Biashara ya stationery ya mtaji mdogo iliyoongezewa thamani

music mimi

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2013
Posts
485
Reaction score
876
Wakuu naomba mawazo yenu.

Nina mpango wa kuanzisha stationery ya mtaji mdogo around mil 5 yani umo kila kitu mpaka fremu.

Naomba ushauri zaidi ya kuprint na kutoa copy pamoja na vifaa kama bahasha, rimu, kalamu, etc

Naweza vipi kuongeza thamani kwenye stationery kwa gharama ndogo lakini niwe na vitu vinavyoingiza buku buku kila siku?

Mie nimewaza huduma kama kutafutia watu TIN, kusaidia mifumo kama nest, heslb, loss report, kuomba vyuo na scholarship, kupiga passport size,

Vipi unaweza nishauri vitu vya ziads navyoweza kufanya bila gharama kubwa ila nikaongeza thamani?

Pia mimi nipo Dar mbezi ya kimara, ni location gani nzuri kwa hii biashara maeneo ya huku au ata Dar sehemu nyingine naweza kufika na kufanya research yangu.

Asanteni
 
Weka huduma ya internet (WiFi). Ambapo mwenye uhitaji anakja na kifaa chake anakulipa, iwe ni simu au pc, unamunga.
  • Buku kwa saa moja.
  • Itakulipa sana
Buku kwa saa ni uchawi weka buku jero kwa siku ukipata watu 5 teyari umeingiza 7500 ukijumlisha na hudma nyingine hukosi elfu 30000 faida kwa siku..sio mbaya kwa kuanzia.
Ila zingatia usimamizi tu.
 
Wakuu naomba mawazo yenu.

Nina mpango wa kuanzisha stationery ya mtaji mdogo around mil 5 yani umo kila kitu mpaka fremu.

Naomba ushauri zaidi ya kuprint na kutoa copy pamoja na vifaa kama bahasha, rimu, kalamu, etc

Naweza vipi kuongeza thamani kwenye stationery kwa gharama ndogo lakini niwe na vitu vinavyoingiza buku buku kila siku?

Mie nimewaza huduma kama kutafutia watu TIN, kusaidia mifumo kama nest, heslb, loss report, kuomba vyuo na scholarship, kupiga passport size,

Vipi unaweza nishauri vitu vya ziads navyoweza kufanya bila gharama kubwa ila nikaongeza thamani?

Pia mimi nipo Dar mbezi ya kimara, ni location gani nzuri kwa hii biashara maeneo ya huku au ata Dar sehemu nyingine naweza kufika na kufanya research yangu.

Asanteni
Amka, nenda maeneo unayoyatarget katembelee uone palivyo, mzunguko wake na watu na upepo wa biashara hapo.....

Ukiridhia tafuta frem itengeneze anza kazi, bidhaa za stationery utazipata kariakoo mtaa wa kipata, uhuru road kuna duka linaitwa furaha nilipita wana bei nzuri pia.

Kwa experience yangu ukiwa na jambo lako ukawa unaliombea ombea ushauri na maoni ya watu HALIFANIKIWI
 
Mchawi ni location tu.
Sehemu zenye kulipa ni karibu na maofisi ya umma yenye pilikapilika za watu kuingia humo na kutoka humo (Polisi, Mahakama, TRA, Benki, Wizara, Mashirika) au karibu na vyuo au taasisi za elimu. Hapo usiogope kama kuna stationery zingine ama la, wote mtapiga pesa.

Siri kubwa ya kutoboa ni hizi tatu tu.
1. One stop centre (yaani mteja akifika kwa shughuli za stationery basi apate kila kitu hapo hapo)

2. Ujuzi mzuri, haraka na uhakika wa kutoa huduma za usaidizi (Watu wengi hawana ufahamu wa kupata au kutengeneza document mbalimbali. Kwa mfano kuna mtu anakuja kuprint barua lakini barua aliyoiandaa unakuta imejaa makosa mengi ya kiuandishi (spelling, format, front, content, grammer) na hajui chochote. Sasa wewe ukimsaidia huyo mteja (hata bure) kurekebisha hiyo barua kabla ya kuiprint, basi utakuwa umemkamata mazima na hatakuja kukusahau milele na kila akipita hapo hata chenji ya kunywa soda atakupa.

3. Uhakika wa umeme wakati wote. Kutegemea umeme wa Tanesco tu atapoteza sana. Hilo gap la kukatika katika umeme ndio mchongo wenyewe.
 
Well noted, nitafanyia kazi ushauri wako. Asante sana
 
Mkuu asante sana umeniongezea kitu kwenye kuongeza thamani na location.

Kama ni mzoefu wa Dsm unaweza Nipa suggestions za maeneo kama una idea.

Shukrani sana
 
Sina shaka yoyote na hiyo milioni tano ya mtaji wa kuanzia, inatosha. Wakati wa kuanza huhitaji mbwembwe nyingi, muhimu huduma za kuwapa wateja ziwepo. Wapo wengi wameanza na mtaji mdogo kuliko huo na wakatoboa.
Sawa, nimekupata
 
Wakuu naomba mawazo yenu.

Nina mpango wa kuanzisha stationery ya mtaji mdogo around mil 5 yani umo kila kitu mpaka fremu.

Naomba ushauri zaidi ya kuprint na kutoa copy pamoja na vifaa kama bahasha, rimu, kalamu, etc

Naweza vipi kuongeza thamani kwenye stationery kwa gharama ndogo lakini niwe na vitu vinavyoingiza buku buku kila siku?

Mie nimewaza huduma kama kutafutia watu TIN, kusaidia mifumo kama nest, heslb, loss report, kuomba vyuo na scholarship, kupiga passport size,

Vipi unaweza nishauri vitu vya ziads navyoweza kufanya bila gharama kubwa ila nikaongeza thamani?

Pia mimi nipo Dar mbezi ya kimara, ni location gani nzuri kwa hii biashara maeneo ya huku au ata Dar sehemu nyingine naweza kufika na kufanya research yangu.

Asanteni
Kama umezungukwa na frem halafu zina madada, weka wifi kila asubuhi unawaunga buku moja jero wanatumia mpaka unapofunga.
 
Mchawi ni location tu.
Sehemu zenye kulipa ni karibu na maofisi ya umma yenye pilikapilika za watu kuingia humo na kutoka humo (Polisi, Mahakama, TRA, Benki, Wizara, Mashirika) au karibu na vyuo au taasisi za elimu. Hapo usiogope kama kuna stationery zingine ama la, wote mtapiga pesa.

Siri kubwa ya kutoboa ni hizi tatu tu.
1. One stop centre (yaani mteja akifika kwa shughuli za stationery basi apate kila kitu hapo hapo)

2. Ujuzi mzuri, haraka na uhakika wa kutoa huduma za usaidizi (Watu wengi hawana ufahamu wa kupata au kutengeneza document mbalimbali. Kwa mfano kuna mtu anakuja kuprint barua lakini barua aliyoiandaa unakuta imejaa makosa mengi ya kiuandishi (spelling, format, front, content, grammer) na hajui chochote. Sasa wewe ukimsaidia huyo mteja (hata bure) kurekebisha hiyo barua kabla ya kuiprint, basi utakuwa umemkamata mazima na hatakuja kukusahau milele na kila akipita hapo hata chenji ya kunywa soda atakupa.

3. Uhakika wa umeme wakati wote. Kutegemea umeme wa Tanesco tu atapoteza sana. Hilo gap la kukatika katika umeme ndio mchongo wenyewe.
Nadhani ungemsaidia na hardware zinazotakiwa(computer zenye ukubwa gani, printer nk nk)za kuanzia kuendeshea biashara hiyo, ingelipendeza sana.

Maana kwa comment yako yaonesha wewe ni mzoefu ama ni intelligent person. Shukrani.
 
Mpango wako wa kuanzisha stationery unaonekana kuwa mzuri na umejumuisha huduma muhimu ambazo zinaweza kuvutia wateja. Ili kuongeza thamani kwa gharama ndogo, unaweza kuzingatia mambo yafuatayo:
  1. Huduma za Kucharaza Barua na CV: Toa huduma ya kuandika na kuchapisha barua za kikazi, CV, na wasifu wa kitaalamu (resume) kwa watu wanaotafuta kazi au fursa za masomo.
  2. Huduma za Kutoa Viapolo/Notarization: Kwa gharama ya chini, unaweza kuingia kwenye ushirikiano na wakili au mthibitishaji ili wateja wawezeshwe kuthibitisha nyaraka zao kwenye stationery yako.
  3. Kuweka Kioski cha Intaneti: Weka kompyuta chache kwa ajili ya wateja kutumia intaneti kwa shughuli kama kuomba kazi, vyuo, au kufanya utafiti mdogo. au pia weka router watu wa karibu na stationary yako wanaweza kutuma kwa gharama ndogo ya buku kwa siku.
  4. Kubuni na Kuchapisha Kadi za Biashara au Mabango: Toa huduma za kubuni na kuchapisha kadi za biashara, mabango madogo (brochures), na vyeti.
  5. Photocopy ya Kitabu Kikubwa (Binding Services): Ongeza huduma ya kufunga nyaraka na vitabu vikubwa vya taarifa au ripoti.
  6. Stationery ya Ubunifu: Nunua bidhaa za ubunifu kama vibandiko vya kiofisi, karatasi za rangi tofauti, na vifaa vingine vya kazi za mikono, ambavyo vinahitajika sana na wanafunzi na walimu.
Kuhusu location, unaweza kufanya utafiti maeneo yenye taasisi za elimu kama vyuo, shule, au karibu na ofisi za serikali kwani kuna watu wengi wanaohitaji huduma za stationery. Mbezi Kimara ni eneo zuri, lakini pia unaweza kuangalia maeneo yenye msongamano wa watu kama Kariakoo au Sinza.
Ukifanikisha kuongeza huduma hizi, unaweza kuvutia wateja wengi zaidi na kuongeza mapato kila siku.
Wakuu naomba mawazo yenu.

Nina mpango wa kuanzisha stationery ya mtaji mdogo around mil 5 yani umo kila kitu mpaka fremu.

Naomba ushauri zaidi ya kuprint na kutoa copy pamoja na vifaa kama bahasha, rimu, kalamu, etc

Naweza vipi kuongeza thamani kwenye stationery kwa gharama ndogo lakini niwe na vitu vinavyoingiza buku buku kila siku?

Mie nimewaza huduma kama kutafutia watu TIN, kusaidia mifumo kama nest, heslb, loss report, kuomba vyuo na scholarship, kupiga passport size,

Vipi unaweza nishauri vitu vya ziads navyoweza kufanya bila gharama kubwa ila nikaongeza thamani?

Pia mimi nipo Dar mbezi ya kimara, ni location gani nzuri kwa hii biashara maeneo ya huku au ata Dar sehemu nyingine naweza kufika na kufanya research yangu.

Asanteni
 
Wakuu naomba mawazo yenu.

Nina mpango wa kuanzisha stationery ya mtaji mdogo around mil 5 yani umo kila kitu mpaka fremu.

Naomba ushauri zaidi ya kuprint na kutoa copy pamoja na vifaa kama bahasha, rimu, kalamu, etc

Naweza vipi kuongeza thamani kwenye stationery kwa gharama ndogo lakini niwe na vitu vinavyoingiza buku buku kila siku?

Mie nimewaza huduma kama kutafutia watu TIN, kusaidia mifumo kama nest, heslb, loss report, kuomba vyuo na scholarship, kupiga passport size,

Vipi unaweza nishauri vitu vya ziads navyoweza kufanya bila gharama kubwa ila nikaongeza thamani?

Pia mimi nipo Dar mbezi ya kimara, ni location gani nzuri kwa hii biashara maeneo ya huku au ata Dar sehemu nyingine naweza kufika na kufanya research yangu.

Asanteni
Kuna Rita, kuna nida,
 
Back
Top Bottom