Biashara ya spare za pikipiki

Biashara ya spare za pikipiki

Premij canoon

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2018
Posts
1,203
Reaction score
2,771
Salaam wakuu..

Poleni na mitikasi ya january nzima, natumai wewe family yako pamoja na jamii nzima inayokuzunguka ni wazima wa afya njema kabisa.

Naam mimi ni kijana mwenzenu kiumri ninamiaka 23, Nimekua nikijishughulisha na biashara ya forex tangu baada ya kijana ONTARIO kuitambulisha hapa jukwaani nakufungua macho ya wengi ambao tulikua hayuifahamu biashara hii.

Binafsi sikuwahi kusoma pale TMT kutokana na wakati huo nilikua hata pesa ya bando ni mtihani kwangu... Nilikomaa kwakusoma PDFs mbalimbali zilizopatikana free kabisa mtandaoni, nimepmbana kwa kiasi chake na nimeshachoma accounts nyingi hadi kufikia hivi sasa. Nilichogundua biashara ya FOREX bila ya kuwa na chanzo chochote cha mapato nje ya forex ni ngumu na stress mnoo.

Tangu mwaka jana nilikua naumiza kichwa sana kutafuta mtaji kwenye FOREX nije kuwekeza kwenye biashara ya kawaida inayoonekanika kwa macho lakini nimekua nikipiga hatua mbili mbele kwenye account na kurudi hatua nne nyuma, kifupi nilipata tabu sana kukuza account, lazikini sikuweza kukata tamaa kwasababu nilikua nikiamini mambo mazuri sikuzote hayataki haraka.

Sasa mwaka huu imekua ni kama muujiza, yaani sikutegemea japokua nilidhamiria kabisa either do or die.. Kifupi niseme nilijilipua (kwa wadau wa forex watanielewa hapa) maana nilishachoka kufuata risk management na bado unachoma account taratibu taratibu hadi mwisho wasiku balance 0.

Week iliyopita jumaatano nilifanikiwa kupata settup katika pair ya VOLATILITY 75 INDEX.. Nilikua na balance ya $723, sasa niliingia kwenye hiyo trade kwa kujilipua, nilitumia lot size ya 0.20 positions 5. Nilikaa na pressure kwa nusu saa nzima nikisubiri price isogee kidogo mblele ya entry yangu au balance yangu igeuke majivu, lakini mungu alikua upande wangu baada ya price kuchezapale kwenye entry yangu hatimae ikaanza kupanda kwenda juu nakuingia upande wa profit, fasta nika lock profit kisha nikaacha market itembee (lakini nilikua na kiherehere cha kuangalia chart, maana hii pair iko volatile sana[emoji23]). Basi hadi kufika saa 9 alasiri price ilitembea hadi pips 2000 nakupelekea kuingiza $20,000+ [emoji24].

Baada ya hapo sikuchelewa... Fasta nikaingia kuwithdraw hiyo pesa na leo ndio imeingia kwenye acc yangu benki, baada yakupata email tu nikaenda ATM kuhakiki balnce yangu ni ngapi, njia nzima nilikua na kimuhemuhe hadi nimemuachia konda nauli [emoji23]. Kufika ATM mapigo ya moyo yalikua yanaenda mbio kupita maelezo huku jasho likinitoka kama nimekimbizwa.

Basi baada ya kuingiza kadi na kufuata taratibu kadhaa hatimae nakuta balance ya 46,160,000/ na chenji kadhaa. Niliruka kwa furaha maana ndio mara yangu ya kwanza kuingiza kiasi hiki [emoji24].

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

Naam turudi kwenye lengo hasa lililonifanya nije hapa.

Binafsi naishi nje kidogo ya jiji la dar, fursa niliyoiona huku ni biashara ya SPARE ZA PIKIPIKI lakini nilikua nataka kuwa na duka la jumla na reja reja ili nipate kuwauzia hawa wenye maduka madogo madogo wanaokwenda dar kariakoo kufwata spare. Sina ujuzi wala uzoefu wowote wa hii biashara lakini kujifunza ni sehemu yangu ya maisha.

Sasa nilikua nauliza ili niweze kukamilisha hii project je mzigo nitanunulia china au dubai? Na je nimeepanga kuwekeza 25,000,000/ kama mtaji kwenye hii biashara kwa kuanzia... Je, kiasi hiki kitajitosheleza kufungua duka la jumla? Naombeni ushauri na mawazo vijana wenzangu [emoji1431]

Nimeamua kuleta hapa kwanza kabla ya kwenda kutafiti kwa wanaofanya biashara hii.. Naamini JF ni pana na wapo watu wanaofanya biashara hii au wenye information kadhaa zitakazonipa ABC's pakuanzia.

NAWASILISHA.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Kuna Ngosha kadhaa wameishika vizuri sana hii biashara ya spare parties za pikipiki Kariakoo.

Kwa sasa wako mbali sana. Kuna mmoja hadi anatengeneza kwa jina lake zinaitwa MKZ ila jina kapuni.

Ushauri wangu: Kuuza jumla mwanzoni na huna jina inaweza kuwa shida.

Anzia mikoani au nje ya jiji kwa kuwa na duka lako Utakavyokuwa unakuwa na kuielewa biashara
ndiyo utaona siku au muda muafaka wa kuingia kwenye biashara ya jumla na kuwa na duka Kariakoo.

Hao hao utakaokuwa unanunua kwao mwanzo ndiyo watakufundisha mengi.

Siri kubwa ya biashara ni USIWE NA TAMAA na UWE NA UTHUBUTU (kitabu cha Rich Dad, Poor Dad).

Kama utaelewa maana yake basi huna haja ya kusubiri jibu.

Nina jamaa yangu anafanya biashara hiyo. Nimeweza kuwafahamu tayari jamaa kadhaa.
Mimi sifanyi hii biashara ingawa nafanya biashara Indirect.
Kama utataka contact yake basi ntakuunga naye - Inbox.

Good Lucky.
 
Kama una moyo mzuri na kupenda wengine wafanikiwe naomba utuwekee screenshot za trading account history kama ulivyoelezea na ujumbe wa email kama sio wa kutuma na kupokea pesa benki ili kutupa motivation vijana wenzako.
Binafsi ninakomaa sana na biashara hii na Nina mpango wa kudeposit kama dola alfu kumi. Mana Nina pa kuanzia.
Tunaomba motivation yako from Forex trading.
Itapendeza kama ukiweka hapa chart graph entry and your exit points mkuu ili tuone hizo 2000 pips
Premij canoon,
 
Una nauli mkononi na lengo lako ni kuuliza basi la kwenda Mbeya lakini ghafla unaanza stori za namna ulivyosafiri juzi kwenda Arusha, ulivyopita Segera, ukala mishkaki mitamu ya nyani Mombo, ukapita Same na kuona warembo kwenye dirisha la Kilimanjaro express. Ukafika Arusha mkagawiwa pipi ila wewe ukapata nyingi zaidi.

Halafu sasa ndo unauliza umbali wa kutoka Dar kwenda mbeya!

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji108]

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Hukua na haja ya kutiririka kuwa umepataje mtaji vinginevyo una mlengo tofauti. (Nyuzi mbili ndani ya nyuzi moja)
Ungesema tu kuwa una mtaji wa mil 25 unahitaji kufanya biashara ya spare.
 
Hukua na haja ya kutiririka kuwa umepataje mtaji vinginevyo una mlengo tofauti. (Nyuzi mbili ndani ya nyuzi moja)
Ungesema tu kuwa una mtaji wa mil 25 unahitaji kufanya biashara ya spare.

Nashukuru kwa kunisahihisha, hapo nimeteleza. Naomba kama unipe ABC's zozote zitakazoweza kunisaida kwenye shida yangu hapo juu [emoji1431]

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Back
Top Bottom