Biashara ya simu used

Joined
Apr 20, 2014
Posts
20
Reaction score
10
Habari wapambanaji wa kutafuta ugali wa kila siku. Mpambanaji mwenzenu nimekuja kwenu mnijuze wapi naweza pata simu used za halali sio za wizi Kwa bei ya jumla nami nikafanya biashara.

Sijajua wafanya biashara wa Kariakoo wanazitoa wapi na ukijaribu kumuuliza mfanya biashara yeyote Kariakoo hawezi kukwambia ukweli atakuzungusha zungusha Tu na kukwambia mtaji wa hela nyingi ili ukate tamaa.
 
Simu used zinapatika nchi zote za dunia ya kwanza. Bongo wengi wanachukuwa nchi za kiarabu hasa Dubai.
 
Nilifanya biashara ya simu used nlipigaga sana hela sema sasa unakuwa kama jambazi one mistake staki shari hii hapa niliiacha baada ya wanangu kama wawili kwenda segerea mpaka leo na mie kuponyoka kwenye tundu la sindano
Ulikuwa unanunulia Bongo? Hiyo ni hatari sana sana. Simu unatakiwa uzifuate mwenyewe nje ya nchi.
 
Nilifanya biashara ya simu used nlipigaga sana hela sema sasa unakuwa kama jambazi one mistake staki shari hii hapa niliiacha baada ya wanangu kama wawili kwenda segerea mpaka leo na mie kuponyoka kwenye tundu la sindano
😃😃 boss ulikuwa Una nunua simu used za bongo nyingi za wizi pole sana ndio changamoto za upambanaji
 
Uko wapi Boss ,Nikuuzie samsung J7 prime
 
Nilifanya biashara ya simu used nlipigaga sana hela sema sasa unakuwa kama jambazi one mistake staki shari hii hapa niliiacha baada ya wanangu kama wawili kwenda segerea mpaka leo na mie kuponyoka kwenye tundu la sindano
Kwa nini mlikuwa mnawindwa kama jambazi mkuu au mlikuwa mnanunua na kuuza simu za wizi?
 
Hicho ni kipengele ambacho hukijui kwani si kila atauekuuzia simu unamjua na ni mwema.kwenye simu used kuna michezo mingi sana michafu niishie hapo
 
Sawa nilitaka kujua tu kipengele kinachosababisha muwindwe ila nishakuelewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…