivyo.....Nina salon yangu ya kiume...ni PM namba yako nitakucheki tuongeew vizuri piaa nikuelekeze wapi ukanunue....
Location ya salon yako ni muhimu sana.....Inlipaa sana ukitengeneza ya kisasa sababu ndani ya miezi 4 ila yako inarudi na unaanzaa kulaa faida....

[HASHTAG]#Utajiri[/HASHTAG] ni upo mikononi mwetu
Bado upo kwenye biashara mkuu?
 
Hebu dadavua mkuu
From my experience,kwa siku saluni ya kike inaingiza hd elfu 70 na kuendelea kutegemea n eneo lenyewe. Ishu ni wadada wahudumu wa saluni,wengi hawatulii wanarubuniwa sana hasa wanaojua kusuka vzr lkn pia wanaiba sana. Anaweza akasuka na hela isiingie kwenye hesabu. Au anaweza Kuwa na Rasta zake na dawa zake pembeni. Usipokuwepo anatuma zake.
 
Mimi sifanyi biashara hii Japo ni mteja wa saloon nzuri na nazipenda kweli kweli. Kwa upande wangu yafuatayo ni muhimu
Saloon ya kiume:
1. Fanya survey na maongezi ya kutosha na vijana watakao kua vinyozi, wengi wao huwa hawajielewi na wanakua na pozi kwa Wateja(customer care ya mhudumu kwa mteja ni muhimu sana) wavalishe uniform

2. Upate nyumba yenye nafasi in which itakua na section kama tatu au nne hivi, iwe na shaving pool, customer waiting area,washing and scrabbing chamber na massage room.

3. Mkuu uwe na mabinti wazuri kama watatu hivi, kwa ajili ya scrabbling,pedicure na manicure plus body massage. Make sure wanakua na uniform kali, siku nyingine vitenge,vikaptula,skin jeans ,tyt n.k. Make sure wanavaa uniform na wafundishe kauli nzur kwa Wateja.

4. Uwe na kafriji kwa saloon yako, make sure ktk bei zako za kunyolea na Huduma nyingine una include na kaela ka soda kwa mteja ila mteja asijue kua ananunua soda. Mteja akiwa nasubiria zamu ya kunyolewa unampa kasoda au Maji na vikaranga fulani amazing,Basi atajiona mfalme na kamwe yaani.

5. Utakapofungua chukua week mbili au mwezi kusoma mazingira ya biashara,then cha kufanya kwa vijana vinyozi unawapa hesabu ya siku au week, kua ww kijana jilipe ila kwa week niletee elfu 70 mezani. Hao ni vinyozi haihusiani na Huduma nyingine.

6. Unapofungua jitahd ndani ya mwezi wa kwanza wa kuanza,Nenda kwenye hit radio station moja ya hapo dom Fanya tangazo ili wakazi wa wajue zawadi ulowaletea.

Kwa saloon ya kike.
Mkuu hii kwa upeo wangu kama mkeo siyo expert wa mambo haya utapata tabu kiasi, management ya wahudumu wa saloon za kike ni ngumu sana.

Tatizo wadada wanafanya ktk saloon hizi hawatulii,wanarukaruka kama nkiwa,Leo yupo hapa,kesho Singida,keshokutwa Utaikuta Mwanza.

Ila ukipata waliotulia utapiga hela. Labda uwachukue na uwafanyie treatment nzuri kuwajenga kisaikolojia watulie. Sasa hapo itabid upate wa sekta zote.
Kusuka, kushonea sijui ndiyo mawigi sijui mawiving, make up n.k. yaan kila sekta iwe na mtaalamu kias ya kwamba hakuna mteja wa kuchomoka.

Customer care ni muhimu pande zote ..
That's all in me sir
good advice . .... although its not hygienic/healthy to consume or eat inside a Barber shop or hair salon
 
Mimi ni mkazi wa Mbeya, Tunduma, niliwaza swala la kujiajiri, nikaona sina kipaji kingine zaidi ya ususi wa nywele, sasa naombeni ushauri, na mtaji wake unaweza kuwa kiasi kagi, tafadhali naombeni msaada wenu.

Ahsante
 
Wanajukwaa, nawasalimu katika jina la kujitegemea.

Nina wazo na nimeanza kutenga sehemu ya pato langu ili nianzishe biashara itakayo niongezea katika kidogo changu nacho pata kila mwisho wa mwezi.

Naomba kusaidiwa katika makadirio hasa katika biashara ya SALON YA KISASA YA KIUME.

Nina imani wajumvi mtanisaidia nini na kiasi gani nahitaji kuwa nacho.

Asanteni na amani iwe kwenu.
 
Nina wazo na nimeanza kutenga sehemu ya pato langu ili nianzishe biashara itakayo niongezea katika kidogo changu nacho pata kila mwisho wa mwezi.

Naomba kusaidiwa katika makadirio hasa katika biashara ya SALON YA KISASA YA KIUME
Ni vigumu kupata figure kamili ya ghalama yote. Ghalama kubwa au ndogo itategemea nini na nini utaweka kwenye salon yako.
--------
KWA SASA FANYIA KAZI HIVI VIPENGELE
- Location sahihi ya kufungua hii huduma - Hapa utakuwa umelenga soko lako ni lipi hasa; Mfano wa maeneo mazuri ni (a) kati kati ya mji au (b)Maeneo Jirani na Taasisi kama vyuo vikuu au shule za bweni et al
- Fahamu ni vifaa gani vitakavyo hitajika na ghalama zake ni zipi

Baadhi ya vifaa ambavyo inatakiwa ufahamu bei zake kwanza ni kama ifuatavyo.

*2x Basic barber chairs
*2x WAHL Clippers - Hakikisha unapata mashine OG za kunyolea, ambazo hazipati JOTO zikitumika kwa muda mrefu, Napendekeza hii brand hasa series 3000, Sababu ni bora na ghalama nafuu.
*Equipment Sterilizer
*Cosmetic Products
*Fabric sheets, towels, apron
*Hair Style Charts
*2x Waiting or Lounge Chairs
*Water heating & storage
*Small Basins
*Backup Generator
*Entertainment System

WAPI UTAPATA VIFAA VYENYE UBORA
- Tafuta kwenye maduka makubwa dar / arusha
- Pia angalia mtandaoni ( Nunua mtandaoni iwapo tu utakuwa umeokoa kiasi fulani cha fedha ukilinganisha na kununua hapa nchini)
- Mfano HAI ni hizi WAHL Clippers - Kwa maduka ya TZ yaliyomengi bei ni kati ya TZS 140,000 hadi 250,000 kwa moja (1) tu. Lakini ukiangalia picha hapa chini utaona nimenunua clippers mbili (2) kwa TZS 178,259 tu ( Ni bidhaa kutoka UK, Ni order ya mwana JF mwenzetu)
upload_2017-4-29_5-29-33.png


upload_2017-4-29_5-30-52.png


upload_2017-4-29_5-30-0.png

------
Kwa kununua toka nje ya nchi kwa Baadhi ya vifaa tumia hii thread www.v.ht/buy4me

Bila shaka kwa ufahamu wangu mdogo utakuwa umepata mwanga kwa kiasi fulani ili kufikia lengo lako.

KARIBU

upload_2017-4-29_5-36-15.png
 
Ujue kufngua so tatizo ila shughuri wafanya kaz ni wasumbufu hatar ndug mpaka nataman funga ya kike yan waznguaji balaaa
 
Ni vigumu kupata figure kamili ya ghalama yote. Ghalama kubwa au ndogo itategemea nini na nini utaweka kwenye salon yako.
--------
KWA SASA FANYIA KAZI HIVI VIPENGELE
- Location sahihi ya kufungua hii huduma - Hapa utakuwa umelenga soko lako ni lipi hasa; Mfano wa maeneo mazuri ni (a) kati kati ya mji au (b)Maeneo Jirani na Taasisi kama vyuo vikuu au shule za bweni et al
- Fahamu ni vifaa gani vitakavyo hitajika na ghalama zake ni zipi

Baadhi ya vifaa ambavyo inatakiwa ufahamu bei zake kwanza ni kama ifuatavyo.

*2x Basic barber chairs
*2x WAHL Clippers - Hakikisha unapata mashine OG za kunyolea, ambazo hazipati JOTO zikitumika kwa muda mrefu, Napendekeza hii brand hasa series 3000, Sababu ni bora na ghalama nafuu.
*Equipment Sterilizer
*Cosmetic Products
*Fabric sheets, towels, apron
*Hair Style Charts
*2x Waiting or Lounge Chairs
*Water heating & storage
*Small Basins
*Backup Generator
*Entertainment System

WAPI UTAPATA VIFAA VYENYE UBORA
- Tafuta kwenye maduka makubwa dar / arusha
- Pia angalia mtandaoni ( Nunua mtandaoni iwapo tu utakuwa umeokoa kiasi fulani cha fedha ukilinganisha na kununua hapa nchini)
- Mfano HAI ni hizi WAHL Clippers - Kwa maduka ya TZ yaliyomengi bei ni kati ya TZS 140,000 hadi 250,000 kwa moja (1) tu. Lakini ukiangalia picha hapa chini utaona nimenunua clippers mbili (2) kwa TZS 178,259 tu ( Ni bidhaa kutoka UK, Ni order ya mwana JF mwenzetu)
View attachment 502364

View attachment 502366

View attachment 502365
------
Kwa kununua toka nje ya nchi kwa Baadhi ya vifaa tumia hii thread www.v.ht/buy4me

Bila shaka kwa ufahamu wangu mdogo utakuwa umepata mwanga kwa kiasi fulani ili kufikia lengo lako.

KARIBU

View attachment 502367
Pasi na kupepesa macho, moyo wangu umefarijika na kuona wako Vijana wenzangu mnao tambua juhudi za Vijana wenzenu. Umenifungua na naamini ntahitaji msaada wako, Naomba kama naweza kukupata inbox tafadhali.

0756 73 72 71
 
Mkuu saloon mtu halipwi mwisho wa mwezi bali ni makubaliano yenu kama mnanyoa kichwa elf 3 unaweza mwambia kinyozi ye achukue 1000 we bok 2 kwa kuanza kama ni babashop uwe na ml 7 mpaka 10
 
BIASHARA YA SALON YA KIUME.

Habari za majukumu wanaMwanza, nina salon yangu ya kiume iliyopo Mwanza mjini, eneo la Mabatini, Mtaa wa Kleruu, Nyumba namba 263/09. Ni salon ya kiume, imekuwepo tokea mwaka 2012 na ina viti 2 (viwili) vya kunyolea. Ni salon ya hadhi ya kati. Ina vitu vyote vya muhimu katika salon ya kiume ikiwemo na sehemu maalum ya kuoshea baada ya mteja kunyolewa.
Salon hii nina nia ya kutokuendelea kuiendesha na ninahitaji mtu ambaye atakuwa tayari KUINUNUA/KUIKODISHA ama akanunua vifaa vyote vya salon vilivyomo humo nami nikamalizana nae.

Bei ya KUINUNUA/KUIKODISHA ni maelewano endapo mtu ataonesha nia ya kweli.
Kwa aliyetayari kuwekeza katiaka salon ya kiume tafadahali sana tuwasialiane kwa mawasialiano yafuatayo:

NAMBA ZA SIMU: 0768 111 123 AU 0787 111 123 (PIGA, SMS AU WHATSAPP KWA 0787 111 123)

BARUA PEPE: mkisusi@gmail.com

SKYPE: Kisusi.Mohammed

FACEBOOK MESSENGER: Kisusi Mohammed

Ntashukuru sana kwa kuwasiliana nami kwa ajili ya biashara hii.
 
Karibu sana mkuu, kuwa nazo ni maamuzi tu. Unaweza kudhani huna kumbe mimi natamani hizo ulizonazo. Tumshukuru Mungu kwa kila hali.
 
Habari wakuu,

Kama heading inavyojieleza hapo juu. Lengo la uzi ni kukutanisha wafanyabiashara na wanaotaraji kufanya biashara ya salon za kiume.

Tupeane changamoto, opportunities, strength na weaknesses ambazo kwa namna moja ama nyingine zinachangia maendeleo ama kuporomoka kwa biashara hii. Tupeane uzoefu na kila nmana ya mambo yanayofaa kwa maendeleo ya biashara hiyo.

Salon ndogo na kubwa. Iwe kichochoroni ama along streets lengo ni kuboresha na kuleta ufanisi.

Naamini wadau tutajumuika pamoja. Asanteni.
 
Back
Top Bottom