Biashara ya Subwoofer

Biashara ya Subwoofer

View attachment 2737846

Bei Ya China Bila Usafiri 60000 kila box (Sabufa Kubwa)
Makadirio Usafiri na tozo za serikali kwa meli 40000 kwa box (Unalipia baada ya mzigo kufika bongo)
Makadirio Muda wa usafiri siku 30-45
Kima cha chini kuagiza (Moq) 20
Gharama zangu ikiwa utahitaji nikuagizie ni 5000 kila box
*****************************************************************
Gharama kiujumla
Bei ya box 60000+Usafiri 40000+Mimi 5000=105000
105000x20=2,100,000 Gharama Kiujumla
Unaweza kulipa kwa hatua tatu
1.Bei 60000x20=1,200,000 hapa tunanunua na kuanza usafiri
2.Usafiri 40000x20=800,000 unalipia baada ya mzigo kufika (siku 30-45 tangu siku ya manunuzi)
3.Gharama zangu 5000x20=100,000 unalipia baada ya kupokea mzigo wako
******************************************************************************
Biashara Hii Bongo
Bei Kwa Jumla (box 5) kila box 125,000-130,000
Bei rejareja (box 1) 150,000-170,000
********************************************************************
Karibuni Nitaendelea kupost bidhaa zaidi kulingana na muitikio wenu
Salim Mhina
0713055107
Morogoro Mjini
Mwaka 2018 kuna dada alifunguaga ofisi kabisa mabibo na tin feki na leseni feki alafu akawa anafanya mpka sponsored mbwa yule.

Alitupiga takribani watu 200 hela xetu ambazo tulimpa atuagizie vitu mie nilimpa 300k ya awali ili tv yngu ikifika nimalizie 400k kwa ajili ya samsung inch 60.

Kilichotokea baada ya mwezi na nusu tunaenda tunakuta imefunguliwa saloon ya kike mhusika hakupatikana mpka leo.

Toka siku hyo hata unielekeze vipi ntakusikiliza tu then huyo ntasepa zangu
 
wewe ungempa hela zako akuagizie mzigo???

kwanini asitoe step za watu kuagiza au connection ya makampuni??
na yeye kaja humu kama dalali na wewe mpuuzi mwingine unajifanya unajua
mbona mchanganuo wangu unaeleweka kama unahitaji kuagiza mwenyewe ni bora zaidi kuna soko kama alibaba,globalsource,made in china na kuna wasafirisha kama silent ocean,ngoka,tosh,unique,mapembelo so hapo unaweza kujitusu mwenyewe.
 
Tunalipia kwa njia gani? Na vipi kama nataka kuagiza zaidi ya box 100, hakuna discount?
malipo yanafanyika bank kwa discount zaidi ni ukichukua kuanzia box 500 ambapo itakuwa 55000 na utaweza kuwekewa brand yako (logo) kwenye sabufa na box lake (branding)
 
Mtanzania hata umwambie kila kitu na umshike mkono umpeleke bado atajisemea umemset, kwa mizigo midogo ambayo n chin ya USD 2k Mara nyingi transporter hujumlishia gharama za Kodi na usafiri pamoja.

Watanzania Biashara zao Mama ntilie, akijibadili sana boda boda au bajaji rejea mada za humu jf kwa watu wenye mitaji wanaotafuta wazi la biashara
Unajua ni kwanini? Ni kwa sababu Tanzania katu katu hakuna mtu anayetangaza biashara yake hadharani na aonyeshe mahesabu yote na jinsi anavyopata faida nono iwapo ni biashara ya ukweli. Ukiona mtu anakuomba ufanye biashara flani kwani ina faida na akakupigia mahesabu yenye faida nono basi kimbia ufe.
 
malipo yanafanyika bank kwa discount zaidi ni ukichukua kuanzia box 500 ambapo itakuwa 55000 na utaweza kuwekewa brand yako (logo) kwenye sabufa na box lake (branding)
Almost 57ml itahitajika. Hopefully mwisho wa huu mwaka naweza kukucheki ila nataka vitu viwe quality sio mafamba.
 
Unajua ni kwanini? Ni kwa sababu Tanzania katu katu hakuna mtu anayetangaza biashara yake hadharani na aonyeshe mahesabu yote na jinsi anavyopata faida nono iwapo ni biashara ya ukweli. Ukiona mtu anakuomba ufanye biashara flani kwani ina faida na akakupigia mahesabu yenye faida nono basi kimbia ufe.
Tatizo lingine pia tunaojua HATUNA MITAJI
 
Ondoeni utapeli wenu wa kizamani hapa. Shirikisheni ndugu zenu kama ina faida sana.
Kuna mahala nimesema inafaida sana boss....je vipi kama kwa hiyo sabufa unahisi ingefaa iuzwe ngapi bongo au china inunuliwe ngapi
 
WhatsApp Image 2023-09-04 at 22.25.24.jpeg

bei ya sabufa na usafiri toka kiwandani hadi kwa agent msafirishaji kuja tz
WhatsApp Image 2023-09-04 at 22.26.06.jpeg

jina model ya sabufa husika
vlcsnap-2023-06-13-12h27m29s619.png

gharama za usafirisha kwa (inahitajika kufanya mahesabu)
vlcsnap-2023-06-13-12h27m44s771.png

gharama ya sabufa na usafirishaji ni pesa ya china so ili kujua kwa pesa ya tz rate ndio izo crdb StackPath
O1CN01Vwc13U23ZFfkP2XHQ_!!2577257269-0-cib (1).jpg

ukubwa wa sabufa ili kujua gharama za usafirishaji (meli huzingatiwa ukubwa LxWxH sio uzito)

KWA UFUPI UNAPOONA NIMEPOST LENGO SIO KUKUHADAA ILI KUKUVUTIA KUAGIZA BALI HII NI FURSA KWA WALIOKUWA WANAHITAJI KUAGIZA CHINA.MIMI NITABAKI KAMA MSAADA NA HATA GHARAMA ZANGU ZI WAZI LABDA KAMA MOYO WAKO UNAONA UCHUNGU JUU YA KUJITAFUTIA RIZIKI KUPITIA UJUZI WANGU.
ZINGATIA USINIITE TAPELI NINGALI SIJAWAHI KUKUTAPELI
KAMA KUNA UDANGANYIFU WOWOTE KATIKA MCHANGANUO WANGU WAWEZA ELEZEA MANA NAJUA WAPO WAKONGWE JUU YA HAYA.
 
Attachments

  • 1693856233819.png
    1693856233819.png
    8.9 KB · Views: 12
Mtanzania hata umwambie kila kitu na umshike mkono umpeleke bado atajisemea umemset, kwa mizigo midogo ambayo n chin ya USD 2k Mara nyingi transporter hujumlishia gharama za Kodi na usafiri pamoja.

Watanzania Biashara zao Mama ntilie, akijibadili sana boda boda au bajaji rejea mada za humu jf kwa watu wenye mitaji wanaotafuta wazi la biashara
Wewe ni Mrundi?
 
Ondoeni utapeli wenu wa kizamani hapa. Shirikisheni ndugu zenu kama ina faida sana.
Baki na fikira zako za kimasikini hivyo hivyo. Toka nenda hata silent ocean pale au gnm cargo au Kilimanjaro kafanye utafiti utaambiwa. Na pesa ya usafiri hulipwa mzigo ukifika warehouse ya msafirishaji hapa Tanzania.

Sasa wewe badala ya kujifunza umekadhania utapeli tu, jinga kubwa wewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimekupeperushia njiwa wako?
 
Back
Top Bottom